Album: Mcheza Kwao
Msanii: BCP Wage
Nyimbo: 15
Tarehe Iliyotoka: 30 Novemba 2020
Utayarishaji wa beat | Producer | Mixing na Mastering: Palla Midundo
Mcheza kwao hutuzwa walinena wazee wetu wa kale. Ni msemo huu ulio msukuma BCP (WAGE) kuamua kucheza nyumbani; si Tanzania au Africa Mashariki bali Africa. BCP ameamua kuongea na Africa, na Waafrika kwa kutumia lugha ilio na waongeaji wengi Africa nzima, Kiswahili.
Na lugha ya Kiswahili ndio ilio unganisha kundi alimotoka BCP liitwalo Swahili Genge ambalo lilimpa BCP jina lake WAGE yani Best Combination Punchers(BCP) Wa Swahili Genge(WaGe); BCP WAGE.
Baada ya kuanzia uchanaji akiwa shule ya upili kule Morogoro mjini akiwa na wanafunzi wenzake, Leonard Mwinuka kama anavyo julikana rasmi alikoshwa na fani hii na akaamua kujitosa mazima kwenye fani. BCP aliendelea kukuza kipaji na akafanya kazi na MC’s kibao.
Kisha wakakutana na producer Palla Midundo. Japo kua nia ilikua ni kutengeneza kibao kimoja na producer huyu BCP aliona vile chemistry yake na Palla ilivyo nzuri akaanza kuwaza kuhusu kufanya Kanda Mseto(Mixtape) na baadae likaja wazo afanye album ambayo beat zote zimetoka kwa Palla. BCP ambaye ana Stashahada ya madawa ya binadamu (Diploma in Pharmacy), akaachia album yake ya kwanza inayo jaribu kutibu magonjwa yanayo isibu Africa yetu. Album hii ni dozi kamili kwa mashabiki wa hip hop kote Africa. Jitibu kwa kupata naka yako.
Dozi hii ya Mcheza Kwao ina nyimbo kumi na tano ambazo ni zaidi ya dakika arobaini na tano ya tiba. Ina vidonge vifuatavyo;
1. Mcheza Kwao
Nyimbo hii ndio ime beba jina la album na ina tukumbusha kua Mcheza Kwao hutuzwa. BCP anatupeleka nyuma ki historia kabla ya wakoloni kuja na ana tuonyesha vile tulikua na mila nzuri na utariji wetu asili ambao chanzo cha kuvurugika ni ugeni uliokuja kwetu. Ugeni umetuponza hivi,
“Majaribio yasiyo na mpango,
Zinatuuwa chanjo,
Uzazi wa mpango,
Dawa chini ya viwango,
Afrika ndio kama dampo,
Haya siyo mambo,
Bora tuwafungie milango,
Ki vyetu tuka struggle,
Tuishi kama kitambo,
Enzi za Mtemi Mirambo”
Kupia nyimbo hii BCP anatufunza kuhusu hisrotia ya viongozi wetu wakubwa wakitambo kama Mytela Kasanda(1840-1884) aliekua akijulika vizuri kama Mirambo.Mirambo alikua ni Mtemi(mfalme) wa kabila la Nyamwezi wa ufalme wa Urambo. BCP anataka tutafiti historia ili tujue vizuri tulipo tokea.
2. Usikate Tamaa
BCP ana amua kumtia moyo mtu yoyote anaye pitia magumu maishani mwake akisema,
“Hizi ni changamoto tu,
Za dunia hii,
Zitapita tuu,
Usikate tamaa!”
Chamsingi anasisitiza tumgeukia mwenyezi Mungu ambaye ni mweza yote kuliko kuwaza mabaya,
“Kuepuka misala,
Usisahau sala, uendapo kulala,
Kwenye zako biashara,
Zakusaka jala,
Siku hizi binadamu pia wanatolewa kafara!”
Ana endelea kusema,
“Usitamani ku kaba,
Usiwaze ku danga,
Bado una mtoto mchanga,
Tandika chini kanga,
Panga hata karanga,
Achana na waganga,
Mume hatafutwi kishamba,
Kwa dawa za miti shamba,
Usizuzuke na pamba,
Wengi wana lalia chaga,
Usiwaone wajanja,
Maisha yao majanga! ”
3. Rudi akimshirikisha Uranium
Mwanamme akilia ujue kuna jambo. Wimbo huu unampata BCP akilia na beat likilia nae. Kilio chake ni kwa mpenzi wake arudi baada ya wao kuachana kwa mda. Mpenzi wake alimucha kwa hili,
“Ukichagua sana utachagua koroma,
Uzuri wako uta utia doa,
Kisa sina pamba, navaa kishamba,
Ndio sababu yakuniacha,
Naisoma namba”
Na japo kua mpenzi wake amemuacha anampa tahadhara kuhusu wanaume anao watafuta kule nje,
“Angalia anae kufaa wakukuvisha pete,
Sio mpaka apendeze ndio useme twende,
Wengine wana maradhi,
Yamefichwa tu na mavazi.
