Uchambuzi Wa EP: Woman
Emcee: Chiku K
Tarehe iliyotoka: 10.05.2022
Nyimbo: 6
Mtayarishaji, Mixing & Mastering: Cjamoker
Studio: Dream Booth

Nyimbo Nilizozipenda: Woman, Naleta Noma, Mapene, Bwesa Bwesa, Bonge La Jiwe

Chiku K

Binafsi sikuwahi mfahamu Chiku K mda mrefu ila kuna mwana flani msanii kutoka Mombasa Kenya ndio aliniambia nicheki kazi zake. Uzuri ndani ya mda mfupi baada ya kuanza kumfuatilia emcee huyu alinibariki na EP yake Woman.

EP kama kawaida ki muundo huwa ni mradi mfupi na ndivyo ilivyo Woman ambao una ngoma 6 na zote zinapiga kwa takriban dakika 18. Kazi inaanza na ngoma Woman akiwa na TK Nendeze  ndio singo ya kwanza toka kwa mradi huu na ambao umebeba jina la Ep. Ngoma hii inaweka vizuri agenda ya mradi huu kuwa ni kuongelea changamoto wanazopitia wanawake kando na kumsherehekea na kumuinua mwanamke. Chiku K anaanza kwa kusema,

“Kwanza kabisa hakuna uzazi bila mimi/
Mwanaume alitolewa ubav’ kisa mimi/
Ili niumbwe mimi mwanamke ardhini asingezingua bila mimi niamini/
Nilipambana na mfumo dume ule/
Wa kuachwa nyumbani wa kiume aende shule/
Wanaume wamalize kula ndipo mimi nile/
Akifariki mume narithiwa tena bure/…”

Baada ya hapa emcee huyu ana amua kukinukisha zaidi akituambia Naleta Noma na mtayarishaji Cjamoker anampa Chiku K mdundo noma pia. Anasema,

“Ukinizingua kama Mama Samia/
Nakata nafunua watoto wanao tania/
Huu ni muda wa kufuta wote wanaodhania/
Napasua mayai yote ya chuki wanayotamia/”

Chiku kaleta noma noma mpaka kitaa…noma noma mpaka iwe balaa! Uuuuw!

Baada ya hapa Chiku anatupeleka kitaa ili twende tafuta Mapene. Juu ya mdundo flani old school mzuka sana Chiku anaanza na kiitikio akisema,

“Macho kwenye mapene/
Kichwa kwenye mapene/
Akili kwenye mapene/
Wowowo mapene/
Ndio maana mi natafuta mapene/
Sina muda wa kuzembea/
Likiwaka mi natembea/
Ndio maana mi natafuta mapene/
Wowowo mapene/”

Wimbo chanya sana unaokutia moyo unapokwenda kujitafutia mkate wako wa kila siku.

Baada ya kutafuta senti emcee huyu anajigamba kiasi akiwaambia wabaya wake kuwa yeye Sio Size Yenu. Anajigamba akisema,

Kila bar ni ya moto/
Mistari ya moto/
Beti kali beat kali zimegeukia soko/
Musipime energy utapata damage mboko/
Ndio size yenu nyie watoto/
Hii hapa ndio inaitwa mwana ukome/
Dogo akililia wembe nampa mkuki umchome/
Yeah siwaogopi sitetemeki kabisa/
Kinyago nilichokichonga hakinitishi nabisha/
Hawanitishi kwa vesi kali hawanitishi kwa flow/
Wanachofanya wao mi nilisha fanyaga before/
Yea mpo wengi  mmeungana lakini pumba/
Msinitishie mateke mi ni punda/”

Katafuteni size yenu mkibisha itakula kwenu anasema Chiku K, ana ubaya na nyie!

Baada ya hapa Chiku anatupeleka kwenye uwanja wa densi ku Bwesa Bwesa ili kutushusha presha, kula bala na kujiachia kiasi. Mdundo upo ki ragga flani ambao utakupa hamu ya kunyanyuka na kucheza kidogo.

Bonge La Jiwe ndio ngoma inayotutamatishia mradi huu. Cheki jiwe lisikupate maana kwenye mdundo wa kudensi bado unaweza jipata densi floor tena. Wimbo mzuri wa sherehe na wa kudumisha umoja kwa wana na familia.

Kwa wale ambao walikuwa wanamfahamu Chiku K mda mrefu kazi hii lazima watafurahia kurudi kwa emcee Chiku na kwa wale kama mimi ambao ndio tumefikiwa na kazi zake hivi majuzi Woman ni utangulizi tosha kuhusu dada Chiku Keto.

Kupata nakala yako ya EP hii kwa Tsh 5,000.00/Kes 250.00 pekee wasiliana nae kupitia;

Facebook: Chiku K
Instagram: chiku_keto
Twitter: ckiku_keto