Toka kwa: Dizasta Vina
Nyimbo: Kanisa
Mradi: Singo
Tarehe iliyo toka: 06.02.2017
Waunda Mdundo: Ringle Beats

Salamu kanisa wako mpendwa katika bwana/
Katika wana waliotaka kufeli nami nazama/
Tangu jana uwepo wako haupingiki/
Tisa una nguvu ya kuwavuta wasiosadiki/
Tikuhitaji mambo ya kugawana madhehebu/
Waumini dhaifu wanahama hama kama wehu/
Ikiwa tangu kale wazazi wangu walichanganywa,
Basi hakika sitahukumiwa kwa kudanganywa, (kanisa)/
Sidhani ka' upo sawa kunibeza/
Maana hata wewe unapitisha dawa za kulevya/
Tukianza ku-confess yaliyo nyuma ya pazia/
We utachomwa moto alafu mi nitaachwa nakuapia/
Sitaki kuamini kuwa sadaka au kusifu kwa fasihi/
Ndio vitanipeleka kwa masihi/
Kitachonionyesha mbingu ni bidii/
Ya kutenda mema so sitaki kujua dini ipi ni sahihi, ah! /
Kanisa unatudanganya kirahisi/
Nyumba ya mungu ni mioyo yetu nahakiki/
Kwakuwa saa hizi,
Jua kali njaa hizi zinafanya ukubali kugeuka taasisi,
Usinishushe hadhi nikizini/
Ikiwa unafuga wachungaji wenye dhambi kama mimi/
Kanisa nakupa pole/
Nje msafi ndani mchafu naomba tusinyoosheane vidole/
Kanisa unaniasa/
Niache kutamani vyeo na wewe unajihusisha na siasa/
Kama mji wa sodoma ulizikwa na anasa/
Mwisho wako upo kama hautabadilika sasa/
Haufanani na meli ya nuhu/
Unaniomba mchango na kodi nimefeli kumudu/
Kanisa unanitapeli kizungu/
Unanizungusha haunionyeshi kanisa la kweli la Mungu/
Eti manabii wana vyeti/
Kanisa lina account ya mitandao ya kijamii mpaka benki/
Wahubiri wanavutana kinguvu/
Kanisa unajitangaza kutafuta umaarufu ? /
Unapishana na muda hakika/
Unachojua pekee we ni kufa kuzika/
Unanishauri nije kwako ndoa ikiyumba kanisa/
Kichekesho kwamba wewe ndio umeyumba kabisa ah!!/
Kanisa nilikuja uniongoze/
Nimpende mungu wewe unaifunza nimwogope,
Jua kali lilinifunza kukaba nikakupa maisha na cha ajabu haujanifunza chochote/
Nasikia una pande mbili za sarafu/
Upande mzuri na upande unaoingia dili mpaka na wafu/
Na unanifundisha baya haliwi na thawabu/
Nilikuwa mjinga na sasa nayabashiri majawabu/
Tunahitaji mafunzo halisia/
Wakati mbinu zako zimejaa mafumbo na sheria/
Kanisa tunaishi na wanafki kudadeki/
Unajifanya rafiki sababu ya ulafi wa chenchi/
Ikiwa huruma ya jah haina kipimo/
Basi kati ya wanaoomba msamaha nami nimo/
Dhambi zako sawa? Tumezidiana kimo/
Mungu aliye hai akuepushie shimo, kanisa huh! /
Umeshindwa kukidhi/
Utu unakutoka sababu umeshikwa na dhiki/
Unasahau lengo unasahau umesimamishwa na sisi/
Pesa inakuyumbisha nawe unayumbisha misingi/
Kijiwe chako hakikuniingia akilini/
Nikafata vijiwe vya pombe vikanitia umasikini/
Kisa kila aliyenionyesha nia nilimuamini/
Leo siwaoni wote wameingia mitini/
Haupo hata kwenye hadhi ya utatu/
Mungu Baba, Mwana, Roho kisa kazi za uchafu/
Kanisa hauchezi pasi ni rafu/
Unaremba altale kuliko hata nafsi za watu/
Kwa sasa ninahisi una bifu/
Na taasisi binafsi kwa sababu haukuwa mwangalifu/
Kama ndani yako wanaoishi wadanganyifu/
Na wanasali hautazalisha watakatifu/
Kuwa mkweli ni wapi ulipoishindwa nielewe/
Hiyo siri yako hauwezi ukaificha milele/
Kama nitachomwa moto wa kukushika ni wewe/
Nishakusafisha kuliko kujisafisha mwenyewe aah!! /