Toka kwa: Dira Ya Uswazi
Wimbo: Happy Birthday Hip Hop
EP: Dira One
Tarehe iliyotoka: 01.12.2021
Muunda Mdundo/Mtayarishaji: Wise Geniuz
Studio: AMG Recordz

Dira One

Beti Ya Kwanza

Hip hop soap soap/
Nyoa para suka fuga afro/
Pata fleva ya hip hop, kunjua roho/
Hip hop ya Green City ina illuminate/
Piga shangwe tuna celeblate/
Tunapiga selfie nakukata keki/
Mbeya City waasisi wa harakati/
Soma map Green City kitovu cha Hip Hop/
History isha andikwa we baki una rap rap/
Miaka ya tisini ndio Hip Hop ilianza/
Kukawa na tamasha la Yo Rap Bonanza/
Washriki Mr ll Sugu na Easy B wengine kadha wa kadha/
Green City like Sedgwick Ave Bronx/
1-5-2-0 recreation room Dj Cool Herc KRS One the evidence/
Hip hop nguzo hip hop misingi yo usi give up kwa stress za mapimbi bob/

Beti Ya Pili

Dira ya uswazi mjenzi huru/
Emcee huru mwenye mistari yenye nuru/
Hip hop ukombozi wengi ina waweka huru/
Piga shangwe masela piga nduru/
Hip hop kingdom Green City ndio ikulu/
Hip hop inawapa watu nguvu ya kupambana/
Maarifa kujua dunia kwa marefu na mapana/
Watu wanapata elimu ndani ya hiphop/
Watu wanapenda burudani ya hip hop/
Watu wamepata heshima sababu ya hip hop/
Watu wamejulikana sababu ya hip hop/
Watu wamepata uongozi sababu ya hip hop/
Watu wanapata pesa sababu ya hip hop/
Watu wanacheza mdundo tu wa hiphop/
Dancers hip hop dj hip hop emcee hip hop/
Tunaendeleza utamaduni wa hip hop/
Mistari yangu kama graphic aina unafiki/
Nisumu kwa wanyoa denge wazandiki/
Hip hop shere na maneno ya ujuzi si upuuzi/

Beti Ya Tatu

Naghani lugha ya picha kama sinema rhymes adimu zenye kificho/
Sieleweki kila hisika makitabu cha ufunuo/
Nastiri jamii na kinywa kama nguo/
Bitii na vionjo mistali ina manjonjo/
Mi ni legendary na mengi ya kughani/
Maisha yangu hip hop kama movie flani/
Dira Ya Uswazi chaka la boti chapa ya noti/
Mawaki rapper nakanyaga chini kama soksi/
Wazee na wastahi heshima kwenye koti/
Salute kwa Sugu na Dj BBG/
Adili Chapakazi na Izzo B/
Lugombo Zero Budget na Wise G/
Uswahilini Matola Isanga family na wote emcees/
Kitaa mishemishe zinaendelea TMT Tunavaa Machata salute Gego Master/

Kupata Nakala Yako Ya Mradi Huu Wasiliana na Dira Ya Uswazi(Andrew Mwakibinga): +255743949917

Facebook: Dira Yauswazi(Dira One) 

             Twitter: Dira One