Toka kwa: Bad Ngundo
Wimbo: Nidhamu Pesa
EP: MB
Tarehe iliyo toka: 01.06.2021
Mtayarishaji: Mtata
Studio: Soweto Records
Beti ya kwanza
Huna nidhamu ya pesa/
Kitaalamu tunasema ni utani unaleta/
Utatafuta kwa tabu/
Ukipata unachafukwa ghadhabu/
Unaponda Mali/
Unatumia bila kuona hali/
Unashika noti unachoma nari/
Ukiwa nazo unasema watakukoma man/
Unachafua meza/
Unafunga bar unaanza kueneza/
Kuna bajaji ya Mia tano unapanda boda/
Unalipa buku ambayo hata ingechanga mboga/
Ufujaji wa pesa/
Nakuiadharau shiling ambayo ilio kutesa/
Ilio kutoa jasho/
Ukaifanyia kazi ulipopitia haso/
Ingekufaa badae/
Ungenunua hata shati ukavaa ung'ae/
Unahonga laki/
Kesho yake unaomba bati/
Huo ni upunguani/
Kwa pesa ndogo unayasahau machungu Yani
Beti ya pili
Tunza pesa ikutunze/
Ukitumia kidogo weka kingi usibumbwe/
Tunaenda hivo/
Kukosa nidhamu ya pesa nikuingiza matatizo Mzazi/
Acha hizo udwanzi/
Ukikosa unashika tama/
Tatizo lako ukipata unaamini tena kukosa inashindikana/
Hilo ni kosa/
Unajipotosha/
Nafasi yako ukidondosha watu wanaokota/
Ulikua tajiri urudi kua lofa/
Jifunze kudunduliza/
Epukana na staree za kufuliliza/
Kipochi unakunjua unanunua chips kuku/
Zumbukuku ili mademu waku busu/
Ukijitusu mfuko unabaki nusu/
Faida inakua kwake hasara kwako usiruhusu/
UJINGA,yatakuja kukushinda/
Jua shida haina bingwa ukitingwa/
Utalaum watu mambo yako ukishindwa
Beti ya tatu
Ngundo: Acha , naku pleas hayo sio matumizi/
Unatumia pesa mingi Kwa kusizi/
Kwanini usifanye mtaji ukakidhi/
Mahitaji usiishi ilimradi unahisi Una nyingi/
Kuna muda zitakimbia/
Ukiwaza kufikiria ulizitumia vibaya utalia/
Mfumo wakuzitoa pangilia/
Na kama unazo zitunze, usiyumbe wala mjumbe usidilibadili tabia/
Usihamasike, na nyimbo za wasanii eti wana wanywe bia/
Ukawa unamwanga chenchi upate sifa kumbe unaumia/
Kesho unagongea fegi huna kila Mia/
Kama mywaji wenzako wakinunua unatamani ukate pegi wanakubania