Baadae utanikumbuka,
Mi ni sie na kazi!
Starehe zina mwisho,
Tena ukicheza sivyo,
Mwisho wake kifo,
Sio kutoa jicho! ”
Mwana mama huyu kamuwacha BCP akitapatapa ka mfa maji. Kwenye beat hili Palla Mdundo anaonyesha vile yeye ni mtunzi mahiri sana.
4. Morogoro akimshirikisha Ephraim
BCP ni mzaliwa na mkaazi wa Morogoro, Moro Town, mji kasoro bahari. Hivyo lazma awakilishe kitaa chake na anausifia kinoma,
“Nimetembea, mikoa flani,
Hapa nyumbani,
Mpaka nchi za jirani,
Hakuna nilio utamani
Huwezi amini mani,
Mpaka mlangoni lami,
Yani kama Miami! ”
Kama Nairobi hayati Kambarage Nyerere alisema ni Half-London, BCP anasema Moro Town ni Miami. “Welcome to Miami” anasema Fresh Prince of Bel Air wa Morogoro!
5. Nafanya Ninachopenda
Je BCP anpenda kufanya nini maishani mwake? Hapa JCP anafunguka yeye ni mtu wa aina gani…
“Sina beef na bongo flava,
Hata hela wakitengeneza,
Wapate show uingezera,
Wajaze arena,
Press conference Serena,
Mi nafanya ninachopenda,
Na mambo yangu yana enda”
BCP kwa nyimbo hii anataka ujue yeye ni real na anamalizia akisema hivi,
“Si mtu wakujisifia, kwa mchizi, maduu pia,
Pia hua spendi, maisha ya kuigiza,
Kujifanya mnyamwezi sina uhakika wa viza,
Mistari si sifu Pizza,
Wakati ni napo lala giza,
Si edit picha kama nime piga Ibizza,
In short hua si feki,
Nyie wenyewe si mna cheki,
Napiga kali vesi,
Na sijioni cake”
6. Usinishauri
Je BCP ni kweli hapendi kushauriwa? Ni kweli hapendi kushauriwa ujinga tu. Usinishauri ni nyimbo ambayo BCP anawachia hisia zake kwa vesi bila kiitikio. Anatuonya hivi,
“Nashaurika ila kuna baadhi ya vitu napinga,
Nafahaamika,
Usinishauri ujinga,
Usinishauri kuimba,
Nime amua kua Yanga, usini shauri Simba,
Usinishauri handaki, mainstream ili kushinda,
Mana hizi harakazi hazija wai kunilipa.”
Pia ana malizia kwa shout out kwa kikundi chake cha Swahili Genge akisema,
“Usini shauri niwe solo artisti,
Bila Genge, WAGE ungemjua vipi?”
7. Massacre
Massacre ina violin strings mzuka sana kwa beat. Juu ya violin hii BCP ana massacre ma MC feki. Nyimbo ni msiba wa ma MC fake. Ana waonya ma MC nguvu ya soda wawe makini,
“Wakija kichwa wana dundwa wana choka,
Wakijificha mi nachoma kichaka,
Mi si tozi mi nishakaa sana mtaa,
So msinletee za ki star,
Ma facka, massacre
Huu ndo mda mwafaka,
Wa ku mada ma rapa,
Marapa wa ma radar,
Hawana mchongo wanazubaa,
Wana shangaa Wage balaa,
Wanavyo tambaa na watakaa!”
BCP ni mbabe wa hili rap game.
8. Usiharibu order akimshirikisha Paragraph
Bata lazma ukiwa kitaa na BCP anaonyesha mara moja anajiachia kwenda viwanjani na hakuna wakumzingua. Paragraph toka Swahili Genge anampa msisitizo waiter akisema,
“Waitress samahani usiharibu order,
Beer hatutaki tunataka soda,
Waiter, kwanza ngoja,
Sisi tuna taka chips-mboga,
Tume paki Mercedes, tume paki Renji,
Tume paki wengi,
Money on hand, hatufati benki,
Tupe tunacho taka, then keep chenchi!
Mi, ugomvi sipendi,
Swahili Genge kubwa limekuwa trendi”
9. Tumechafukwa akimshirikisha Adam Shule Kongwe
Kwa wimbo huu Wage amemshirikisha Adam Shule Yao ambae kama kawaida yake ana mistari makini kwenye beat ambalo lina speed ya gear namba tano.
Kuchafukwa ni neno la mtaani linalo maanisha kuwa na akili ambayo si yako, kufanya mambo bila kujali mtu, mambo ya kikorofi au ya kibabe. Baada ya kutofanikiwa kuwa kwenye remix ya Punch Norris ya Adam, BCP hatimaye alipata fursa ya kufanya kazi na Kongwe ambae aliweka vesi moto inayo muonyesha vile yeye ni mbabe kwenye hili game,
“Hata tusipo sema tumechafukwa kama,
Wee elewa mda wote tumechafukwa sana,
Tukitaka kuchana hatujiulizi,
Ukituona kwenye show, fanya kama tulivyo,
Tuna rap sana ndio mana hawa tuigi,
Wanajua wataishiwa ndio mana wana bana matumizi,
Wakitema utumbo nawatoa na vichwa,
Na watoboa macho kupoteza ushahidi”
Nae BCP haja achwa nyuma,
“Wanashinda bar, kama bapa,
Hawana ujanja ma rapper,
Wanaliwa kama papa,
Sababu ya bata,
Ni ku fowardie picha zao?
