Toka kwa: Elisha Elia
Wimbo: Venye Itakua
Albam: Bazenga EP
Tarehe iliyo toka: 2019
Mtayarishaji: Bigbeats Afriq
Studio: Big Beats Afriq

Beti ya kwanza

Yeh! Binadamu wengi wanafiki sai/
Hata wafuasi wa Yesu bado walimcritise/
Ukisleki watapanga kukumanga/
Ukidedi wana party wakichanga kwa matanga/
Mhh! natanga natanga mpaka kieleweke/
Ukileta pang'ang'a tunakuchanja hata bila machete/
Mpaka mambang'a gava imewapiga teke/
Mipaka na panga nivuke pia inahitaji ndege/
Damn! ndio maana me huwanganga niko high/
Hatupendi mihadarati lakini ngwai huwa ni uhai/
Shikwa mashati kama ganji yangu me nakudai/
Hatujapata Uhuru na tunaongozwa na Muigai/
Six feet deep huwanga shimo ya kila mtu/
Me ni bigting wanabonga kunihusu/
Niite king king hao wengine huwanga ni mabusu/
Murder each beat na mistari utadhani ni Kungfu/

Beti ya pili

Hatutachoka kutafuta/
Usikufe moyo ngoja yako inakuja/
Hata kibogoyo huweza kutafuna/
Walijifanya wachoyo wanatuona tukivuna/
Hehe, the only rapper ana flow vi-fine/
Nani mwingine ka si Elai na huwezi deny/
Kuna wengine hawataki mimi kuniona live/
Lakini Mungu ni yule yule bado tuna climb/
Tulichorea crime sai ni pen na mic men/
Huwezi deny baraka yenye Mungu amenipee/
Na sishangai kuona muda inafly ju/
Kuna matime huwezi gundua nini inakuja next/
Walidhani tuko palepale/
Watiaji tunajua wanakwanga walewale/
Leta PiliPili niongeze Morale/
Wikendi ikiwa fiti tunashukuru ma-Barley/

Daraja

Asikwambie mtu hautamake it/
Mungu ndio analeta Mungu bado ndio anatake it/
Life nikujikaza siku itafika/
Utakubalika kila pande utasifika/
Fanya chochote unapenda men/
Usijali hata ka wanakulenga then/
Usiworry wakilisha represent/
Kuna siku macitizen watakuja kukupa 10/10!