Uchambuzi wa Albam: Chapters
Msanii: Abudabi Tembekali
Tarehe iliyotoka: 30.01.2021
Nyimbo: 9
Watayarishaji: Judah “K Dawg” Ndaaku, Musa Okoth
Mtayarishaji Mtendaji: Mtaa Afriq Organization/Abudabi Tembekali
Mchanganya Sauti Na Midundo: Shaky (Mandugu Digital)
Studio: Angaza Studios, Truce The Label,
Wiki jana niliamua kucheki gumzo la Ondu Street Lawyer pale YouTube kwenye channel yake Back2Basics Podcast. Kwanza nilianza kuskiliza mazungumzo yake na dada flani muhimu sana kwenye harakati za Hip Hop Kenya, Nimoh Futuristic wa Sauti Za Mabinti na baada ya kumaliza nikaamua kucheki mazungumzo ya Ondu na emcee Elisha Elai. Hapa ndipo nilipomfahamu kwa mara ya kwanza emcee Abudabi Tembekali na mradi wake aliouachia mwaka huu Chapters.
Baada ya kumaliza kipindi nilizama mtandaoni kutafuta project hii na mda si mrefu nikaanza kuiskiliza. Mradi unaanza na ngoma nzuri sana inayopiga gita zuri sana uitwao Time. Wimbo ni mzuri sana unaoelezea magumu ya maisha anayopitia maishani mwake na vita anavyopitia kichwani kwake kwenye hii safari ya maisha.
Japokua mradi huu ni mfupi wenye nyimbo tisa una nyimbo kibao mzuka sana kama wimbo unaokuhimiza na kukutia moyo akikwambia kuwa sasa ni Wakati Wako. Kwenye boombap flani old school Tembekali anakutia moyo akisema kwenye ubeti wa pili,
"Weka doubts away na uzipee 1 hundred na 10 percent extra/
Usi sound too desperate wacha ku ngoja binadamu wata ku fail ni nature/
Tenda wema pace thank me later/
Sidai praise Zi save for Sunday church/
Beware ni exam watakugeuza crush dummies kushinda test za kebs ah!/
Sema loudly heads plus hands up/
Miguna Miguna step back kwa plane sir!/
Walikataa kukupee pass ki Fred JKIA 48 hours waku detain ah?/
Cheza safe ki vault na lock shit up/
CBK Njoroge vile na chase bank/
Take charge ka talk-oh wasini drain batt,
Sitawacha wani hold back again!/"
Wimbo mwingine poa sana nilioupenda sana ni Sleepless unaomkuta Abudabi akikataa kulala hadi afanikishe ndoto japo kua ndoto huja usingizini, Dunda Na Me ambao unamkuta emcee huyu akijigamba vile ana uwezo wa kuamsha umati kwenye tamasha.
Kwa wale watafutaji wimbo wenu ni Sauti Ya Dough (Pesa) akiwa na Ma Buruguda, akisema Tembekali kwenye kiitikio,
“Shinda hustle Kila dakika/
Sauti ya doh Ina niita/
Ma ngori hazita ni bakisha/
Sauti ya doh Ina niita/”
Nyimbo nyingine kama Hizi Machuom ambayo ni wimbo wa kula bata, Everyday ambao ni wimbo wa utafutaji
Wimbo wa mwisho Chapters ambao ndio umebeba jina la mradi huu. Wimbo unapiga vizuri kwa vinanda na bass gita na vinanda wazimu sana. Hapa unaskia kidogo kuhusu maisha ya Tembekali binafsi, changamoto anazopitia na matumaini yake kuhusu siku za usoni.
Uchimbaji wa handaki leo umenifikisha mpaka D kwa Abudabi Tembekali. Nimefurahia kuskiliza mradi wake Chapters na nadhani wewe pia ukiuskia utakubaliana nami kua ni mradi mzuri.
Facebook: Abudabi Tembekali(Abudabi)
Instagram: abu_tembekali