Toka kwa: D Ukingo
Wimbo: Kamusi
Albam: Africa The Album
Tarehe iliyo toka: 15.12.2020
Mtayarishaji: Pallah Midundo
Studio: Kinasa Records

Beti 

Ni zaidi ya kufikirika ku compare na kamusi/
Sarufi zatiririka mfano mabomu ya urusi/
Waonao mwanzo eti huwa wa mwisho/
Pasipokuwa na chanzo haiwezekani hitimisho/
Upande mwingine ni present versus future/
Inabidi yajulikane wala na si kufichwa/
Kwa ukweli wa mambo yawekwe katika mada/
Ni kama aina ya nyimbo zitungwe kitafsida/
Mfano wanyama wangekuwa na mawasiliano/
Daily panapotakiwa wangeitisha kongamano/
Wangekuwa kama binadamu sio hafifu/
Tunapowauwa baina yetu kungejengeka beef/
Ingekua vipi binadamu tusinge kufa/
Kifo kinapo beep tukizibe kama nyufa/
Overpopulation kivipi ingetutikisa/
Tungeweza kila section sisi kuzigusa/
Residential areas vipi kwake kujaa/
Tabu ingewakuta low class ndo wakose furaha/
Wa upper wanaotesa wangeliweza darasa/
Au nao wangeshuka basi wafunge kurasa/
Wasingeweza eti kisa sekta zao upgrage/
Wakiteleza mikono yao kwenye pesa za aid/
Endeleeni kupiga pesa kwa wingi/
Pia kuzikumbata kwa mfumo wa shillingi/
Mwisho upo sio kwamba maovu hamyalipii/
Kuishi kwema ni kuwa na utu na misingi/

Kiitikio

Kamusi, inayoniongoza/
Kamusi, inatoa maono/

D Ukingo