SEHEMU YA KWANZA – WASIFU

Nobody Is Safe 4 ni wimbo wa nne kutoka kwenye mtiririko wa nyimbo za Nobody Is Safe za Dizasta Vina, Wimbo umerekodiwa na kufanyiwa uchanganyaji sauti na producer Ringle beats kwa wasiomfahamu ndiye aliye-produce masterpiece nyingine za dizasta kama Hatia IV, Nobody Is Safe 3, Kanisi na nyinginezo, Ringle ndiye executive producer wa album ya The Verteller.

Nobody Is Safe ni nyimbo za majigambo moja ya desturi maarufu kwenye utamaduni wa Hip Hop ambapo msanii hudhamiria kuonesha position yake kwenye ulimwengu wa sanaa hii ya uchanaji. Humu Dizasta anaonyesha uwezo wa kuchana, kutiririka, mashairi ambazo ni sifa za kawaida kwa mwanahiphop lakini pia anatumia nafasi hii kuonyesha umuhimu wa uwepo wake kwenye sanaa. Kifupi ni sehemu ya CV inayoonyesha skills za msanii na mtiririko wa hizi nyimbo ni CV nzito sana.

SEHEMU YA PILI (MDUNDO/INSTRUMENTAL)

Kitu kinachoufanya huu wimbo uwe na utofauti si mashairi pekee, ni pamoja na mdundo. Kwa mara nyingine Dizasta na Ringle wanaonyesha a sparkle that can come out of their connection baada ya NIS 3. Original setting ya mdundo wa nobody is safe 4 ni Marekani ya mashariki, ambako cha kushangaza sio pande pendwa sana ya producer Ringle ambaye ni mnazi wa Dre ambaye anatokea West coast. MOOD yake ni mchanganyiko wa MYSTERY na HORROR  yaani hali kati ya kutatanisha na kutisha. Una drums za BOOMBAP au kama waswahili wanavyoita KUBUM KUBAM aina ya udundaji wenye asili yake jiji la NEW YORK marekani kutokea miaka ya 90.

Mdundo una mchanganyiko wa vitu vilivyopigwa kiuhalisi (original composition) na sampling (ukataji),

Sauti ya binti au mama inayosikika sehemu kubwa ya mdundo inaitwa sample inayoitwa SQUAD 1.  Kama ambavyo Eat ya Young Ma ilitumia sample iliyotumika kwenye Money power respect ya the Lox, sample ya NIS4 imetumiwa na producer Rastel kwenye beat inayoitwa Dilhun. (Dilhun by Rastel Beatz. https://www.shazam.com/track/571543996/dilhun)

Sehemu za beats zilizobakia zimepigwa live na Ringle ambaye ni mtaalamu wa kupiga keyboard.

SEHEMU YA TATU (LUGHA)

Wimbo wa NIS4 una stanza 28, zenye wastani wa mistari 4 kila moja. Kimahesabu wimbo una zaidi ya mistari 112. Kila mstari una wastani wa maneno 4 kila mstari, Kwa maana hiyo wimbo una zaidi ya maneno 448.

Wimbo una lugha tatu za Kiswahili (89%), Kiingereza (10.99%) na lugha yake mama ya Kinyakyusa (0.001%)

Na lugha hizi zipo kwenye formats 2, rasmi na isiyo rasmi.

Rasmi yaani lugha yenye mpangilio wa kiofisi (official language) upo kwenye sentensi kama SIJUI MWISHO ILA NAJUA NIENDE WAPI. Na isiyo rasmi yaani ile yenye mpangilio usio wa kiofisi(unofficial language) upo kwenye sentensi kama. “NIKO OG” au “HAWAJAANZA KIKI”.

