
Black Beats/Blaq Beats
Kawaida ya watayarishaji wengi wa muziki, kazi zao hujulikana sana na mashabiki zao kuliko wao wenyewe. Aboubakar Dachi kama anavyojulika rasmi tayarishaji Blaq Beats ambae ni mzaliwa wa Arusha ila mkazi wa Dar Es Salaam ni mtu ambae kwa msemo wake ananpenda kazi zake ziongee.
Kazi zake zimeongea na kuwafikia wengi pamoja na kuwagusa hadi Micshariki Africa tukaona itakua mzuka sana kama tutaweza kumpata mhandisi huyo wa sauti ili tuweze kumfahamu. Kwa mara ya kwanza tunamleta kwenu kaka Blaq Beats In This Micshariki Africa Hip Hop platform.
Skia Playlist ya Black Beats/Blaq Beats hapa
Karibu sana kaka Black/Blaq Beats....Tuanza kwa kukufahamu majina yako rasmi, unatokea wapi na unajihusisha na nini?
Asante sana timu ya Micshariki Africa. Jina langu ni Aboubacar Dachi ama Black Beats ambayo ni alias yangu. Mimi nimwezaliwa Arusha lakina shughuli zangu nyingi nazifanyia Dar Es Saalam.
Tueleze kuhusu hili jina lako la kazi Black/Black Beats (pamoja na ile jingle "Black In This"). Haya majina yalikujaje na yanamaanisha nini? Hii jingle yako "Black In This", ilikujaje tupe story ya muhuri wako wa kazi, uliupata vipi?
Historia ya hili jina la Black Beats linaanza wakati nilipokua naanza beat production, nilikua na kaa sana na kaka mmoja ambae alikua anaitwa Sonyo. Sasa yeye kwenye kukaa nae kwa mda mrefu alinipa nick name ya DJ Black Muslim. Kwa hiyo nilivyo anza kufanya beat production watu walipokua wananiuliza ki kazi, nilikua najitambulisha kama Black Muslim.
Lakini baadae nikaja kukutana na JCB (Watengwa) wakati nilipokua nafanya zile kazi serious na hapo ndipo akanishauri kua hilo jina la Black Muslim ni ngumu sana kwasababu linakaa kidini kwa hiyo akaniuluza, “Kwanini usijiite Black Beats au Black Midundo?” Akaanza JCB na kisha baadae Chaba akaniita Black Beats baada ya kufanya nae kazi, kwa hiyo inatoka kwenye Black Muslim kwenda kwa Black Beats.
Ikaande kwa mda mpaka ilipofika miaka ya 2018 na 2019 nilipo bahatika kufanya kazi na wasanii ambao wengi walikua Tamadun Muzik, especially kama Nikki Mbishi na One The Incredible.
Kwa hivyo kuna wimbo mmoja ambapo One The Incredible aliweka kama shout out kwa producer kwa kusema, “Black In This!” Kutoka hapo nikawa nimeipenda hiyo “Black In This” ndio nikawa nimeitumia kama jingle yangu.
Awaili nilikua naitwa Black Muslim ila baadae JCB na Chaba wakazoea kuniita Black Beats nayo ikakua lakini baada ya Uno kufanya ile intro ya “Black In This” ndio nikaichukua nikawa nimeitumia kama signature ya nyimbo zangu.
Tupe historia yako ya awali, ulizaliwa wapi, lini na kimasomo ulisomea wapi shule ya msingi, ya upili na pengine elimu ya baadae? Utoto wako ulikuaje?
Mimi nimwezaliwa Arusha mwaka 1987 huko kwenye hospitali ya Mount Meru. Nimekulia Arusha, nimesoma mpaka darasa la saba na nilipo maliza darasa ya saba nikaja Dar Es Salaam kwa ajili ya masomo ya sekondari.
