Verse 1:
Ninakupa, Na Nitakupa Sifa Mara Zote/
Ya Kwamba Umebarikiwa Kupita Mabara Yote/
Hebu Tafuta Kwa Kutazama/
Sidhani Kama Utakuta, Hakuna Wa Kufanana/
Historia Yako Naijua Ni Kubwa Sana/
Tatizo Walioandika Wanazusha Wanatuchanganya/
Wangeweka Wazi Ungeichukua Chati/
Maana Bila Wewe Wenyewe Wangekua Wapi/
Wakizuga Hawakumbuki Na Wengine Kuuchuna/
Wakumbushe Ile Miaka Mia Nne Ya Utumwa/
Ndo Maana Nasema Siwazimii/
Wakiuliza Nini Shida, Buffalo Soldier Naiweka On Repeat/
Walichukua Vyetu Wakatuchukua Peku/
Na Walichotuachia Eti Kumjua Yesu/
Na Bado Wanakuponda Umefulia/
Ila Plan Nilizonazo Watakonda Watatulia/
Chorus:
Ninakupenda Kwa Moyo Wote/
Nataka Upande Sio Uporomoke/
Nakupigania Urudi, Uwe Kama Zamani/
Nikusifie Uzuri Nikitazama Ramani/ X 2
Verse 2:
Kwanza Kiapo Cha Moyo Kwenye Nafsi Iliyonyooka/
Halafu Wa Ndani Amlete Hapa Aliyetoka/
Kweli Tumekwama Mpaka Kuambiwa Giza? /
Au Mawazo Kama Haya Yatakuchania Visa? /
Weka Elimu Inayotufaa Sio Elimu Ya Mkoloni/
Walimu Na Vitabu Na Sio Simu Za Mkononi/
Hali Inabadilika Mi Nadhani Mnaelewa/
Tukipinga Mabadiliko Dhidi Ya Hali Ya Hewa/
Tukiamua Kuwa Na Mawazo Endelevu/
Hatushindwi Kufumua Kila Mfumo Tegemezi/
Tupinge Mitazamo Ya Kilafi/
Tubalance Malighafi Na Mgawanyo Wa Nishati/
Sio Mpaka Mlami Ndio Tuwe Bab Kubwa/
Ubora Uliwepo Kabla Hata Ya Wao Kuja/
Tuzalishe Vya Kwetu, Vile Vyenye Ubora/
Ving'ora Vya Bei Tuwalizie Wakora/
Chorus:
Verse 3:
Ah! Hamuoni Hata Uchungu Kwa Mtima/
Nyadhifa Ni Za Muhindi, Mzungu Na Mchina/
Kisa Kujengewa Madimbwi Mabwawa/
Fikra Kama Macho Ya Shinji Kagawa/
Mzalishaji Mkuu Mwanamke Muinue/
Kazi Hadi Ajira Hizo Fikra Za Uziue/
Fufua Na Vumbua Vipaji Vya Ugunduzi/
Miundombinu, Ya Ndani Kwa Ndani Iwe Vizuri/
Watu Walivuja Damu Ili Tupate Uhuru/
Si Hata Jasho Hatuvuji! Tunakufuru!/
Na Zile Siasa Za Upande Mmoja/
Ni Za Kuacha Na Vibaraka Wasake Boda/
Tuanze Na Hayo, Mengine Yatajipanga/
Kilichonishawishi Hadi Mimi Nitaje Haya/
Natamani Siku Moja, Nitazame Nyuma/
Nione Afrika Ya Gaddafi Na Ya Kwame Nkurumah/