WIMBO UNA MISAMIATI ISIYOTUMIKA MARA KWA MARA KWENYE MAONGEZI AU NYIMBO

Maneno kama;

ORTHODOX - mtindo au utamaduni usiobadilika
PAY CUT - punguzo la mshahara
INFINITY - isiyo na mwisho
SHEHENI - iliyojaa
LUBEGA - vazi la jamii ya Maasai na Jaluo, linaziba kifua kupitia bega la upande mmoja na kwapa la upande mwingine.
MARKING SCHEME - karatasi yenye majibu inayotumika kusahihisha majaribio
IMPECCABLE - yenye kiwango kikubwa
DRAWING BOARD - ubao wa mipango na majaribio
REASONABLE DOUBTS - kiwango cha ushahidi kinachotakiwa kufikiwa au kuzidiwa ili kumlinda mtuhumiwa kwenye kesi ya jinai
MUNDU - nyenzo inayosaidia kukata nyasi
PEEK A BOO - mchezo wa nyumbani ambao mtu mzima anacheza na mtoto, Anajificha uso kisha anajionyesha ghafla kumshangaza mtoto.

SEHEMU YA NNE (MATUMIZI YA LUGHA)

Wimbo wa NIS4 una fani kama zilivyo nyimbo nyingine.

Hizi ni baadhi

TASHBIHA —— Dizasta alilinganisha kitu kwa kutumia neno kama

Mfano

- Nasimama kama Eiffel tower naangaza jiji
- Kama nabii jinsi navyoitabiri kesho
- Asili kama Masaai na Lubega
- Controversial kama September eleven na Osama
- Kichwa kimetapakaa books kama library

TASHIHISI —— Dizasta alikipa uhai kitu kisicho hai

Mfano

- Jamii imeshiba sana ujinga
- Nasimama kama Eiffel tower
- Facts zina-shout beyond doubts
- Media wanaogopa nyimbo zangu kama Nudity
- Nimezika vitabu kichwani

SITIARI —— Dizasta amelinganisha bila kutumia kama au mithiri ya

Mfano

- Mi’ ni paycut
- Mi ni zigi ninayeficha stimu

LAKABU —— Dizasta amejipa majina ya ziada yanayoonyesha tabia yake kama msanii

Mfano

- Nageuka Kifo idea inayofanya mkakeshe church
- An orthodox delivery kama K DoT
- Simba wa Teranga
- Cobra

SEHEMU YA TANO (MTINDO)

Mtindo unaomtambulisha Dizasta Vina na kumtofautisha na wasanii wengine ni mfumo wake wa kutumia mchanganyiko wa akademia tofauti za kielimu

Mfano

Sayansi > kutumia terms mbalimbaliza kwenye field ya sayansi. Mfano maneno kama

- Gene pool (Jamii moja yenye aina mbalimbali za taarifa za vinasaba nb full population genetic information)
- Drawing board (Term yenye maana ubao wa kufanyia mahesabu, majaribio au kutunzia taarifa ambao unawekwa maabara au vyumba vya kujifunzia
- Maabara (chumba maalumu chenye hali ya kutengenezwa mahususi kwa ajili ya uchunguzi na majaribio)
- Medulla (sehemu ya nyuma ya ubongo maalumu kwa kusafirisha taarifa kutoka kwenye uti wa mgongo kupeleka kwenye sehemu za mbele za ubongo kwa ajili ya tafsiri na utekelezaji, pia huratibu kudunda kwa moyo na upumuaji)

History > kutumia terms za kihistoria

- NDULI (IDD AMINI DADA) - Afisa wa kijeshi na Raisi wa zamani wa Uganda kwenye miaka ya 70 ambaye anasemwa kuwa ni miongoni wa viongozi wakatili kwenye historia ya Uganda na Afrika mashariki.

Thiolojia > kutumia terms mbalimbali za kithiolojia kama
Kama NABII jinsi ninavyoitabiri kesho)
Utaishia kuomba msaada kwa MUNGU baba mwenyezi
Hapa wabaya wana-WORSHIP

Mithiolijia > Kutumia maneno ya elimu ya kusadikika au isiyoonekana kwenye ulimwengu wa kawaida

Mfano

Naishi kwenye DIMENSION ambayo MIUNGU tu ina-settle
Fahisi > kutumia maneno kutoka kwenye literature
Maneno kama SHAKESPEARE au AN ORTHODOX DELIVERY ni miongoni.