Washa data, na wa paka matha f*cka,
Wame yataka, Wage panga nawakata,
Hata kama mmejipanga msiniparamie,
Master,Nakalisha umati,
Naweka vina kati,
Hata mkija tag, hamni weki mtu kati,
Msilete za ki waki,
Kwa mc ambae anaishi kama Paci”
Je una uwezo wa kusimama kichwa kwa kichwa na MC anae ishi kama 2 Pac?
10. No Mercy
No Mercy bado ina endeleza maangamizi yaliyo fanyika kwa Massacre. Bado BCP anazidi uwa ma MC hewa. Anasema BCP kua hii ni kampeni ya ku uwa ma rapper feki. Skiza anavyo wawinda,
“Nilipewa habari zenu tangu wiki ya juzi,
Kuna machizi wanajifanya wajuzi,
Wakipita anga hizi hua wana rap nuski,
Siku taka ku gwaya nikafanya uchunguzi,
Na bahati mbaya hua si wakuti,
Leo kama zari kukimbia mme bugi,
Toka mbali naskia zenu sauti,
Na punch zenu zaku vunjia biskuti,
Kufika mimi ndio kuchana mme mute,
Kisa mna jua nikipiga unajua hauinuki”
11. Yes We Can akimshirikisha Paragraph
Huwezi mlinganisha BCP na ma rapper wengine kama vile huwezi kulinganisha FUSO na Yutong. Akichukua kauli mbiu ya rais mstaafu wa America, Barrack Obama, BCP anasema anaweza, YES He Can anasema,
“Kutafuta najua,
Si wa ki sure,
Ila mjini natanua,
Mziki mkubwa, Wage KR Mulla”
Njoo pupa pupa, MC upasuke sura,
Napiga double cross, 1,2 napiga Ndosi,
Napiga goti, kwa Mungu, sio kwa boss,
Rap imenikomboa,
“Ilaumiwe hip hop” kwangu slogan ya kiboya”
12. Mpenzi
Mapenzi yamenoga kwa mwana wa BCP na haogopi kusimulia kua rapper mgumu pia anaweza yayushwa na mapenzi yazamani bado akisema,
“Natamani tena nafasi kwako nipate,
Niambie uko wapi, mapema niku fuate,
Niko alone tangu ili siku ujikate,
Ni me miss, nime miss mate,
Vile vitu vya usiku mchumba sio poa,
Siwezi kuvipata ata kwa dada poa,
Wage mapepe, ila kwako nimepoa,
Ningekua nime oa, ningevunja ndoa”
BCP kazama kwenye dimbwi la mapenzi.
13. Tuongezee
Waiter tuongezee, hazi toshi hizi beer. Bata batani kuku kibandani wakati BCP anaamua kuingia batani tena,
“Tumesha zoea kulala li saa li moja,
Kuamka na hango over,
Kupoteze vinonga nonga,
Sijui lini nilikua sober!”
Hatari.
14. Put Your Hands Up
Huu wimbo ndio single ya kwanza unao tambulisha album. Pamoja na Palla kwenye Mdundo huu wana irudisha boom bap hip hop na anaonyesha vile yeye ni MC hardcore. Kama unakubaliana nae anakwambia “Put Your Hands”.
Iskize na kuipakua hapa - Put Your Hand Up
“Walisha ni hofia hommy tangu na anza,
Moro town hommy, sio Mwanza, Mwanza,
Wanaogopa kuja DSM mpaka Chuga,
Wage ngumi kubwa na wanyuka,
Nawajua wakali wenye, mi ni njaa wao menu,
Mii ni star wao fame,
Chata kila sehemu,
Wanangu wana ni support,
Sababu mchizi si copy,
Kwenye vesi si ongopi,
Battle si ogopi,
Na Hip Hop siondoki,
Na apa kubaki hapa”
Wage Inshallah tutakua nae mda mrefu kwenye hili rap game kama utanyanyua mikono na kumuunga kwenye safari yake ya usanii.
15. Nipo next
BCP anajionyesha vile yeye yupo level ya juu, matawi ya juu akisema,
“Wage ka change, flow mpaka vesi,
Kwa sasa yeye yupo next”
Anajilinganisha na ma legendary wa zamani anaposema,
“Tuko tofauti kama Bongo na Alabama,
Wage ni mixer ya Dogo na Cowbama”
Kupitia album hii je BCP amepeleka game hadi level ya juu? Sina shaka kusema kua Mcheza Kwao hutuzwa na kwa kupitia album yake ya kwanza lazma ma MC wakae,wamskize na wa mtuze BCP kwa kutoa albam ambayo ni moja wapo za album bora za hip hop mwaka huu wa 2020.