Nyimbo: Jua
Msanii: Fikrah Teule ft. Kaa La Moto & Viquee Ofala-Jua
Album: Azania Na Wanawe
Producer: Teknixx
Mchanganya sauti na vyombo: HR The Messenger
Tarehe iliyo toka: 31.10.2020

Alale pema Mugabe,msalimia Lucky Dube/
Natokea pwani sema alipo lala bi Kidude/
Historia, hata wakirudia hapa ndo kwetu/
Namjua Makeda, Malkia, sijui lolote kuhusu Yesu/
Fungeni macho tuombeni, shamba zenu niachieni/
Tumerudi utumwani, bila mafimbo, macheni/
Wakisoma madeni mwivi anatuletea msaada/
Wakati wakiiba faida zimebaki kwenye msalaba/
Mweusi kama Kaa, rangi hazibadiliki kamwe/
Peace kwa Wangari, walo kata miti walileta ukame/
Mame haha ndo hehu na uwia kaya/
Zile sauti za ndege, sauti za miamba zilitu inspire/
Walio pigania uhuru si ilikua ni uhuru wao/
Kumuondoa mzungu ili unitawale wewe na wanao/
Shamba Swaleh Nguru, mzawa naishi ki squatter/
Hizi ushuru mnazo ukoto, si mpatie wanao sota/
Nasubiri Jua lichomoze ni wafungue walio zizini/
Nipoteze uafrika kisa nimefungwa kifungo cha dini/
Dawa ya ukabila ubaguzi/
Endelea kuzini na racists ama kabila zingeni unizae mimi/
Ile nyumba nilio vunjia nayo ungo ndio si rudii/
The region of man is Africa, au bado hamniskii/
Watu wangu wa Maasaai, si walishi na nyama waka furahi/
Sawa na the garden of Eden kama Adam yupo Shungwaya/
Nicheke ama nilie zote zinabaki kelele/
Hizi michele, vipele, zinaletwa na watu wa mbele/
Ilimradi tu mpuguzwe, na dawa tu muuguzwe,
Na hawa ma super powers wanao tugawa ili tuburuzwe/
Nimekufia Sankara shuka la Kwame Nkurumah/
Nipe ala, nipige Kayamba pepo Mduruma/
Walize Vuvuzela, Sauzi ifike hadi Rufiji/
Waondoke na miji waende kijiji wamsalimie bibi/
Tujiandae, tusisahau kucheza Kirumbizi/
Hii future baadae inaeza fikia tukawa wakimbizi/
Kuku mlinde mwanae, kuna Kipanga na Mwewe/
Afrika kuungana, mabadiliko huanza na wewe,
Ona…/