Jiografia > kutumia maneno kadhaa ya kijiografia mfano

Nasimama kama EIFFEL TOWER naangaza jiji
Kwanzia MANGUZI mpaka MWANZA

Utamaduni > kutumia maneno ya kijadi kuonyesha utamaduni fulani

JANGIRI waliyemkabidhu beto
Asili kama MAASAI na LUBEGA

Falsafa > kutumia sentensi zinazozalisha maswali ya kifalsafa mfano

- Nageuka kifo Idea inayofanya mkakeshe church
- Sijui mwisho ila najua niende wapi

Tehama > kutumia elimu ya tehama mfano

- Ma-CODE ya kiprogrammer
- My next bar is a cheat CODE no my last bar is cheat code every bar is too vital

Siasa na Intelijensia >  kutumia maneno ya field ya siasa na diplomasia za kitaifa

- Controversial kama SEPTEMBER ELEVEN na OSAMA
- Wulize MAKADA natema ngumu sana haumezi
- Sina makuzi ya kubuni VYAMA

Michezo > kutumia maneno ya kimichezo

- Simba wa teranga (timu ya taifa ya soka ya Senegal
- Nina nguvu zaidi ya DROGBA
- Defense to striker mode
- Ball player nadondosha record pro kama NBA athlete

Sheria > kutumia maneno kutoka uwanja wa sheria mfano,

- beyond your reasonable doubt

Stadi za kazi na maisha > kutumia maneno kutoka uwanja wa ufundi stadi

wanabadili angles napojadili NYENZO

Uongozi na utumishi > kutumia maneno kutoka kwenye uwanja wa uongozi na utumishi mfano

- Sauti ya UMMA natangaza RAI naeleweka

SEHEMU YA SITA: VIUNGO (REFERENCES)

#COBRA

Dizasta anasema “Master na-move ka’ Cobra”. Moja ya distinctive feature ya nyoka aina ya Cobra ni defensive displays zake hasa akiwa analinda mayai yake. Wana uwezo wa kusimamisha karibia theluthi ya mwili wake kumvaa au kumtishia adui, kutema sumu kwa umbali zaidi ya mita mbili, na wanapiga kelele (hissing) kukemea adui hata akiwa mbali. Tunafahamu how defensive Dizasta Vina alivyo kwenye kulinda uasili na uhalisi wa sanaa yake (Originality and Authenticity). Labda ndio sababu kuu si muumini mkubwa wa Media kubwa za Televisheni na Radio. Kukazia hili anasema “Nimejjficha ka’ kibabu cha imani, moyoni sina hila nimezika vitabu kichwani”

#DROGBA

Dizasta aliposema “nina nguvu zaidi ya Drogba” wengi wanadhani ni nguvu za mwili ambayo ni sifa tambulika ya Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Marseille na timu ya taifa ya Ivory Coast.  La hasha!! Mwaka 2005 timu ya taifa Ivory coast baada ya kuifunga Sudan kwenye mechi ya kufuzu kushiriki fainali za kombe la dunia walihitaji Egypt iifunge au at least wasuluhu na Cameroon ili wafuzu, Wakati mpira wa Sudan ni 1-1 Cameroon walipata penalty. Hii maana yake wakifunga basi Ivory Coast wasingefuzu tena, Pierre Wome akakosa na kumaanisha Tembo watacheza World cup kwa mara ya kwanza Ujerumani. Wakati wachezaji wakiimba kwa furaha Drogba akasimamisha sherehe na  kuomba kurekodiwa akiomba wananchi wa nchi yake kuungana na kuacha vita za wenyewe kwa wenyewe, Drogba alipiga magoti, wachezaji wenzake wakafuata, Machafuko yakaisha. Ndio nguvu Ambayo anaisema Dizasta.

#EIFFEL-TOWER

mnara wa Eiffel uliojengwa mwishoni mwa miaka ya 1800 ni alama kubwa ya nchi ya ufaransa. Dizasta anasema “Nasimama kama Eiffel Tower naangaza jiji, ambalo nipo tangu mastaa wa bongo hawajaanza kiki” akimaanisha Eiffel Tower ipo kabla ya structures nyingine kubwa kama Empire state na nyinginezo.