Nikiwa huku Dar nikasoma mpaka Form 6 kisha nikarudi Arusha ambapo ni nyumbani. Nilipofika Arusha nikaendelea masomo ya chuo mpaka nikapata Diploma ya Computer Engineering. Kwa hiyo baadae tena kwenye kusogea sogea wakati najigundua kwenye production pia nayo computer engineering hii ilinisaidi kwenye hii fani ninayo fanya kwa sasa ya music production kwasababu tunatumia ma komputa na software.
Kuenda shule na kusoma hasa hasa computer engineering kumenisaidia mimi kuweza ku navigate kwenye maswala ya production.
Haya maswala ya muziki ulijikuaje umezama ndani? Hebu tupe historia yako kuhusu sio tu utayarishaji bali hata muziki ki ujumla?
Mimi ni Muisilamu na nimekulia kwenye familia ya Kiislamu ya kidini ambayo wana practice dini kweli kweli kwa hiyo pia muziki kwetu ni kitu ambacho hakikua au hakikupewa kipaumbele, ingawaje kwenye famila yetu kuna watu wawili, watatu ambao pia ni wanamuziki.
Kama kuna babu yangu, mdogo wake bibi yangu ambae alikua mpiga ngoma na amewai kufanya kazi na watu wengi akiwepo Waziri, wale walikua wa nyota band na Njenje. Kwa hiyo babu yangu alikua na elimu ya kupiga ngoma kabisa, elimu ya muziki wa band.
Saa nyingine nilikua niki kaa nae na pick vitu kutoka kwake ingawa nilikua sijui nitakuja kua nani baadae. Kwa hiyo ni kama nilikua nachukua data tu ambazo sikujua nitakuja kuzitumia lini.
Nimekulia kwenye mazingira ya kifamilia ya kidini, shule ni Madrasa na singeweza kuskia muziki kwasababu access ya kuskia muziki ni mzazi.
Nimekuja kujua mziki ukubwani mpaka kua na interests za kutengeneza, yaani vile maisha hayana formula, sio kitu unachojua utakuja kukitegemea ila unajikuta umeza zama kina kirefu tofauti na vile ulivyolelewa.
2000/2003 kama sikosei nikiwa Form 2 hapo ndo album ya 50 Cent, ‘Get Rich Or Die Trying’ inatoka. Sasa ndo kipindi ambacho mimi ndo naskiliza Hip Hop. Baada ya kuskiliza huu mradi wa 50 Cent mbali na kuskiliza miziki yote ile pale ndo nilipata inspiration, baada ya kuona aina ya beats zinavyo lia, jamaa anavyo tengeneza muziki nikawa super inspired.
Sasa na pia kizuri au kibaya nilikua na rafiki pembeni ambae alikua msanii wa handaki, yeye alikua ananipeleka kwa washkaji zake ambao walikua wanafanya beat making na kupitia huko na mimi ndo nikawa nae sasa ile passion imeanza kuja, nikajifunza kidogo kidogo kwa hawa watu ninao kutana nao kufanya beats.
Mtu mmoja wapo niliekutana nae alikua anaitwa Bano Styles, alikua mshkaji sana na mwanangu mmoja, alikua anakuja kwake, wanaunda midundo. Kupitia Bano Styles nikajifunza mwenyewe kwa kuangalia vitu anavyo fanya kwa hiyo mimi nilikua nikipata time kukaa kwenye PC na Software.
Katika zile hatua za awali nilikua nikiunda mdundo watu walikua inspired wananiambia vile ni nzuri, kua mdundo ni mkali. Hili lilikua linanipa motivation kali zaidi ya kuendelea na hatimae kujikuta hapa nilipo.
Pia wewe unajitambulisha kama music producer na sound engineer, hebu tufafanulie hapa unamaanisha nini? Haya ni majukumu mawili tofauti?
Mimi najitambulisha kama producer na kama engineer (mhandisi) ingawa kuna wakati kazi zangu napelekea engineer kama Chizan Brain hua ana finalize kazi zangu. Ni kwasababu pia inatokea kurahisisha kazi na pia kufanya kazi inakua easy kutoka ni pale producer unapokua una uwezo wa kufanya mastering.
