Boshoo Ze Son (Ninja)

Utangulizi; Karibu Boshoo na shukran kwa kukubali kuhojiwa nasi ili tuweze kumfahamu Boshoo (Ninja) na shughuli unazozifanya.

Kabla ya kuendelea mbele tunaomba kujua majina yako kamili

Mi naitwa Mathias James Lekule

Asili yako ni wapi, uko wapi na unawakilisha Mkoa gani?

Mimi baba yangu  asili yake ni mchaga ila maisha yake na familia kwa ujumla yaani babu ni Korogwe na mama yangu ni Mzigua ila mimi nimezaliwa Tanga na nimekulia Tanga kinachomjenga mtu ni tabia ya aliko lelewa ndo maana  naiwakilisha Tanga nikiwakilisha Moshi ntakuwa nimewasnich wana Korogwe ila mimi ni Mchaga ,Mzigu au(Chagua) kwa maana ya Chaga na Zigua.

Kwanini uliamua kujiita Boshoo?

Boshoo ni jina la Babu yangu mzaa mama alikuwa anaitwa Boshoo Kayembe alikuwa ni mwimbaji wa Bendi ya zamani Congo ilikuwa inaitwa Extra Mazembe kama sikosei

Mbona pia unajiita Ninja?

Ninja ni kwasababu ya michano tu haina maana yoyote ile. Uninja wangu unapatikana kwenye mashairi yangu, sina mapanga, beats ndio mapanga yangu na unyama wangu huoneka vizuri juu ya beat na kupitia kinasa

Kitu gani kilikusukuma mpaka ukajikita kwenye utamaduni huu wa Hip hop na kuacha kufata kile kilichokuwa kinafanywa na mwenye jina lake (babu)?

Kuna kaka yangu mtoto wa mama mkubwa anaitwa Nady alikuwa anachana zamani nikawa nasoma mistari yake naenda kuichana shule kipindi hiko ni primary basi nikajikuta napenda maana nilikuwa nikifanya nashangiliwa sana basi kwa umri ule ikawa ndo fahari yangu mpaka nikakua na kujitambua kichwani mwangu ikabaki hii kitu.

Sawa. Ukiachilia mbali kaka yako, je baada ya hapo wapo ambao walikushawishi kufikia hapo ulipo kuanzia bongo mpaka ughaibuni?

Wa kwanza alikuwa Langa Kileo(R.I.P) kiukweli kwa upande wangu mimi.

Tukiachana na hayo, track yako ya kwanza ulifanya lini, na katika studio gani na iliitwaje?

2009, Image Rec, Tanga braza aliniambia siku hiyo twende studio tukafika nilikuwa na mistari yangu nilivyochana wakafurahi na naikumbuka hadi hiyo mistari mpaka leo.

Mpaka sasa Una kazi ngapi, Kati ya Mixtape(Kandamseto) na albums na zinakwenda kwa majina yapi?

Nina ngoma zaidi ya 15 ambazo ni pamoja na zilizopo kwenye tape na nina Mixtape moja inaitwa Ujamaa Shari na pia Ep moja inaitwa Kwa Yoyote Inaemuhusu. Sina albam bado.

Nakumbuka tape yako ya kwanza ulifanya na Ngwesa nyimbo zote, je ulifanya kazi ukiwa chini ya Ngwesa kama msimamizi wako au ulifanya nae kirafiki tu?

Ilikuwa na makubaliano kadhaa ambayo siwezi kuongea hapa ila pia ilikuwa ni platform kwangu watu wengi walinijua kupitia pale pia Duke alihusika kwa kiasi fulani.

Kitu gani kilifanya mixtape yako ukaipa jina Ujamaa Shari ?

Huo ulikuwa ni wimbo na kuna bonde la unafiki nililivuka ikanibidi niiandike na kuipa jina hilo ni urafiki ushkaji ambao hauna faidi na mwisho ni kuchomana au kufanyiana mambo ambayo si sawa.

Zinapatikana Vipi? Kama kuna links tunaomba tuzipate

Wasiliana na mimi au Ngwesa kwa kupitia namba ya simu 0718844462

Baada ya kutoa mixtape yako ya Ujamaa Shari nini kilifuatia kwenye project zako?

Zilifuatia kolabo na single kadhaa na ndo mpaka hapa tulipo.

Nini malengo ya mbele kwa kile unachokifanya na mziki wako kwa ujumla?

Ninachokifanya nione matunda yake hiyo ndo final na ndo ukweli.

Ni ukweli mkubwa sana, ila kwa Industry yetu umejipanga vipi kukabiliana na fitna?

Najua ina changamoto sana na ni swala pana sana  niko ndani ya box sasa ndo kwanza naanza kukutana na hizo changamoto ila  nitapambana nazo kwa namna yoyote kwa kuwa si ndo njia niliyochagua.

Emcee ni kioo cha jamii je taswira ya mziki wako ni ipi kwenye jamii inayokusikiliza?

Najaribu kuwa mbunifu na kufanya miziki tofauti tofauti ili niweze kumgusa kila mtu ajira,mapenzi,siasa,burudani n.k maana siwezi kuongea kwenye wimbo mmoja mambo yote ila kwa miziki najaribu nimguse kila mtu kwenye jamii inayonizunguka.

