Dr. Luis

Kumpata Dr. Luis ilibidi tuzame “Chini Kabisa” kwa usaidizi wa ma emcee Adam Shule Kongwe na Javan “Chuna” Ngozi. Kazi hii ya CK pamoja na “Grenades From North” ya Rap Poetic Grenades (RPGs) ndio iliniwezesha mimi kutaka kujua kuhusu Daktari huyu wa midundo anayepatikana Kaskazini mwa Tanzania. Tulia, soma makala upate dozi kutoka kwa Daktari bingwa, North Block Records.

Skia Playlist ya Dr. Luis hapa

Karibu sana Dr. Luis hapa Micshariki Africa...Dr. Luis hivi hili jina ni lako halisi na wewe ni daktari wa kweli au wale ma dokta kama Dr. Shule na Dr. Dre?

Luis ni jina langu halisi lakini mimi sio daktari kitaaluma, na kuitwa Dr Luis ni artists wenyewe walinibariki hiyo nickname.

Wewe ni dokta wa nini?

Mimi ni daktari wa midundo…

Naomba tukufahamu majina yako rasmi, unatokea wapi na unajihusisha na nini?

Majina yangu rasmi ni Luis Elisa Markos, natokea Arusha najishughulisha na Music Production.

Tueleze kuhusu maisha yako kaka ulizaliwa wapi, ulisomea wapi na kitaaluma umejikita kwa kitu gani? Luis tueleze kuhusu utoto wako ulikuaje?

Nimezaliwa Arusha (Mount Meru Hospital), nimesoma Enyuata & Ngarenaro Primary Schools… Kindoroko Sec (O - Level), Lyamungo Sec & Arusha Meru (High school)… UDOM (Bachelor Of Arts, Tourism & Cultural Heritage Management)...

Utotoni nilikuwa mtulivu na msikilizaji mzuri wa muziki haswa Hip Hop na Reggae kutokana na kaka zangu walikuwa wakinunua hizo tapes na kujikuta nipo ndani ya ulingo.

Dr. Luis tueleze historia yako inapokuja kwenye maswala ya utayarishaji, ulijikutaje hapa?

Kwa ufupi tu kwenye utayarishaji wa midundo nilianzia ghetto kwangu baada ya kununua computer nikiwa na rafiki yangu anayeitwa Alex ambaye kwa sasa amejikita zaidi kwenye michano na kuacha beat making… Muda ulipita kidogo akatokea Nonstop na High Smoke hapo nikaona ni vyema sasa tuanzishe studio yetu 2008 kwa msaada mkubwa wa baba(R. I. P)…

Binafsi mimi nilikufahamu kupitia mradi wa Adam Shule Kongwe na Javan, “Chini Kabisa” kabla ya kudaka nakala ya RPG's, “Grenades From North”. Hebu tupe hapa orodha ya miradi yako mingine ambayo imetoka chini ya usimamizi wako...

Miradi ni mingi tuliyoiandaa North Block Records ambayo imetoka na mingine bado haijatoka.

 1. The Mix Gefenx by High Smoke
 2. 7 O'clock ya Alex & Digalar
 3. Hip Hop Maasai ya Wadudu Wa Dampo
 4. Wadudu Asilia ya Wadudu Wa Dampo
 5. Grenades From North ya Rap Poetic Grenades (RPGs)
 6. Angserian Project chini ya Omega 5
 7. Mangi Sabas ya Fedoo
 8. 8. Chi Mixtape ya Adam Shule Kongwe
 9. Dr. Shule ya Adam Shule Kongwe
 10. Chini Kabisa (CK) ya Adam Shule Kongwe & Javan (Chuna Ngozi)
 11. VUTA PICHA by Kung Fu Kanja
 12. Kutoka Kwangu Kuja Kwenu (KKKK) ya Adam Shule Kongwe
 13. Nyota Ya Mizani ya SlaiYank
 14. Mashariki Ya Fikra ya Micshariki Africa, Fedoo na Msito (Vocals)
 15. Tangu Tumboni ya BooxKCK
 16. Chronic Tape ya Lule (Unreleased)
 17. Borbo Crew ya Mtalebano (Unreleased)
 18. Chini Ya Reli ya Uncle D (Unreleased)
 19. Rap Game ya Bubamangi
 20. Olo One Kikosi

Wewe binafsi una miradi yako iwe ni beat tape, album, ep au hata mixtape?

