Careem Akiiwakilisha Mitaa Anayotoka Ya Mombasa.

Mwaka ndo umeanza hivyo na emcee Careem kutoka Mombasa ndo wa kwanza kutufungulia mahojiano na wasanii wetu kutoka Africa Mashariki. Careem ni mmoja wa ma emcee kutoka Mombasa ambae ana peperusha vizuri bendera ya Hip Hop kule nchini Kenya na kutokana na kazi yake mpya tukaona ni vyema tupige nae gumzo ili tujue nini tutarajie kutoka kwake mwaka huu wa 2025.

Careem ni karibu miaka miwili tangu tulipo fanya mahojiano yetu ya kwanza? Unaendeleaje kaka?

Poa sana Micshariki Africa. Naendelea poa, shukran kwa maulana.

Mara ya mwisho tulipo ongea ulikua umeachia EP yako...baada ya hapo ni miradi gani umeachia tena ambayo mashabiki wanapaswa kuijua

Ndio, nakumbuka niliachia EP yangu ya kwanza ‘Talent Ipo.’... baadae nikatoa mixtape ya pili, ‘Hapa Bars Tu Vol. 2’ inapatikana YouTube na Audiomack. 

Kwa huu muda tunapoongea najitayarisha kutoa EP ya pili, ngoma mbili tayari zimetoka ‘Hunger For The Mic’ niliyomshirikisha rap battler mkongwe kutoka Kenya, Harry Lee na underground Hip Hop rapper/emcee PTah anaeishi Uingereza. Ngoma ya pili iliyotoka ni ‘Rap Up 2024 -254’...

Vipi hali ya muziki wa Hip Hop Mombasa na Kenya ki ujumla?

Hali ya mziki wa Hip Hop Kenya na Mombasa inazidi kukua, vijana wa kizazi kipya wanajituma kwa mfano kina Emkay 64... anakipaji kiziuri cha ‘rap-sing’, niiteje rap kuimba hahaha.  Dildz pia anajituma kwenye rap. Alafu mzee mzima wa hiki kizazi Careem nawakilisha tasnia ya mistari vilvyo hususan Hip Hop chini ya handaki, Pwani na Kenya kiujumla.

Tukiongelea Kenyan Hip Hop inazidi kukua, wasanii wengi wanafanya poa, kazi zao zinaonekeana. Big up kwao na kwangu!

Careem Na Mural Ya Mwendazake PMG The Producer (B Records)

Mwaka huu umetufungilia mwaka na kitu kipya, kitu tofauti...tueleze kuhusu ngoma yako mpya 'Rap Up 2024 254'. Kazi hii ilisimamiwa na mtayarishaji gani kutoka kwa uandaaji wa mdundo mpaka mixing and mastering?

Yes ilikua ajab sana kwa wasanii wengi, ilikua siri kati yangu mimi na producer wangu Musa Kiama. Nilimuelezea kuhusu hili wazo tokea mwezi Septemba 2023, kua nina nia kufanya kama vile Uncle Murder [anavyofanya kila mwaka], akaniambia,”Wewe fanya bro uko poa ki mistari...” Mwanzo wa mwaka 2024 akaunda mdundo nikaupenda...

Kuanzia Januari 2024 nikaanza kuandika matukio yote yaliyotokea nchini Kenya ambayo yali trend kwa notebook tu na ilipofika Desemba tarehe 2 nikaanza chonga mistari...na ilipofika Desemba tarehe 26 nikawa ninemaliza mistari yote.

Zoezi la siku tatu [la kukariri na kuchana mistari yangu] na kisha tarehe mbili mwaka mpya tukarekodi pale Kubwa Studio kwasababu mtayarishaji wangu Musa alikua busy hiyo siku, hivyo  hatukuweza fika studio yake ku rekodi... na hivyo ndo wimbo wangu wa ‘Rap up 2024 254’ ulizaliwa.

Kwa hiyo mdundo uliundwa na mtayarishaji Musa Kiama wa B Records ila tuli rekodi Kubwa Studios, Mombasa.

Nani alihusika kwenye kuandaa ile video?

Video iliundwa na videographer wangu Bullet Shots, same person aliunda video yangu ya pili so ‘Ghetto Freestyle’.

Je inspiration ya kuanzisha ripoti hizi za mwaka lilitoka wapi?

Inspiration ilitotka kwa mchanaji wa kutoka Marekani, Uncle Murda. Mimi ni shabiki wa hizo kazi zake za ‘rap ups’ mbaya toka azianzishe!

Idadi ya beti au mistari iliyo andikwa kule ni kiasi gani?

Mistari kiujumla ni 124 kama sijakosea, hahaha, sababu wakati wa kuandika sikuwahi hesabu ila beti ni 31 no kiitikio kuimba ni mara kumi...

Je hizi rap up zako ndo zitakua fungua mwaka yetu kutoka kwako kila mwaka?

Bila shaka toa shaka hili litakua jambo langu Kenya. Nia ya kufanya jambo hili nikuonesha Pwani kuna vipaji, kua tuna uwezo mkubwa katika utunzi. Nitaendelea kuwakilisha hili wazo la ‘rap up’ hadi mwisho wa maisha yangu. Niombeeni afya na uzima.

Mapokezi kutoka kwa mashabiki yamekuaje?

Walistaajabu sana na kunisifu. Nyimbo ilifanya vizuri pale TikTok kwani iliangaliwa na zaidi ya watu alfu tatu, jambo ambalo lilinifurahisha sana mimi binafsi.

Kwenye hii ngoma umegusia matukio ya kitaifa na pia yale yaliyotokea kwenye kiwanda cha muziki na sanaa. Je pengine kuna watu uliowataja humo ndani ambao wamelalamika?

Hapana, sidhani kama kuna yoyote amehisi kama nilikua na ubaya na ngoma ile. Natutumai wameichukulia kazi ile kwa uzuri kutokana na umahiri wa utunzi wa mashairi yangu. Kuongezea naweza sema nilio wataja nimewataja kiheshima, sikufanyia mtu istihzai zozote kwani nilitaja visa/matukio kulingana na matukuio yalivyotokea.

Pia nimeona sehemu flani kwenye video chata la 'P-Mani Records'. Kwani umesajiliwa kule au hii ishu imekaaje?

C.E.O wa hiyo label (P-Tah (Wa Furu)) alipendezwa na hiyo kazi akaamua kusimamia uandaaji wa video hiyo. Kwa ufupi nadhani hiyo taarifa inajitosheleza kuhusu maswala yetu na P-Mani Records. Mengine zaidi yakijiri mtaya shuhudia.

Tukimalizia tueleze nini tutarajie kutoka kwako mwaka huu?

Mtarajie EP ya pili ambayo natarajia itatoka kati ya mwezi Juni au Julai.  Jina la EP nitalizuia kwa sasa. Baada ya hapo huenda nikachukua mapumziko kidogo kimziki nipumue hadi Januari 2026 ambapo nita waangushie Rap Up 2025, hahaha.

Shukran sana kwa mda wako 'Uncle Murda' wa Mombasani! Hapa Bars Tu mwanangu!

Shukran sana mimi ni Uncle Murda wa 254, wa Pwani na Mombasa pia! [Hapa Bars 2]!

Mcheki Careem kwenye mitandao ya kijamii kupitia;

Facebook: careemke
Instagram: careem__ke
Twitter: @careemke