Africa ni taifa sa ki vipi waigawanye,
Kama walitukuta watakuwaje wafalme,
Hawa wajinga walijivisha nyadhifa,
Alafu viongozi wetu wakawaita ma Chifu,
Wauwaji kama Leopold, Congo,
Ma milioni ya watu walifukiwa kwenye udongo,
Sambamba na ukatili kama kukatwa mikono,
Na kutumikishwa hakuja fikaga kikomo,
Migodi ya Sauzi vibarua ni wazawa,
Licha ya kazi ngumu walichukua roho zao,
Almasi na dhahabu zenye damu,
Mateso mbalimbali ya mababu kwenye mashamba,
Mi napata moto kwa hakika,
Hasa inapofika siku ya mtoto wa Africa,
Kaburu, kutafuta uhuru kwani kosa,
Na walilia watoto wa ki Zulu na ki Xhosa