Kwa hiyo sasa anaefanya mastering anakua ni engineer kwasababu ana knowledge ya frequency and sound, kwamba anajua the whole sound iweje, limitation ya mziki, power ya mziki ni engineer ana control hivyo vitu kwasababu ana elimu ya sound.
Ni kitu ambacho producer anajifunza lakini skio la engineer takes time and experience. The more experienced you become ndio unazidi kua mhandisi (wa sauti). Kadri uzoefu unavyo zidi na unawezo wakuzielewa frequency ndio unavyokua engineer.
Sio lazima producer uwe engineer lakini inapendeza kama producer ukiweza ku master kazi yako, yaani ni producer/engineer. Lakini engineer anaweza akawa mtu special wa ku polish/kung’arisha ule muziki, kuuweka kwenye standard na quality, ikawa ni radio ready song. Radio ready yaani manake kwamba ina vipimo vyote, ime mixiwa vizuri, imefanywa mastering vizuri, sound kwamba ipo radio ready.
Kwa hiyo kuna engineer, kuna producer. Ni rahisi sana kwa producer kua engineer kwasababu over the years unaweza ukajifunza, uka learn na ukawa una lile skio, kwasababu skio ni kama muscle, inafanya mazoezi, linavyoskia ndio linavyo komaa. Kwa hiyo unaweza ukafika level umekomaa kwamba unajua hii quality ni yenyewe.
Ni kama muonja beer uki taste unajua hii imeiva au haija iva, kitu kama hicho.

Mdundo au ngoma yako ya kwanza kuwai ku rekodi ni upi? Je mapokezi yalikuaje kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki? Pia ni ngoma au mdundo gani uliokutambulisha rasmi kwa mashabiki wa Hip Hop wakasema, "Dundo la nani hili?"
Ngoma yangu ya kwanza kwenda ilikua ni nyimbo ya JCB ambayo alimshirikisha Fiq Q na Kalapina ambapo chorus inaenda
“Nashinda kila sekunda kaa nime invest kwenye muda/
Sina muda wa ku spendi hata kwa cash za kuzuga/”
Ngoma lilikua linaitwa ‘Sina Muda’.
Kwa hivyo baada ya ku meet na JCB akanikubali akachukua beats zangu baadhi na baada ya muda. Wakati huo bado nilikua ni youngster na naweza sema sikua nafanya muziki wakati huo kama daily kwenye maisha yangu, ilikua part time, part of my talent lakini ndo hivyo talent ilikua inaonekana ni kubwa.
So baada ya kumpatia JCB midundo yangu kisha ngoma hiyo ndo ikatoka. Mostly underground artists walikua wanakuja studio wananizunga wanataa midundo kwani walikua wanajua uwezo wangu lakini kwangu mimi midundo ile nilikua naiona ni mikali kuliko wale artists ambao walikua wamenizunguka na hili linilazimu mimi kuweza kuwatafuta artists wakubwa na kwa bahati nzuri wakajitokeza akina JCB na tukafanya kazi.
Hii ndo ikawa kazi ya kwanza na ikaenda na ikanitambulisha vizuri kwa watu wengi kwasababu JCB wakati huo ndo alikua ameshindashinda tuzo kwa hiyo alikua ni wa moto mno na kipindi hicho Hip Hop ilikua kwenye peak ya juu na wimbo ukaenda na walioshirikishwa nao walikua babkukwa.
Basi hiyo ngoma ikawa imenitambulisha kwanza kwa hawa wasanii wenyewe akina Fid Q na Kalapina na wengine wote ambao ni fans wa Hip Hop waka appreciate na pia nikapata recognition kwa ma producer wengine ambao waliskia kazi, kwa hivyo ikawa ni blessings.
Kwa upande wa familia yangu hakukua na maswala ya muziki kwa hivyo hakuna vile ningeenda kuwaambia kuhusu maswla ya muziki, ingekua hard kidogo.
Ila nilifurahi kwasababu wimbo ulienda, JCB akanitambulisha kwa watu nikawa sasa officially recognized kama kuna producer anaitwa Black Beats.