#SEPTEMBER ELEVEN

Inasemekana 2001 wanajeshi waliohusishwa na kikundi cha Al qaeda waliteka ndege 4  zilizobeba wafuasi wa kujitoa muhanga kuilenga Marekani. Ndege mbili zilielekezwa kwenye majengo ya World trade center New york, moja Pentagon na nyingine kwenye viunga vya Shanksville Pennsylvania. Watu zaidi ya 3,000 waliuwa na kufanya marekani kanzisha operesheni ya kupambana na ugaidi. September 11 ilizaa baadhi ya conspiracy theories. Wengine wakisema ni Mashambulizi ya kuigizwa (staged attacks) kuzalisha agenda dhidi ya Iraq. Wengine wakisema kuna serikali kuu ya dunia ilikuwa inaisujudisha Marekani baada ya kukosea, Wengine wakisema kulikuwa na nyaraka za siri za CIA na wizara ya ulinzi ya Marekani zililengwa kupotezwa. Wengine wanasema Pentagon ilivuja kiulinzi hivyo Serikali ilitumia Ndege za abiria kuficha aibu ya kulipuliwa na bomu na kutangaza ni Ndege za kawaida tu zilitekwa nk. Kuishi kwa hizi theories kunafanya kweli kamili kuwa ni kizungumkuti, Dizasta analinganisha level za uandishi wake na levels za controversy za issue ya September eleven na kusema “Ma-code ya ki-programmer, nani wa ku-compare Ball player nadondosha record pro kama, NBA athlete levels soo sana, Controversial kama September eleven na Osama”

#TIME-MACHINE

Ni kweli kwamba Msafiri kimuda hawezi kwenda future na kuuliza maswali ya kijinga kama, msanii gani anatamba? Fashion gani ipo kwenye peak nk. Atauliza maswali muhimu kama hali ya usalama, hali ya hewa na magonjwa mapya ya mlipuko ili akirudi wakati wa nyuma atoe taarifa zitakazoepusha future mbaya. Dizasta anasema,  “Emcee naishi future, ila nina maujuzi tangu jana, napitwa na upuuzi maana maufundi yamejazana” akimaanisha kuwa m ana-deal na masuala muhimu tu ndio maana masuala ya kipuuzi yanampita.

#GENE_POOL

Kibalojia, population kubwa ni very likely kuwa na genetic diversity. Yaani kunakuwa na uwezekano mkubwa kuwa na aina nyingi  za taarifa za vinasaba. Ile population inaitwa Gene pool yaani kwa kiswahili kisicho rasmi ni bwawa la taarifa za vinasaba. Dizasta anasema “Hii ni Gene pool si ya kuita nyimbo hii”

Akifananisha NIS4 na gene pool kwamba kuna diversity of information and aspects kwenye verse moja tu.

#NDULI

Mwl Nyerere alilitumja neno hili kwa Idd Amin akimaanisha mtu mbaya, wengi wanasema ni neno la kizanaki lililotoholewa na waswahili kumaanisha mtu katili au asiye na ubinadamu. Dizasta alisema “Maemcee hawanipendi kama Nduli” akijifananisha na Idd Amin ambaya inasemekana kutokana na ukatili wake hakupendwa na wazawa wa Uganda na walowezi wa kizungu.

SEHEMU YA SABA: WORD PLAYS

Baadhi ya wordplays nilizozivumbua kwenye NOBODY IS SAFE 4 ni

1) nakomaa sio simple licha ya kusemwa na WASENGENYAJI 😉
2) king of underground literally I’m down to the earth, hapa kwenye down to the earth kuna maana mbili, mfalme wa handaki ndio maana yuko chini, au down to the earth  akimaanisha kuwa humble!!
3) Amesimamisha kichwa kinamwaga madini 😉
4) NIMEKETI mahala ukweli UMESIMAMA
5) My next bar is a cheat code, no my last bar is a cheat code. Every bar is too vital (hapa anamaanisha Wimbo mzima ni Password)
6) Natema yai kama Vegan (Vegans hawali wanyama au vitokanavyo na wanyama hivyo Dizasta ana-assume kuwa Vegans wakila mayai watayatema, lakini kwa upande mwingine kutema yai ni kuongea lugha ya Kiingereza)

SEHEMU YA NANE: HOME WORK

 Kama kawaida Dizasta anatuacha tafakari,

  1. Kesho ni swali (Sijui mwisho ila najua niende wapi)
  2. Nini maisha baada kufa, tunasali kwa sababu ya hii hofu. (Nageuka kifo Idea inayofanya mkakeshe church)
  3. Nini kweli kuhusu September Eleven (Controversial kama September eleven na Osama)
  4. Kuna viumbe wengine nje ya hii sayari yetu (Naishi kwenye dimension ambayo miungu tu ina-settle)

SEHEMU YA TISA: RELEVANCE

kwa kiasi gani Dizasta anaongea ukweli?

