Toka kwa: Ambecal AMC
Wimbo: Mtaa Kwa Mtaa
Kanda Mseto: Rap From Ambecal (RFA) – Vol 1
Tarehe iliyo toka: 2017
Mtayarishaji: Moodhood
Studio: One Nation Music Group (Mwanza)
Beti ya Kwanza
Toka kijijini nawasili mjini/
Mwanza Mwanza ntaanzia wapi kifikra nkitathmini/
Uku nimekula bati bati na mimi/
Mara hakaja jamaa akauliza kwani we unaishi Mabatini/
Nkamwambia hapana mi hapa mjini wa kuja/
Sijui lugha naninapoelekea ni Buzuruga/
Pia hata nakotoka sikumbuki /
Ngependa unitembeze maeneo tofauti/
Fresh tukaenda uku uwoga shaka ni zuru/
Akaniambia husiofu sababu hapa tupo mtaa wa Uhuru/
Mara giza nkamuuliza mbona mwanga hautoi/
Akaniambia sa huu ndio mtaa wa Makoloboi/
Hoi ghafla alinishanganga aliposema /
Eti mbona kuna wabaya wanaoishi mpaka Mji Mwema/
Wenye hurka shtuka ili husije juta/
Na wala husifanye pupa huu mgeni husije umbuka/
Ndipo nilipo shtuka baada ya kuskia kwa Msuka/
Nilijua labda ni jini pengine naenda kufa/
Akaniambia haya ndio majina ya hapa mjini/
Haina haja ya kushangaa ila unapaswa kua makini/
Kiitikio 1
Huu ugeni! Mgeni Mwanza
Nakutana na ugeni wa majina ya miji ila
Kiugeni sijisemi kama mshamba
Ila majina ya miji mwenzenu yananshanganza
"Mwanza" Mwanza
Nahii ndio
"mtaa kwa mtaa"
*nimepita Pansiasi kote Mihama, Mabatini
Yani"Mtaa kwa mtaa" mitaa yote ya kati Nyakato, Igogo mpaka Mbanda Chini
"Mtaa kwa mtaa" na kwa utafiti asili ya uwepo wa hii mitaa nshaibaini
Ndani ya "Mtaa kwa mtaa" na hii ni story fupi ile siku nlipofika Mwanza mjini
Beti ya pili
Tukazidi songa kimkato na penyo/
Mwanza ni city ila nlishangaa kusikia Nyakato kuna National/
Tukapita Meko kurudi gheto/
Usiku kucha ukapita mpaka ikafika kesho/
Hasubui uku breakfast imedorola/
Ilinishangaza na mahali tulipo ni Chai Bora/
Akaniambia twende Nyamanoro au Nyamagana/
Nkamwambia dah! Kokote cause mi uwa napenda sana nyama/
Nilishangaa sana nkashika tama/
Nliposkia eti kuna mahali panaitwa Ghana/
Nlifikiri labda nchi kumbe hapana/
Ni maeneo tuu ambayo uku kiuwepo yanapatikana/
Nlitikisa kichwa nkamwambia fikra/
Nimeijua Mwanza ila majina ndio yanayonidatisha/
Mpaka nimekosa furaha kabisa/
Akaniambia basi kama ndio hivyo twenzetu uwanja wa Furahisha/
Ukafurahi/
Kiitikio 2
Huu ugeni! Mgeni Mwanza
Nakutana na ugeni wa majina ya miji hila/
Kiugeni sijisemi kama mshamba
Ila majina ya miji mwenzenu yananshanganza/
"Mwanza " Mwanza
Nahii ndio
"Mtaa kwa mtaa"
*Nimepita kila kona Igoma Buhongwa mpaka Kishiri
Yani "Mtaa kwa mtaa" pande zote Bugarika, Nella, Illemela ata Kitangiri
"Mtaa kwa mtaa" na kwa utafiti asili ya uwepo wa hii mitaa nshainakili
Ndani ya
"Mtaa kwa mtaa" na hii ni story fupi Mwanza mjini ile siku nlipowasili