Ukaguzi Wa EP: Mambo Kavu EP
Msanii: Cafu Da Truth
Tarehe iliyotoka: 7/7/2020
Nyimbo: 5
Ma producer/Wapiga Midundo: Mambo Makes Music
Mchanganya Sauti na Midudo: Mambo Makes Music
Studio: Mambo Makes Music

Cafu Da Truth(Kushoto) na Mambo Makes Music(Kulia)

Uviko 19 ilipotangazwa kuwasili rasmi Kenya tarehe 13 mwezi Machi 2020 wengi hawakujua kuwa maisha kama wanayoyajua yatabadilika hapo hapo. Kirusi ambacho kilidhaniwa hakiwezi kutufikia kwani Kenya ipo mbali ki jiografia na Wuhan, China kilipochipukia kirusi hicho kiliingia bila kubisha hodi mlangoni na hakikuja na nia nzuri.

Akiwa kitaani kwake Cafu Da Truth aliguswa moja kwa moja na ugonjwa huu. Corona ilileta mambo ya curfews na partial lockdowns kati ya jimbo moja hadi jingine ha hii iliathiri sana maisha ya wananchi wa Kenya ki ujumla. Kutoka kwa mazingira haya magumu na maovu aliyoyaona Cafu Da Truth wakati huu ndipo alipoamua kuchukua bic yake na kuanza kuorodhesha magumu aliyopitia yeye, familia yake na wa Kenya kiujumla. Kwa kujivika kofia ya mwana historia, Cafu Da Truth alitupatia ripoti yake kwa jina Mambo Kavu EP.

Mradi huu ambao umeundwa ki ubunifu na wenye mashairi ya kina unafunguliwa rasmi na wimbo uitwao One Time ambapo Cafu anatema mistari wakati Mambo akiimba kwenye kiitikio. Kwenye boombap beats mwanzo mwisho Cafu anafunguka kuhusu kero walizopitia wananchi wa Kenya kwenye wimbo ambao kusema kweli unaweza kupigwa klabu kama nyimbo zote zilizo kwenye EP hii na wasikizaji wakaweza kupata burudani pamoja. Cafu anathibitisha hili akisema,

“EP ni genje/
Mnaeza request kwa station/
Tumerudi na Mambo tena/
Ma messenger kwa roof Mambo Mbotela/
Kwa Coup ’82 akisoma news/
Nyi mna target ma views/
Tunataka ku make ngoma kila mtu anaweza skiza ma tunes/”

Wimbo huu kama nyimbo zifuatazo una gusa kila kona ya maisha ya mwananchi wa kawaida wa Kenya na kote duniani alieathirika kwa namna moja au nyingine na janga la Uviko.

Homesick ni wimbo mzuka sana unaomkuta Cafu akitukumbushia kule tulipotoka kabla ya hii hali ngumu kutukuta. Kwenye beat safi sana Cafu anatema nyongo kwenye vesi ya pili akisema,

“Pandemic tungefight from the onset/
Buda stay home waoni watu homeless nyuma/
Wengine kuchujwa makeja na situation ni hopeless bila unga/
Before ‘rona kwa corner jobless tupa lugha/
Boeka kaa tu kwa nyumba, niki stare kwa ukuta/
Na nikikumbuka flight za Wuhan/
Fucked up juu tulikubali foreplay saa tumeanza kujuta/”

Wimbo unaelezea madhara zaidi ya lockdown kama vile unyanyasaji wa kijinsia kuongezeka katika ndoa pamoja na ndoa nyingi kuvunjika. Mambo makes music nae kwenye kiitiko anaimba vile tumebadilika akisema,

“Si tumejificha design ya kobe/
Funika macho, face mpaka ata kope/
Tukisota si waChina tuwakope/
Me niko home sick, me niko home sick/”

