Toka kwa: Eddy Mc
Wimbo: Huruma Kwa Wagonjwa
EP: Mbio Za Wenge
Tarehe iliyo toka: 12/07/2021
Mtayarishaji: 10th Wonder, Black Junior, Dr. More
Studio: 99Records, Punchline burudani
Ubeti 1
Kuna muda inahitajika faraja kuliko pesa/
Nayo pia tu inakuja vile tulipo pema/
Bado tunzi za Kanchape kwao ndio wimbo pendwa/
Busara Ni kuishi nao labda kesho sipo tena/
Unaweza kulia wewe baada ya kumuona mgonjwa/
Ila mgonjwa akacheka baada ya wewe kukuona/
Ukamkumbusha kipindi ye yupo mzima/
Anafanya michakato anapata kipato kiaina/
Anakula bata nyumbani anapaacha safi/
Mke mahitaji anapata na mkwanja anakata nice/
Upone haraka na urudi ulingoni/
Kijiwe wanaulizia mjomba fure kulikoni/
Afya ina maadui kibao sema hatuwaoni/
Na sisi tumekua viburi Sana hatukomi/
Ila nature inatulinda km bodyguard/
Mask off nadundika bila worry man/
Kiitikio
Chorus,fanya kama umeguswa kwa yote yanaowakuta/
saidia unapoweza Vita ya uhai kubwa,×2/
saidia unapoweza Vita uhai kubwa,×2/
Ubeti Wa Pili
Wengine Ni tegemezi basi hofu Ni Top/
Miguu inaning'inia juu Hospital/
Wanaisakama nafuu so kidogo/
Fanya ukawape moyo tu so kisogo/
Vifo vingi hutokea kwa kukosa msaada/
Japo uwape chochote inatosha kwa sana/
Sio na ma camera kama unashoot scene/
Mwenzio ana maumivu mguu haushuki chini/
Mtu anagonjoa amini haifai deshi/
Usichukulie poa peleka ata chai fresh/
Leo unaringa upo mzima ila kesho mashakani/
Ajali uja popote ata ukikaa tu maskani/
Utashangaa! Gari imeacha njia imekuvaa/
Kiuno kimeitikia umekaa/
Basi tuwe karibu na watu wenye Hali ngumu/
Kuna mengi yanawasibu na bado hawanywi sumu/