Je wewe umejikita kwenye midundo ya Hip Hop tu au unapiga midundo aina yoyote bora jax tu?
Mimi ni producer ambae nategemea msanii amekuja na vibe gani kisha tunafanya kazi iwe ni reggae iwe ni afro beats, tuna piga kazi.
Ukiwa kama producer hauna lable kua unatengeza reggae ama Hip Hop ama nini. Kwa ufupi producer ni mtu ambae anaeweza kutengeneza muziki tofauti. Asilimia ya wasanii wengi wanao nizunguka wanafanya Hip Hop ndo maana unaniskia sana kama mtayarishaji wa Hip Hop ila nafanya za kucheza, za kuimba chache chache kutokana na wale wanaotaka mziki huo.
Hata mwaka jana na Mex nilifanya EP inaitwa ‘Afro Vacation’ ambao ni mradi ulikua una Afro beats tupu!
Na inapokuja kwa studio unapatikana studios gani aidha umeajiriwa au unaimiliki wewe?
Mimi sija ajiriwa ila nio partnership na Lufunyo, mmiliki wa studio ya 41 Records ambayo hits nyingi sana zimefanyika hapa. Hapa ndo alikua Mandugu Digitial, pia alikua Lamar Fishcrab. Mimi ni business partner wake tunafanya kazi na kisha tunagawana kwa asilimia ila pia ni kama freelancer ambapo hua naitwa studio tofauti na pia wasanii wapo free kuniita kwenye studio yoyote walipo wao.
Ngoma mbili ulizoziunda zishawai kushinda tuzo la Micshariki Africa Emcee Of The Month, hapa nazungumzia 'Price Up' ya Nikki Mbishi pamoja na 'The Legacy' ya Wakazi. Unajiskiaje kuhusu hili?
It's a big honour kuona kuwa my contribution to Hip Hop is appreciated and valued. Inanipa motisha ya kufanya zaid na zaidi.
Black tuzame sasa kwa catalogue ya full projects za wasanii ambazo ulishiriki kwa namna moja au nyingine kuziunda iwe ni EP, Mixtape au album. Tupe majina ya wasanii husika na project zao.
Kazi ambazo nimeshiriki kufanya ni nyingi kutoka mwaka 2016 kwenda 2017 nimeshiriki kufanya nusu ya album ya Chaba 009 ambayo ilikua inaende kwa jina ‘Tanzanite Miele’ ambapo nimefanya kama asilimia 50 ya album, kuna nyimbo kama ‘Washa Washa’, ‘Fungulia Ma Umbwa’, ‘Nachapa Viboko’, ‘Mwanangu’ na ‘Tanzanite Milele’ ambayo imebeba jina la album.
Pia nimefanya album ya Davan Trappe kwa kama asilimia 70 kwenye album yake ‘Lyrical Testimony’. Alafu nikaja Dar baadae nikafanya kazi na Ghetto Ambassador asilimia 70% ikiwemo nyimbo kama ‘Aste Aste’ na nyingine nyingi kwenye album yake ‘Hisia Za Burudani’.
Mwaka 2019 nikafanya portion ya album ya Nikki Mbishi kwenye nyimbo kama ‘Priceless’ na ‘Buni Mbinu’ akiwa na Belle 9 kwenye album ya ‘Sam Magoli’. Baadae pia 2019 nadhani pia tulifanya kazi na Wakazi kwenye EP ‘The Massacre’ yake wakati akikaribia ku launch album yake ya ‘Kisimani’.
Pia tukienda mbele nimefanya kazi na Mex Cortez ‘Monsoon Winds’, EP ya ‘Afro Vacations’ na singo singo zipo kibao. Pia nilifanya kazi kwa mradi wa ‘Lyricist Lounge’ wa Fety Jen .
Pia nimehusika kwenye album ya Mansu Li ya ‘Love Life’ nimefanya ngoma mbili mle. Kwenye album ya JCB ‘Fundi Mitambo’ kuna ngoma tatu mle.
