Msanii: Andre K (Rest In Power)
Extended Play (EP): Elimu Yaa Juu (EYJ)
Tarehe ya uzinduzi: 05.06.2017
Utunzi wa biti: Sam Chad, Slim Sal
Nyimbo: 4
Mara moja moja hua anatokea mtu mwenye kipaji cha uchanaji kule chini kwenye mahandaki ya hip hop. Wanaopata kumsikia wanajua kua mtu huyu akiendelea vizuri kukuza kipaji chake kwa nidhamu anaweza kuwa mwalimu mzuri kwa wanafunzi wa falsafa ya hip hop. Marehemu Andrea Peter Kimolo (Andre K kwa jina la kazi) alizaliwa mwaka 1990. Busara zake za uandishi ulimfanya atambulike kama Rap Suleman. Kipaji chake kilianza kutoa miale akiwa mdogo na japo kua alikua mwalimu wa shule ya msingi alikua na kipaji cha ziada, mhathiri wa chuo kikuu cha hip hop.
Ilikuonyesha kua umri wake ki hiop ulikua umeenda tofauti na umri wake wa ki mwili aliamua kuanza kufunza wana hip hop Elimu Ya Juu tarehe tano Juni 2017.
Extended Play (EP) ya Elimu Ya Juu (EYJ) ipo na units nne ambazo mwanafunzi anatakiwa azisikilize kwa makini, azielewe na akihitimu apewe shahada yake
1.“Nenda kasome” ikifunzwa pamoja na Slimsal
Baada ya muda mrefu wa maombi mchumba wa Andre K amefikiwa na kuitwa kwenda chuo kikuu. Japo kua Andre K hakuwahi ona mlango wa chuo kikuu amejawa na bashasha kwani mpenzi wake amepata fursa yakuendelea na masomo yake. Anamwambia hivi,
“Usione nipo kimya sio hasira, ni huzuni/
Pia ‘na furaha umepiga hatua nzuri/
Nilikesha nikisali kukuombea matokeo/
Mungu amefanikisha, unakwenda chuo leo!”
Andre K pia hasiti kumpa mpenzi wake tahadhari anapokwenda chuo kwani anahofu shemeji yetu anaweza kwenda chuo na akabadilika. Anamuonya akisema,
“Hofu yangu kubwa usjie ukaleta vituko/
Upendo usije zama kisa ubize na umbali/
Tukaja tengana nikaulizwa na nyumbani/
Wote wanakucheki, mkwe na shemeji zangu/
Usije ukawaangusha na huu ndio wosia wangu…”
Pia anampatia tahadhari mpenzi wake kuhusu maisha yanayo msubiri kule chuo,
“Unaskia, huko kinacho matter mitandao/
Wasichana wanaiga, hawajali miili yao/
Jitunze, ukaishi na taratibu za kidini/
Ukumbuke kwamba kuna swala la ukimwi…/”
Pia anazidi kuweka msisitizo zaidi juu ya tahadhari alizo toa hapo juu anapo malizia vesi ya pili,
“Usije badili na mitindo ya mavazi/Naskia waathiri hata penzi wana hitaji!”
Je mrembo wake ataskia?
2.Karibu chuo ikifunzwa pamoja na Big Thinker, Slimsal na Therapist
Mpenzi wake Andre K anaingia chuo na kukaribishwa na bango kubwa pale getini lililo mwambia, “Karibu Chuo!” ila waadhiri wanamkaribishia kwa kumwambia,
“Maisha huku, Tough! Tough! Tough! Tough! /
Pesa zina kata Chap! Chap! Chap! Chap! /
Ukiwa na akili Chaf! Chaf! Chaf! Chaf! /
Kawaida tu ku Sup! Sup! Sup! Sup!”
Pia anapofika shuleni waalimu wa michano wanoa msaidi Andre K bado wanampa hali halisi ya maisha ya chuo. Wanamwambia kua tofauti ya chuo na shule ni wanafunzi kutovaa sare,
“Kwanza kabisa huku hakuna uniform/
Skin, jeans na vi mini hii ndo skuli bro! /”
Pia wanaendelea kumtahadharia binti kua chuo kikuu usipochunga kila siku ni kula bata ila mathara yake yapo,
“Ushafika huku homy, huku fully bata mpaka, kuku yaani/
Utakula starehe, shida mpaka ziku laani/
Piga chini boyfriend, kuna sponsor waku kukunanii…”
Na haya yote anakwambia yanaaweza kufanya ukarudia mtihani, ukapata supplementary,
“Visa vya wakufunzi na washkaji kisa dame/ Kuna walo sup kisa fame!”
