Wimbo: Explore And Exploit
Toka kwa: Amphoterick Tz ft. Robert Mugabe
Mradi: Single
Tarehe iliyotoka: 31.05.2022
Watayarishaji: Wise Genius & Ommy Pah
Mixing & Mastering: Ommy Pah
Studio: MV09
Beti Ya Kwanza
Walikuja na mashua ama meli toka Ulaya/
Wakatukuza wake zao, wa kwetu wakawaita malaya/
Dini zetu za mababu zikawekwa kapuni/
Wakatuambia tukitii mamlaka tutafika mbinguni/
Kilichotuponza ni ukarimu wa kiAfrika/
Ndicho kinacho tugharimu hapa tulipofika/
Bara la kiza lenye mito na mabwawa/
Misitu yenye kila miti ya kuzalisha madawa/
Achia mbali hayo madini na hizo mbuga/
Afrika tuna nyanda za kutosha tukiamua kufuga/
Bahari za kutosha tukiamua kuvua/
Kudadeki mabeberu mbona watatutambua! /
I bring it back to the majesties/
Back to where Rap is, Africa your skin reflect the necessity/
Come back home and review the history/
Men we’ve got the remedies that cured the mystery.../
Mugabe: “If Dogs and Pigs know their Mates, can human beings remain human beings if they do worse than Pigs. There will never be a regime change here; there will always be the people of Zimbabwe”
Beti Ya Pili
Ukoloni mamboleo ama Neo-colonialism/
Ndiyo huu nau-adress kwenye rhythm/
Awe mChina ,Mzungu ama Mhindi/
Chunguza utagundua maslahi yake ni ya ushindi/
Ardhi yetu vijakazi wenyewe/
Ndugu zao wabaguzi wamewekwa watusimamie/
They divide and conquer, wanaleta farakano/
Hazina yetu inasepa tukiendeleza mapambano.
Kwa wa-Tz,Warundi, Wakongo mpaka Rwanda/
Unamjengea shetani ghorofa ,unaishi kwenye banda/
Huna uhakika wa misosi mpaka teknolojia/
Saayansi yetu si uchawi, washasimangia..
Tuungane kwa pamoja tuna nguvu/
Utajiri wa kutosha wanaye Mungu sisi tunayo Miungu/
I bring it back to the majesties, back to where Rap is Africa/
Your skin reflect the necessity, come back home and review the history/
Men we’ve got the remedies that cured the mystery/
Mugabe: “The Western countries in particular the United states and European union, who impose illegal sanctions against Zimbabwe as to our surprise and that of sitic and the rest of Africa, refuse to remove those sanctions.”
Beti Ya Tatu
Jisahaulisheni kuhusu mashujaa wa kiafrika/
Kwa nadharia uchwara mboni zetu zafunikwa/
Simika nguzo, chinja mbuzi fanya tambiko/
Amsha mababu wakusikie wazuie mafuriko/
Ya maradhi ma umaskini,ujinga piga chini/
Waafrika tuna mitutu tumekosa magazine/
Namaanisha uthubutu ndiyo silaha tumeweka chini/
Tubadili mitaala isadifu uhalisi/
Sio hizi theories, vitendo vinakosa ufanisi/
Ikiwa dunia kijiji, mipaka izingatiwe/
Mwanajeshi funga mkwiji,tusisalitiwe/
Vibaraka wanyongwe, wanakosesha matonge /
I bring it back to the majesties/
Back to where Rap is…Africa/
Your skin reflect the necessity, come back home and review the history/
Men we’ve got the remedies that cured the mystery/