Yaani nimehusika kwenye miradi ya wasanii kibao especially za Hip Hop artists. Pia nimehusika kwenye album ya Frost wa TGP ambae yuko na We Present Africa ambae nilifanya nae ngoma mbili tatu, still project ni nyingi ambazo nimechangia, zaidi ya album sita au saba.
Baada ya hapa sasa tupe majina ya wasanii ambao umeshawai kufanya nao kazi hata kama sio full projects?
Nimefanya kazi na wasanii wengi wakiwepo Chaba, Nikki Mbishi, Ghetto Ambassador, One The Incredible, Mansu Li, Zaiid, Wakazi, Mex Cortez, Fresh Like Uhhhh(Pablo), Mr. Blue, G-Nako, AY, Fid Q, Cado Kitengo, Blvck Queen, Eli Hekima Davan Trappe, Meddy Botion, Hard Mad, Chindo Man, JCB Watengwa, Fredrick Mulla na wengine wengi!
Mchakato wako wakuanda kazi iwe ni beat, ngoma moja au hata full project upoje kutoka pale mteja anapokuja kwako hadi pale unapo mkabidhi kazi yake?
Process yangu ya kazi ipo hivi, wajua mimi wasanii wengi mostly wanao nitafuta mimi, hua wamepata namba mahali kisha wananitafuta aidha kwa message au simu. Wengi hua hawataki kuja studio kwanza, hua wananiambia vile wanapenda kufanya kazi na mimi, wanapenda vibe, kisha wanaomba beats midundo miwili mitatu, waone itakayo wafaa ili waifanyie kazi.
Kwa hiyo nyingi ni maandalizi ya awali ambapo unakuta mara nyingi namtumumia ambayo nishaanda kabisa. Mara chache chache sana unapata yule mtu ambae anataka muanze nae kutoka mwanzo au mwingine anakutumia links za mziki ya aina flani na anakuomba umuandalie mziki wa aina hio.
Wewe kama mtayarishaji hua unajihisi vipi kazi ambavyo umeisimamia mwanzo mwisho kazi kisha inakua kubwa ila msanii ndio anapewa credits zote na wewe umewekwa kapuni?
Aisee swala la recognition kwenye kazi inapokua kubwa ni muhimu. Kazi inapokua kubwa alafu recognition kwa producer ni ndogo which means biashara yako wewe ndio imedogoshwa kwasababu lengo haswa ni la wewe kutangaza biashara yako ili watu waskie ukubwa wa kazi na quality ya kazi ili na wewe uweze kupata wateja.
Sasa kama kazi ilikua ni kubwa alafu ikienda kisha producer akawachwa nyuma inakua kidogo inakatisha moyo, inaleta stress. Mziki unaleta stress, watu wanapata mpaka msongo wa mawazo, unakuta mtu alitumia nguvu zake kufanikisha jambo alafu yeye amebaki mtu wa nyuma.
Kiukweli hili swala linarudisha watu nyuma na wanabaki na mawazo na fikra kibao na ki ubunifu mtu anakwazika kama ana kwama vile.
Hii chemistry yako na crew ya Tema Yai, Nikki Mbishi ilikujaje na kadhalika na inakurahisishiaje kazi wakati mkiwa mna andaa project?
Nikki Mbishi nilikuta nae kwa mara ya kwanza kipindi hicho cha mwaka 2016/2017 sina uhakika wakati nilipolua nafanya kazi kwenye album ya Chaba 009 kwenye wimbo unaoitwa ‘Washa Washa’ ndo siku nilikutanana Nikki Mbishi.
Chaba alikuja nae studio, kulikua kuna show inafanyika Arusha, na kisha Chaba akamwambisa kuna studio ya mshikaji wangu huko kuna beats bali, kisha wakaja na kwenye kupiga mdundo wa kwanza ndo hiyo Nikki akaichagua ndo nikawaundia wimbo unaoitwa ‘Washa Washa’.
