Uchambuzi Wa Album: Born Free Compilation Album
Emcee: Elijah Moz
Tarehe iliyotoka: 04.07.2023
Nyimbo: 13
Midundo: Kunta Official Beats, Dez Shitstrumentals, Hefe, JT, Charawe, Nzive Beast, Nick Wathi, Buff G, CMG Records
Mixing & Mastering: Kunta Official Beats, Ananda A World, Buff G, JT, KD Keslam, Hefe
Studio: Nawiri Records, Truce Label, Make It Loud Records, CMG Records, Andromeda Records, Essen Records, JT, Uptown Records

Nyimbo Nilizozipenda: Konshens, Kimangoto, Lugha Ya Dooh, Hebu Shhhh, Resistance, Mbogi Mbwegze,

Elijah Moz

Elijah Moz mwaka jana baada ya kimya cha mda mrefu alirudi tena na mradi wake “Born Free” ambayo ni compilation album mzuka sana. Emcee huyu ambaye ni nusu ya kundi la SoulMates Music aliona ni freshi atukumbushie kua bado yupo kwenye game na bado ana mazaga kibao kwa ajili ya mashabiki wake.

Mradi huu ambao umewashirikisha Nigress, Flamez, Djungle, Flaco, Eslam, Young Bradley, Jimwat, Illicit, Rish, Buff G, Kev Mamba unafunguliwa rasmi na ngoma ya Dandora Cinema ambapo emcee huyu anatamba akitueleza story za maisha yake ya kitaa juu ya vinanda vya Kunta Official beats.

Kitu ambacho kilinivutia sana kwenye mradi huu ni mashairi ambayo yanagusa sana jamii. Mradi umeongelea maswala kama changamoto zinazotukabilii kitaa, ‘Dandora Cinema, maswala ya usakakaji hela, ‘Lugha Ya Dooh’, majigambo ya msanii, ‘Hebu Shhh’, na kutetea na kusimamia haki zetu na ukweli pia ‘Resistance’.

Pia kuna ngoma inayotuhimiza tujiamini na kupigania ndoto zetu, ‘Never Said’ akiwa na E-Slum pamoja na ‘Awesome God’ inayotumia sampuli kutoka ngoma flani inayoenda kwa jina hilo hilo ambayo ni ngoma yakumshukuru mwenyezi Mungu kwa ajili ya wema wake.

Kwenye ‘Moshi Mbwegze’ akiwa na Djungle pamoja na Flaco jamaa wanaongelea mambo ya ganja kwa njia ya ucheshi sana. Pia kwenye album kuna ngoma ambazo SoulMate Music (Elijah Moj na Nigress) kama vile ‘No Apologies’ na ngoma yao pendwa kutoka kwa wawili hawa ‘Konshens’. Kwenye ‘Konshens’ wawili hawa wanatuhamasisha kujiamini kwa chochote tunachokifanya, anasema hivyi Nigress kwenye kiitikio na sauti yake mzuka sana,

“Niko na swali la Konshens/
Calm yourself I don’t mean no offence/
Una tell those una pretend/
The way you living ma’ it make no sense/
Soon you got to realize that you are royalty sitting on a dream/
Better make the sacrifice you need to reach your possibility/”

Kwenye compilation hii pia kuna cyphers kadhaa ambazo utazipenda pia. Elijah Moz ametangaza ujio wake kwakuzaliwa tena na hakuna kitakacho mzui kufikia malengo yake kwani yeye ni ‘Born Free’