Wimbo: Kitanda
Toka kwa: Duke Tachez ft. Fivara
Mradi: Father X-Mas
Tarehe iliyotoka: 26.12.2023
Mtayarishaji Mixing & Mastering: Duke Tachez
Studio: MLab

Fivara

Intro:

Yeah yeah/
Magokoro na Father Xmas round hii/
Yeah/

Beti Ya Kwanza

Umbo lake ni mstatili na miguu mine/
Kina mengi ya kujadili hadi kuundiwa tume/
Toka BC mpaka Yesu na Mtume/
Ni sehemu ya kurelax migongo yetu isiume/
Ni kifaa muhimu tuulize wanaume/
Tunapotoa vitu adimu na kuuliza kama ume-/
Enjoy, “kama hujaenjoy basi sema”/
Haujakiwasha homeboy huyo haji tena /
Masculinity inapimwa sio kitoto/
Wasikulimit ndio zinakopikwa ndoto/
Kipewe heshima wanakozaliwa watoto/
Wagonjwa wanahangaika na kupitia msoto/
Tunapolala na wengine pia kufa/
Tunapozikosa jala kwa kutoachia shuka/
Tunaponjunja, kula nyeto na kuwaza/
Kupumzika unapoibuka ghetto kujilaza/
Unapotulizia hasira endapo wamekukwaza/
Au zikikushika hasira shambulizi unakopanga/
Ni ghala ya silaha uvunguni kuna panga/
Hata kama kuna taa uvunguni hakuna mwanga/

Kiitikio

Mambo mengi yanatokea kwa kitanda/
Kuna mazuri ya kishenzi pia majanga/
Kwa hizi tenzi kuongea nimejipanga/
Binadamu kabuni mengi hakukosea kwa kitanda/

Mambo mengi yanatokea kwa kitanda/
Kuna mazuri ya kishenzi pia majanga/
Kwa hizi tenzi kuongea nimejipanga/
Binadamu kabuni mengi hakukosea kwa kitanda/

Beti Ya Pili

Tunapo-lay low, kupiga story, kusomea/
Iwe madesa ya shuleni ama story na ngonjera/
Story na masela zinakopigwa za kutosha/
Unapochill ukiweka vocha na kuanza kuongea/
Unaporudi kudondosha ukiwa umechoka/
Baada ya kusota ama stimu kukolea/
Unapohitaji utulivu hiyo ndio sehemu husika/
Unapohisi maumivu hiyo ndio sehemu ya kufika/
Iwe ni tatu kwa tano, iwe ni sita kwa sita/
Iwe ni cha laki tano, iwe cha kuanzia maisha/
Chochote kile, pallet, chuma, double decker/
Pa kuombea msamaha mwenza kanuna kaboreka/
Najitupa baada ya kula nguna nimetosheka/
Ndoto nyevu nakitupa na mashuka naloweka/
Hakibagui uwe mzima, uwe na dozi/
Hakichagui uwe sinner, uwe mkombozi/
Wenye chozi utawafuta, vikojozi utawakuta/
Wanga wanawanga usiku, watu wanadozi na mifupa/
Ambao hawatumii vyao, uh labda Walozi/
Pornographers ofisini na mapozi watakupa/

Kiitikio

Mambo mengi yanatokea kwa kitanda/
Kuna mazuri ya kishenzi pia majanga/
Kwa hizi tenzi kuongea nimejipanga/
Binadamu kabuni mengi hakukosea kwa kitanda/
Mambo mengi yanatokea kwa kitanda/
Kuna mazuri ya kishenzi pia majanga/
Kwa hizi tenzi kuongea nimejipanga/
Binadamu kabuni mengi hakukosea kwa kitanda/

Beti Ya Tatu

Make your bed, you gone lay in it/
Chunga kisiwe cage, you gone stay in it/
We muda jipoteze nisikuongopee/
Itafika stage you gone pay in it/
Kinaweza kuwa divine, kuwa evil/
Kikakuweka kwenye line au kukupa matatizo/
Kitumie vizuri pindi ukipata likizo/
Amka fanya mazoezi usijepata shinikizo/
Tulia kokotoa matumizi, maingizo/
Ndiko idea tunakotoa hatuigizi maigizo/
Usichokilalia haujui Kunguni wake/
Oya usichokilalia haujui uzuri wake (Utajuaje?)/
Hivyo usijitoe ufahamu/
Hakizai haramu basi mtoto mzuri aje/
Uzuri kila mtoto anakuja na sahani yake/
Haujui kila msoto unakuja na amani yake/
Maamuzi ni yako ukakaze ujikunyate/
Japokua ni chako usijidumaze kazifuate/
Fursa zaidi ya kumi, vaa shati usimame/
Ukapambane maana mtaka cha uvunguni sharti ainame/

Kiitikio

Mambo mengi yanatokea kwa kitanda/
Kuna mazuri ya kishenzi pia majanga/
Kwa hizi tenzi kuongea nimejipanga/
Binadamu kabuni mengi hakukosea kwa kitanda/
Mambo mengi yanatokea kwa kitanda/
Kuna mazuri ya kishenzi pia majanga/
Kwa hizi tenzi kuongea nimejipanga/
Binadamu kabuni mengi hakukosea kwa kitanda/

Outro:

Yanafanyika mauaji/
Wengine wanafanya maombi, sala, dua au meditation/
Unajua? /
Hah hah/