Tuzungumzie kuhusu kundi ambalo ulikuwepo wewe Maarifa, Moh Rhymes na Chief Songea je kundi lipo au ndio lishapoteza mwelekeo?

Halikuwa kundi ilikuwa ni team na hii tulishaizungumzia sana ilikuwa ni project ya Duke Tachez  ikaisha ndo ikawa mwisho hapo ,lakini kwa kuwa tulikaa pamoja sana tukazoena tukawa kama ndugu ikawa tukikutana tunafanya kwa love lakini Maskatiaz official haipo tena ila tunaweza tukakutana tu tukiamua tukafanya hata ngoma kama Maskatiaz.

Je akitokea mtu mwingine tofauti na Duke na kutaka kurudisha Maskatiaz mtakuwa tayari kurudi au ni mpaka Duke atoe ruhusa?

Kama mikakati ikikaa poa ni sawa lakini tunakuwa Maskatiaz lakini  kila mtu awe na miziki yake pia isiwe kundi tu moja kwa moja then kila mtu akashindwa kuonesha ukubwa wa talanta yake.

Unachokifanya kinaendana na ulichowekeza na unachokivuna

Hakuna kikubwa nilichovuna mpka sasa ukiongelea mali lakini nimevuna mashabiki wengi ambao ndo daraja la kunivusha niendapo.

Mbali na utamaduni wa Hip hop unajihusisha na kitu gani?

Mi ni mjasiriamali nafanya biashara ndogo ndogo kuuza T-shirt na hata vikapu.

Akitokea mtu akakwambia Boshoo wewe ni whack hufuati misingi wewe utamjibu nini?

Mi sio nabii kaka kivipi nisipingwe. Watu wanampinga Mungu sa sembuse mi andunje....

Dakika kumi za maangamizi zilikupa jina kubwa sana na watu wengi wakazidi kukufahamu je ni changamoto gani ulizipata baada ya kipindi kumalizika?

Baadhi ya watu karibu wanaona kama naringa now unajua nini? Unapoianza safari wanakutia moyo unapoanza kuonesha mafanikio wanaibua vikwazo.

Vikwazo gani umekumbana navyo baada ya show kwenda hewani?

Kama hivo mtu kuona kama unaringa so kama alikuwa anaweza hata kukusaidia ushauri ndo hupati tena.Kuna mtu alinitumia sms, simjui, sijawahi kumuona halafu ananiambia naomba namba ya Jr,Frida Amani na Dullah Planet(wote wa East Africa Radio), nikamjibu awatafute wenyewe hata Insta watampa basi jamaa aliongea sanaaaaaaaaaaa!

Ya Kweli Yapi", kitu gani kilifanya ukaandika huu wimbo?

Wimbo unazungumzia changamoto za mapenzi ukiwa na pesa na ukikosa pesa na usaliti na uwongo ndani yake.

Tueleze kidogo kuhusu EP yako Kwa Yoyote Inaemuhusu ambao ndio project yako ya hivi karibuni kama sijakosea

EP yangu inangoma 6 na inapatikana kwenye platform zote za streaming kama vile Deezer, Sportify, Boomplay, Audiomack,Amazon na kadhalika. Ep hii hapo awali ilikua na nyimbo tano ila baadaye tuliongeza wimbo wa Bajaj kama bonus track.

Pia nilitoa video ya wimbo Toa Shavu niliomshirikisha Jay Melody unaopatika kwenye EP hii.

Tutegemee nini baada ya mradi huu kutoka?
 
Natarajia kutoa singles kadhaa, freestyles ,video ila pia naanda albam yangu ya kwanza ambayo natarajia itakua na nyimbo zaidi ya kumi na itakua tofauti kabisa.
 
Mbona uliamua kuachia EP Kwa Yoyote Inaemuhusu kwenye streaming apps?

Enzi hizo nikitoa singles zangu na Mixtapte ya Ujamaa Shari nilikua bado niko nafasi flani underground enzi hizo Digg Down ila naona nimepiga hatua flani ambayo sasa pia nalenga soko la mainstream ili wana wazidi kukaribia.

EP niliita Kwa Yoyote Inaemuhusu ili kila mtu apate kuisikiliza ila kuaanda mazingira ya kuwauzia bidhaa yetu hapo mbeleni. Lengo kubwa ni kua mziki uwafikie wengi ili mambo yaende. Ni changamoto kama unawekeza kwenye mziki na haupati chochote kama umewekeza kuandaa nyimbo pamoja na video.

Kwa mfano nimeunda nyimbo zote 6 na Wenene Studios na ku shoot video na Elvis (Redshot) na zote hizi kuna gharama nimelipa na uwezekano wakurudisha hizi senti ni vigumu kama mziki hautawafikia wengi kwani hata nikiuza kwa mmoja mmoja ni vigumu sana kurudisha hata kile kiasi nilichowekeza.

Unaiongeleaje underground ya Bongo?

Siku hizi hatupendani na majungu mengi sana vijana sisi wachache ndo wana love ya kweli kwa wasanii.

Boshoo asante kwa mda wako, kwa kumalizia tutajie majina unayotumia katika mitandao ya kijamii na kutaja njia ambazo mashabiki zako wanaweza kupata kazi zako. 

Wasiliana na Boshoo kwa kupitia mitandao ya kijamii;

Facebook: Boshoo Ze son
Twitter: Boshoo15
Instagram: boshoo_ze_son
YouTube: Boshoo