Kutoka hapo Nikki alikubali na ile ile siku tukafanya nae ngoma ambayo ilikua inaitwa ‘Kunguru Hafukigi’ ila kwa bahati mbaya nikapoteza files zake kwasababu nilikua kwenye movement kuja Dar. From there ikawa ni kama Nikki amekubali beats zangu na yeye ni rapper mzuri na mimi natengeneza midundo mikali, hapo chemistry lazima itokee, one way or another. Nikki ni rapper elite na beat ni kali kwa hiyo kazi lazima iwe nzuri.
Nilipokuja Dar mwaka 2017/2018, tukazidi kujuana ku spend mda mwingi studio na chemistry na Nikki Mbishi ikawa nzuri tukafanya kazi zikaenda zikiwepo ‘Gambosh Freestyle’, ‘Priceless’ na nyimbo zingine nyingi kibao za Nikki Mbishi.
Kwa kipindi hicho pia kukawa kuna series zimetengenezwa kukawa kuna track zinaitwa ‘Power’, kuna track wanawekwa wasanii kama 9 alafu zinatoka. Zilitoka track mbili kwasababu zilikua zinanigharimu muda alafu pia kukusanya watu kwa hiyo ikawa inachelewa, inachukua mda. Kwa kipindi hicho pia nilibahatika kukutana na Wakazi, baada ya kufanya nae kazi yeye ndo akanikutanisha na Mex Cortex. Nikaanza kufanya kazi na Mex kisha nikaanza kukutana na watu wengine ambao ni Tema Yai Nation ambao ni Pablo, Clint na wengine.
Chemistry ilitokea kwa Mex, Wakazi na Pablo ndo nimefanya nao kazi sana kama Tema Yai. Mex nimeanza kufanya nae kazi mda mrefu sana karibu miaka mi nne mitano sasa tumekua pamoja tukiachia miradi pamoja tumetoa album plus EP moja moja kibao zikiwemo series za Barbenders zile mimi na yeye since tumekutana tumekua tukifanya hizo project zote.
Kaka hizi mbanga za utayarishaji zinakulipa au inabidi kupiga na kazi zingine ilikuweza kukidhi mahitaji?
Aah muziki peke yake hautoshi kwasababu circulation ya fund kwenye muziki ni kidogo haipo stable. Kuna wakati business inakua ni high season inakua na low season na ukichangiwa na wana asilimia kubwa na muziki wa Hip Hop pia hawajawekeza budget kubwa sana kwenye kufanya production. Kwa hiyo pia inakua na changamoto, otherwise brand ikiwa kubwa una hukakika wa kupata wateja wengi itakua vizuri. Hili linamaanisha itabidi uwe na consistency kubwa na nyimbo ziwe zinatoka nyingi kali itakurahisishia wewe kupata wateja wengi, vinginevyo inabidiki kama maisha yetu ya kibongo unachanganya muziki na shughuli zingine ili mambo yaweze kwenda.
Neno la mwisho na wapi unapatikana kwenye mitandao ya kijamii, barua pepe na pengine simu?
Ningependa kumaliza kwa kusema shukran sana kwa timu nzima ya Micshariki Africa kwa recognition na kazi yaku fanya research yakujua watu na kuweza kuwatambulisha kwa watu ambao hawakuwafahamu waweza kuwafahamu kuweza kutengeneza msingi mzuri kwa njia ya mtu kufanya biashara kwasababu mnamtangaza.
Kwenye mitandao ya kijamii napatikana;
Instagram: @blackbeatsinthis
Facebook: blaqbeats
Twitter sipatikani, napatinaka tu Facebook na Instagram
Email: Bakardutch@gmail.com
Shukran sana kwa Boom Bap Beats zako, japokua upo nyuma ya pazia, midundo yako hutubariki sana kwenye speaker zetu. Kila la heri kwenye shughuli zako..Black In this!
So it’s a good thing, ni kama mnapa mtu mauwa yake wakati bado yupo hai aweze kuyanusa. It’s a good thing, big up kwenu sana, ninashukuru sana kwa kunipa hii nafasi. Shukran sana tena na kila la heri kwenye mishe zenu.