  • Jamii imeshiba sana ujinga?

Dizasta anaamini material njema hazishiki chati za juu kwa sababu jamii inashawishika kirahisi na masuala ya kipuuzi. (Jamii imeshiba sana ujinga that’s the reason I’m not famous). Kwa kiasi kikubwa yuko sahihi. Kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita ukiangalia chati za nyimbo 20 bora za vyombo kadhaa vikubwa utagundua zimesheheni nyimbo zinazoabudu ngono na pombe na anasa kwa ujumla.

  • Ku-inspire the culture

Mwaka 2018 ambapo Dizasta alitoa wimbo wa HATIA II ikiwa ni sehemu ya pili ya Wimbo wa Hatia, Dizasta  alihamasisha utamaduni wa kutoa nyimbo zenye jina moja kwa mfumo wa muendelezo. Kutokea hapo Wasanii wengi wamefuata huu utamaduni ambao asili yake ni MEDIAVEL LITERATURE ULAYA. Msanii Maarifa akaja na Series yake inaitwa MAARIFA YA MAARIFA, Boshoo akaja na series yake inaitwa GIFT FREESTYLE. Young Killer akaja na SINAGA SWAGA, Rapcha naye akaja na series akaiita LISSA.

Kama utachunguza Hatia I na Hatia II au hata Ndoano ni nyimbo ambazo Dizasta amerap kwenye ara za muziki usio na drums zaidi ya progressive melodies tu, na zote zinahusu mapenzi na usaliti. Alafu anakaa katikati ya kuchana na kufanya spoken words. Haikupita muda tukasikia nyimbo kama A NEW GIRLFRIEND STORY ya Young Killer, Lissa ya kwanza na pili za Rapcha, huku Hatia III zikishabihiana na nyimbo kama Darasa huru au Who I Am za Nacha.

Wanaomfahamu Shaulin hawana haja ya kujiuliza, Shaulin ni carbon copy ya Dizasta kwanzia flows hadi vituo.

Kwa hizo analysis naweza kusema Dizasta amemaanisha alichosema kuwa “Style yangu ime-inspire the culture

Ime inspire the Nengos, the Shaulins, the Nachas
The Boshoos, the Killers, the Maarifa, the Rapchas
Nimeacha DNA hata nikidanja sina deni tena”

  • An orthodox delivery

Dizasta ni miongoni mwa wasanii wachache ambao hawajawahi kwenda nje ya midondoko yake ya asili. Yaani a laid back flows huku akiwa slightly late on go kwenye beat za boombap. Anasema (an Orthodox delivery since wayback kama K Dot) akijifananisha na Kendrick Lamar yuleee wa OVERLY DEDICATED

  • Kuishi Future

Dizasta ana msimamo wa kimapinduzi kwa upande mwingine. Mara kadhaa ameimba kuhusu kubadilisha fikra na tabia zetu kwa ajili ya afya za jamii zetu, Dizasta ametangulia kuachana dini za kimapokea ya kimagharibi, ubazazi dhidi ya wanyama na makundi athirika kwenye jamii. Ni aina ya lifestyle ya kesho kwa nchi zetu ndio maana anasema “Emcee naishi future ila nina maufundi tangu jana

  • Kukumbatia asili

Dizasta ni mzalendo wa baadhi ya tamaduni za asili za ki-africa na mara kadhaa ameimba kuhusu umuhimu wa kuzikumbatia tamaduni hizo mfano kwenye wimbo kama HATIA III, KANISA au WIMBO USIO BORA. Kwenye NIS4 anasema “Asili kama Maasai na Lubega”.

Makala haya yalichapishwa kwanza kule Twitter na Dizasta Vina ambae ndie mchambuzi hapa.