Wimbo: Hali Zetu
Msanii: Elikizo
Mradi: Book Of African Poem (BAP)
Tarehe iliyotoka: 04.03.2023
Mtayarishaji: Jegalla OG
Mixing & Mastering: Jegalla OG
Studio: Old Garage

Beti Ya Kwanza

Kujibana hawaoi vijana wanajimaster/
Walalahoi wenye dhamana ni mapasta/
Huna kosa unapigwa na polisi/
Bila ubishi wanajitosa kukufilisi/
Haukidhi mshahara mtumishi havai Kaunda/
Wauza ndizi biashara haizai matunda/
Mfumuko wa bei kila uchao madhila/
Ubao mizunguko yote per day bila bila/
Dili zimelock nywila, hazitengamai hila/
Hazilipwi fadhila, Kati ya Lila na Fila/
Yalifanya mapenzi kipofu akaona wivu/
Usienzi ushenzi hofu inaua live/
Wakaka wanaotoga wanaliwa viboga/
Wengine wapaka poda wanajiuza kwa oda/
Hustle zaidi ya mchacho, hakuna tupatacho/
Chako kidogo ambacho, vigogo hujia kwacho/
Tulale macho, wasitawale wenye nacho/
Mamlaka ya mapato wanataka makato/
Kwa battle, hawajali hujamake mchakato/

Chorus

Hali zetu halisi, maisha sio rahisi/
Tukipata buku tunakula jero/
Huku makapuku ndio tumejaza selo/ x 2

Beti Ya Pili

Kupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma/
Unaweza soma degree ukazidiwa na diploma/
Inapogoma Plan B sangoma hawi reformer/
Kuchagua kazi unajichoma utaibukia koroma/
Si wametutelekeza sababu ya Umangimeza/
Choko mchokoe pweza binadamu hutomueza/
Kifupi Jino la pembe sio dawa ya pengo/
Ukiwa mzembe hawakupi tafu wanazengo/
Jihadhari kipya kinyemi ingawa kidonda/
Ukimwi hawasemi upo digitali hutokonda/
Kumbe ndugu chungu Jirani mkungu/
Na Mzungu hawezi kuwa Mungu/

Chorus

Hali zetu halisi, maisha sio rahisi/
Tukipata buku tunakula jero/
Huku makapuku ndio tumejaza selo/ x 2

Beti Ya Tatu

Utalaumu watu, ukiendekeza uchawa/
CCM wakuone fyatu ukibeza Ukawa/
Maisha ya ma fighter sio tu kuwa taita/
Ukiacha insta, fesibuku na Twitter/
Patashika uswahilini Bet kuuza roho/
Kusaka dough baharini tunauza roho/
Kusaka dough barabarani tunauza roho/
Utakabwa koo chochote tule kinywani/