Maisha ya chuo atakayo ishi dada yetu yatategemea na maamuzi atakayo chukua.
3.Kachetuka ikifunzwa pamoja na Adam Shule Kongwe(A.N.KO)
Baada ya mda mrefu ya shemeji yetu kwenda chuo ameanza kua na hofu kuhusu mpenzi wake kwani amekua kimya tangu aende chuo. Ana amua kumtafuta mshikaji wake “Kongwe” ambae nae alifaulu kwenda chuo kimoja pamoja na mpenzi wa Andre K.
Baada ya kusahabiana na kujuliana hali mshikaji anaanza kumueleza vile binti alivyo kabadilika alipo fika chuo. Wanaanza kumjadili biniti,
“Andre K: “Shem wako sahii hivi wapi? /
Adam Shule: Nikuulize wewe maana haonekani classi/
Andre K: Ulisema kozi mnasoma watu nyomi/
Labda alikaa mbali na ukawa haumuoni! /
Adam Shule: Si leo tu, jana hadi teacher alimuulizie,
Ngoja nichukue menu na kisha nakupigia! ”
Rafiki yake anaanza kumueleza yaliyo jiri kwa binti huyo na kusema vile awali alikua binti alie penda masomo ila alikuja badilika baadae hadi kuanza kuenda na waathiri wa chuoni pia,
Kongwe, “Semester ya kwanza alikua top of the college/
Shortly akazingua naku drop pole pole/
Ilikua baada ya class na maktaba ilikua ni pori lake/
Katukimbiza sana ukipita ni stori zake”
Ila alibadilika ghafla,
Kongwe, “Utamshikia wapi, magari yana cross daily/
Anabebewa mpaka simu na wanamuita boss lady!”
Na hadi alishaanza kutembea na waathiri,
“Ma lecture wengi wanampata vilivyo/
Manzi wako usimpime, kakamata kitivo!”
“Manzi wako usimpime, kakamata kitivo!” pia inaonyesha vile lugha ya Sheng ya kutoka Nairobi, Kenya imepenya hadi vyuo vikuu Tanzania. Manzi ni jina analoitwa mrembo, binti au msichana mzuri.
Kwenye vesi ya mwisho mshakiji wa Andre K anaamua kufunguka vile binti alivyo badilika ila aliendelea kumpa matumaini kuwa pengine binti bado anampenda,
“Unathan utani man, manzi kachetuka na ndo hivyo/
Sema huenda nafasi alikupa bado ipo! ” /
Akili yake haikuwa tena masomoni,
“Course work, wala haimstress, haisumbui/
Hawazi cha assignment, test wala UE”
Andre K anabaki kachanganyikiwa hadi kakataa kumuamini mshikaji wake ki Tomaso na zaida ya hapo anakufuru,
“Kesho nashika basi, mwanangu bora nije/
Sikuamini kabisa, mamaangu mwanamke”/
4.Bora usinge enda shule… Ikifunzwa pamoja na Slimsal
Andre K amebaki na majuto na masikito kwa nini mpenzi wake alienda kutafuta Elimu Ya Juu. Anaona ni bora hangeenda shule kwani elimu imemponza binti huyo. Binti kabadilika hadi basi,
“Umebadilika tangu ufike huko chuo/
Hakuna call, hata SMS kwa mkupuo/
Upendo umeshashuka kama vile uchumi/
Hauniwazi tena, baby girl ushani do me! /
Nikipiga mimi mara uko discussions/
Kati ninacho skia ni sauti za ma champagne! ”
Andre K kabaki na huzuni kwani elimu kubwa imempa binti akili ndogo. Anaendelea kulalamika,
“Upo lecture au uko lodge na lecture? /
Una paper au ndio unanisebenza? ”
Maswali kibao anauzila K kuonyesha vile uaminifu haupo tena kati yake na mpenzi wake.
Elimu Ya Juu inaonyesha vile masomo ya chuoni ni mazuri ila changamoto pia zipo. Mtu anaweza faulu na kuhitimu na shahada yake bila tatizo au anaweza shindwa kujizuia na kufuata vishawishi vilivyo jaa vyuoni na akatoka chuo na akili pugwani kuliko alivyo ingia chuo. Andre K anatuonyesha kua mtu anapo kwenda kusoma chuo anahitaji ku kua ki elimu na ki utu pia.
Ukitaka pata hii EP ya marehemu Andre K wasiliana na Adam Shule Kongwe Hamisi
Cc: Javan Guevara Miracle Noma Kanja Wizle Marshal De