Mradi wangu binafsi nategemea kuachia mwaka 2024 nikiwa nimewashirikisha wasanii tofauti wa hapa Arusha pamoja na mikoani.

Ofisi zako North Block Records zinapatikana wapi na huwa mnajihusisha na nini ?

Base ya North Block Records ipo Kambi Ya Fisi japokuwa kwa sasa studio inapatikana Sakina opposite Night Park Resort… Studio inajihusisha na audio production in general.

Na je hapo North Blocks nyie mmesajili wasanii wowote ambao wanakuwa wana mkataba na nyie?

Wasanii ambao kwa sasa tunafanya nao kazi ni Rap Poetic Grenades (RPGs), Lu Da Chronic, Bubamangi na Emgeez.

Kama mtayarishaji unakabiliana na changamoto gani ki kazi na unazitatua ki vipi?

Changamoto zipo kila mahali chini ya jua…Lawama huwa zinatokea pale unapokataa kufanya kazi na msanii kutokana na kiwango chake kuwa chini, issue za usela kwenye kazi… Hatua nazochukua ni kumuelewesha artist mpango kazi ulivyo na asipoelewa ni kumkataa tu, studio zipo nyingi hapa town.

Utayarishaji ni karama au mtu hufunzwa?

Kwa upande wangu naona zote ni sahihi, lakini vikienda kwa pamoja huwa bora zaidi.

Msanii anapokuja kwako mfanye kazi mchakato wako kutoka umpokee mpaka mfanikisha kazi yako ni ipi?

Cha kwanza namsikiliza nikiona anaweza basi taratibu nyingine za ufanyaji kazi hufuata.

Je unaona kama watayarishaji wa muziki hususan wa Hip Hop wanapata heshima wanayostahili?

Heshima wanapata japo sio kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na wanaofanya genre tofauti.

Dr. Luis pia ulipata fursa nzuri ya kuhusika kwenye uandaaji wa mradi wa Micshariki Africa, “Mashariki Ya Fikra”. Unajiskiaje kuhusika kwenye kazi hii na mambo yaliendaji mlipokua na Fedoo studio, jamaa ni one take au ilibidi mrudie mara kwa mara? 😄

Najivunia sana kushiriki kwenye mradi huu kwa kuweza kuwa sehemu ya team iliyofanikisha mradi huu… Fedoo ni mmoja wa emcee hatari sana kuwahi kutokea na tukiwa studio ni one take hakosei… Hadhira inatakiwa impe sikio na kusapoti miradi yake aliyoiandaa na anayoendelea kuiandaa.

Hali ya Hip Hop Arusha ipoje, Utamaduni upo vizuri au umefifia watu wameamua kuutosa? Nani baadhi ya ma emcee inatakiwa tuwape skio ambao wanakuja  kwa kasi?

Utamaduni wa Hip Hop Arusha bado upo imara sana. Ma emcee wa kuwapa skio wanaokuja kwa kasi ni kama Walady Family, RPGS, Tejo Clan, Emgeez Gang, Bubamangi, Thug Truth, Mox G, Wadudu Wa Dampo, Bero claw etc.

Tukimalizia tupe neno lako la mwisho na utueleze wasomaji wetu wanaweza kukupata wapi kwenye mitandao ya kijamii pamoja na simu

Mwisho kabisa nawashukuru wanaoendelea kusapoti utamaduni huu wa Hip Hop kwa kununua kazi za wasanii pamoja na Micshariki Africa kwa kuendelea kuwa jukwaa imara zaidi la Hip Hop Afrika Mashariki.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza ukanipata kupitia

WhatsApp: +255752130157
Instagram: @northblock_records
Facebook: Luis Markos

Shukran sana kwa mda wako Dr. Luis....

Pamoja sana 👊🏽