Peace and Much Love Family

Leo ni Tarehe 8 Nov 2021 (Ndio tarehe makala haya yaliandikwa na kuchapishwa kwanza) . Kwa wale wanaofahamu na wasiofahamu mwezi wa November ni mwezi maalum kufundishana juu ya Historia ya Hip Hop. Mwezi November unajulikana kama Hip Hop History Month.

Am your philosopher I will guide you through that. Ntaandika maandishi kadhaa na pia ntafanya The Gego Show kuelezea History of Hip Hop.

Tuanze kwanza, kwa nini November iwe Hip Hop History Month? Well, ni Elimu ya kawaida sana kwa wanajamii wa Hip Hop ya kwamba Historia ya Dunia Sio Historia ya kuaminika sana sababu Historia hiyo inaandikwa na mwenye nguvu dhidi ya wasio na nguvu.

Kwa kulifahamu hilo wana Hip Hop walitaka wao wenyewe wawe ndio wanaoelezea Historia yao na ili kufanikisha hilo walifanya kitu kinaitwa Meeting of the Mind hapo 1994.

Lakini hata kabla ya kukutana kwenye hiyo Meeting of the Mind, kundi maarufu kwenye Utamaduni wa Hip Hop lijulikanalo kama Zulu Nation walikuwa na tabia ya kukutana na kupanga mambo kadhaa juu ya Utamaduni wa Hip Hop ikiwemo kupangilia kitaaluma unachokifahamu leo kama Principles na Elements of Hip Hop Kulture.

Hivyo basi Zulu Nation kila November walikuwa wakikutana, na wao mpaka leo wanasherehekea Hip Hop mwezi November.

Hivyo 2001 wakati tunaenda United Nation kwa ajili ya kuitambulisha Hip Hop kama International Kulture of Peace and Prosperity ilikuwa ni muhimu kuweka siku kadhaa ambazo Utamaduni wa Hip Hop unaziona kama ni muhimu na unahitaji dunia izitambue.

Hivyo wiki ya tatu ya May ikawekwa kama Rap Music Day na hii ilitokana na marehemu Andre O’Neal Harrell kuanzisha process ya Proclamation ya hiyo siku kwenye mji wa New York. Hivyo Rap Music Day ikawekwa kuwa 3rd week in May.

Wana Historia wengi wa Hip Hop na muanzilishi wa Hip Hop Kool Herc wanasema kwamba 11 Aug 1973 ndio Party ambayo ndio imekuja kuwa Hip Hop ilifanywa hivyo siku hiyo inatambulika kama Hip Hop celebration Day na mwezi wote wa 8 ni Hip Hop celebration Month.

Mpaka hapo bado mwezi November haukuwekwa na hivyo kwa sababu Zulu Nation huo mwezi kwao ni muhimu maana yake ni mwezi muhimu kwa Hip Hop pia na ndio ukawa mwezi wa kufundishana juu ya Historia ya Hip Hop.

Kutokana na hizo precedence ndio maana tarehe hizo utazikuta kwenye Hip Hop Declaration Of Peace ya United Nation na pia tarehe hizo utazikuta kwenye bunge la Senate kama Senate Resolution 335 of 2021 ambapo nchi nzima ya Marekani kwa sasa inatambua Hip Hop na sherehe hizi za Hip Hop kisheria.

Hivyo kuna siku maalum kusherehekea muziki wa Rap maarufu kama Rap Music Day hii ni kila wiki ya tatu ya mwezi May.

Kisha kuna 11 Aug kila mwaka hii siku ni Hip Hop Celebration Day na pia mwezi mzima wa August ni Hip Hop Celebration Month.

Na mwisho kuna Hip Hop History Month ambayo ni kila mwezi Novemba tunautumia mwezi huu kuelezea watu, matukio na maeneo yaani  People, Places and Things ambayo kwa ujumla wake ni muhimu kwenye Utamaduni wa Hip Hop.

Hivyo kaa tayari sasa ili uweze kuongeza uelewa wako juu ya Hip Hop kuanzia 1973-2021 ukiwa na mimi;

Peace,
Gego Master,
Hip Hop Philosopher, Scientist Emcee
G.E.G.O Master,
Tel: +255764293025
Instagram: mekillergego

To be Cont...!