Assume ndio wimbo wa tatu kwenye EP hii. Wimbo huu unakuomba wewe uvae kiatu cha mtu mwingine ili uweze hisi vile ki namfinya. Kwenye wimbo huu ambao wameshirikishwa Unit 1678 ma emcee wote waliohusishwa wanakuacha ukiona kuwa kama wewe unalia hauna kiatu cha kubadilisha wenzako hawana hata miguu ya kuvaa viatu! Kama kawa Mambo Makes Music kwenye kiitikio anasimama tena na kuonesha umihumu wake pia kwenye EP hii pia. Cafu anatema nondo za msingi tena akisema,

“Rahisi sana face ku sell hizo smiles/
Kuja tour wee upige lap za mind/
Kuna maua nipe time niko alive/
Life is short usi assume kuna time/
Ati hizi tracks ziko easy tu ku write/
Ukiniita out niko busy tu kila night/
Sisi Posho Mill design tuna grind/
Usijali giza we imagine kuna light/
Ni wa blind usi assume hawana sight/
Wakichoka usi assume hawana psyche/
Na wakisota usi assume hawana price/
Wamenyoa usi assume hawana lines/
Hawana page usi assume hawana likes/…”

Weigh Me Down ni wimbo wa nne kwenye EP ambao mdundo wake uko bouncy sana na ni wimbo wa kukutia moyo hata kama unapitia magumu gani maishani mwako. Toka kwa mashairi, mdundo na kiitio wimbo utakuacha na hisia chanya hususan ukiupiga kwenye speaker zinazotoa mdundo freshi sana. Chemistry ya Cafu na Mambo inazidi kuonekana dhahiri hapa wakati mambo akitu serenade na sauti yake nzuri na kutupatia matumaini kwenye kiitikio akisema,

“I’m not a prophet but ni hobby inanipeanga vision/
Don’t you forget to work on what you had timiza mission/
Naona mwangaza baada ya giza/
Kilicho na mwanzo huwa na mwisho/” (I’m not gonna let this weigh me down)

Wimbo wa kupiga wakati unapitia magumu.

Single iliyobeba mradi huu ni Mbukinyaa. Kule Kenya kuna makampuni tofauti ya mabasi kama vile Mombasa Raha, ENA, Mash, Coast Bus na pia Mbukinya. Emcee huyu aliamua kutumia jina la basi la Mbukinya kuunda wimbo wa kimapinduzi hapa akitumia jina hili kumaanisha yeye ana basi la mapinduzi kwa kimombo Revolution Bus. Mbukinyaa kama wimbo wa mwisho nadhani uliandikwa hadi wino ukaisha kwenye kalamu ya Cafu. Kama kawa Mambo Makes Music kwenye kiitio naye amesimama wima kuhakikisha wimbo unasimama sio tu ki mdundo bali hata kwenye kiitikio. Kama kawa nondo juu ya nondo toka kwa Cafu akisema,

“Hamtaki kuona system imetupiga deepthroat/
Hadi mwananchi akibonga hakosi ma veins kwa shingo/
Level ya brainwash ni evil/
Ka jirani hu complain kwake kuna kombamwiko/
Na ye ndio hu protect rais wetu na pistol/
Na wakiendelea kutushika ju ya kuimba wimbo/
Napigia Smallz Lethal/
Namwambia pia me niko offended na na represent the people/
Ni simple, either kuna food kwa riko/
Na mme legalize ombitho/
Muanze ku cure the syndrome/
Anzeni ku invest on something you can build on/
Acheni ku squander billions/”

Mradi huu wa kimapinduzi ulikuja wakati mwafaka sana kwa wana Hip Hop sio tu wa Kenya bali hata Africa Mashariki kwani wote walidhurika na janga la Uviko kama vile emcee Cafu ila yeye alichukua changamoto hii na kuamua kukabiliana nayo kwa kuandika mashairi. Mashairi haya yaliandikwa ki ustadi na kwa kupitia mkono wa producer wake akafanikisha mradi ambao umeweza kutuliwaza na kutupa nguvu kuwa kama Cafu alipitia haya yote aliyoyaandika na akashinda sembuse mimi? Mambo Kavu EP ndio mpango mzima toka kwa Mambo na Cafu!

Kwa mawasiliano mcheki Cafu kupitia
Facebook: Cafu Da Truth
Instagram: tallrapmidget
Twitter: TallRapMidget