Harakati za 8town Crew Graffiti zilianzishwa nchini Kenya na kuleta matokeo chanya kwa kuanzisha Elementz Kenya, jukwaa la mtandao linalounda nafasi mahiri na ya kiubunifu inayo angaza vipengele 5 vya Hip Hop pamoja na kuandaa mazingira mazuri kwa ajili ya watu kushirikiana na kuungana na ili kuweza kuonesha vipengele hivi vya Hip Hop na jinsi vinavyoweza kuonekana na kupatikana kwenye sanaa tofauti.





Tukio hilo lilifanyika Jumamosi tarehe 24 Februari huko Muringa Studio za Tipo, Muringa Road Adams Arcade, Kilimani kuanzia saa saba mchana. WBG a Graffiti Wrew chini ya 8town-crew pamoja na washiriki wake Rigo Diaz, ish_artlives, Stic One, Ebrah, Daddo, Sess, Slick, Swift 9, Detail7(Spray UZI) na wengine wengi walichora kuta kwenye nafasi za wazi ambazo zilitolewa kwa wasanii wa graffiti ambao walishiriki kama vile Kyymist , Snarloxx kutoka Marekani, Jr Penseli, n.k na maonesho ya muziki kutoka kwa wanamuziki chipukizi na wakongwe kama vile Syntax Era, One Bullet, Tangale, Rufnek, Shazzy B, mshairi Teardrops, Micko Migra na uzinduzi maalum wa toleo la muziki na Tribe 53 ft Girongi Oya.
Pia kulikuwa na muziki kutoka kwa wazoefu kama vile Nafsi Huru, Kayvo Kforce, Mdudu Dudu, G Hunter, Man Njoro ambaye alipamba jukwaa na kuleta matokeo chanya kwa wasanii wapya. Hili kwa hakika lilifanya tukio hili kuwa darasa la muziki la ushauri ambalo lilizidi hali ya kawaida ya watu kwenye hafla, kwa mtazamo wa maneno Elementz Kenya sio tu tukio la kawaida la Hip Hop bali ni mtandao mpya wa kuinua muziki wa Hip Hop K nchini Kenya na Afrika Mashariki.







