Burnbob Wa Kitaa (RIP)

Burnbob Wa Kitaa kwa jina halisi anaitwa Agai amezaliwa, kasoma na kuishi katika jiji la Mbeya, Tanzania.

Kwenye maisha yake alitumiana kujihusisha sana na sanaa hasa uandaaji wa muziki na kufanya kazi nyingi akiwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza midundo pamoja na kufanya mixing. Alikua producer wa MaKaNTa Records.

Miongoni mwa miradi mikubwa aliyohusika kipindi cha uhai wake ni albam ya Momumo iitwayo Hisia na Momumo, albamu ya Nala Mzalendo itwayo Mimi Na Taifa Langu na kanda mseto ya Wabibi emcee itwayo Misingi. Pia alihusika kwenye mradi wa album ya Lugombo iitwao Upendo Utuongoze.

Ukiacha umahiri wake kwenye uandaaji wa muziki pia alikuwa ana uwezo mkubwa wa kurap. Kabla ya kifo chake alitaka kuachia nyimbo yake itwayo Nimeamua Kuchenji. Umauti ulimkuta alipopata ajili ya bajaji tarehe9/6/2021 amefariki akiwa na miaka 24.

Mradi Burnbob Beat Tape Vol 1 unakuja kwa lengo la kukumbuka kazi zake na kumfanya azidi kuishi mioyoni mwetu na tuna muenzi kwa vitendo. Pia tunathamini mchango wake kwa familia yake ndio maana Black Ninja kajitoe huu mradi na kipato kitacho patikana kutoka kwa mradi huu chote atakababidhiwa mama mzazi wa Burnbob Wa Kitaa.

Sio lazima uwe msanii ndo uweza kununua ila mtu yeyote anaweza kununua na kusapoti kinacho jambo hili. Unaweza kununua sasa mradi huo kupitia Airtell (+255)685248565 jina George Mwenda. Muuzaji wa album hii ni Wabibi Emcee .Peace ✌