Uchambuzi wa album: Wazalendo Raia
Msanii: Fikrah Teule
Tarehe iliyotoka: 05.07.2021
Midundo: Musa Kiama (MK) HR The Messenger, Jot Kosmos, Grandmaster Teknixx, Sango
Mtayarishaji Mtendaji: Fikrah Teule
Mixing & Mastering: PMG
Studio: Philosophy Records, B Records

Fikrah Teule

Fikrah Teule ni emcee ambaye yuko busy sana. Mwaka jana aliachia mradi wake wa pili Azania Na Wanawe ambao ulipokelewa vyema na mashabiki wake. Mwaka huu emcee huyu alijitosa studio tena na matokeo yake ni mradi wake wa tatu kwa jina Wazalendo Raia.

Wazalendo Raia ni mradi ambao umejaribu kubaki katika zile formula zilizoleta mafanikio kwenye mradi wake Azania Na Wanawe; mashairi na uchanaji mzuri, midundo mizuri pamoja na ma emcee waalikwa wa hadhi flani ki ubunifu na ki utunzi.

Mradi huu  ulikua na ma emcee waalikwa toka Kenya kama vile Young Njita, Assum Garvey, Kayvo Kforce, Musa Kiama(ambae ni producer hapa pia), Monski, HR The Messenger(producer), Van Jan na wengi pamoja na muimbaji Viquee ambae ashafanya kazi na Fikrah Teule kwenye miradi kadhaa hapo awali. Pia kwenye mradi huu Fikrah alipata fursa ya kufanya kazi na Azma (Tanzania) kwenye wimbo Namakinika, Nash Mc (Tanzania) kwenye Tubadilike pamoja na Black Psalmist(South Africa) kwenye Same Language.

Mradi huu ambao baada ya utangulizi mzuri ki acapella uitwao Tutazidi Kupanda unabadili hadi gear ya pili kwenye wimbo wa pili ambao una magwiji wa uchanaji kama Kayvo Kforce, Azma na Assum Mponda kwenye wimbo ulioundwa vizuri na Grandmaster Teknixx, Namakinika. Fikrah anatema wa kwanza kwenye mdundo huu akisema,

“Big baller my circle got smaller kama full stop chini ya exclamation mark/
Niki try ku connect dots in the dark/
Black out kanipa hope light itacome/
My people come first/
Closely na love ya fam utafunga maskio ulipigia mbuzi guitar/
Kayamba na shakers hubiria mitaa/
Same shit ilifanya nika go to gospel/
But then my head turned back nikarudi tena/
My voice switched to tenor/
Legend ka Shakes Makena/
Must be a rebel ama TD Jakes tena/
Wape samaki na mkate wa kila siku/
Sema nao hata Kama hawakuskizii bila kitu/
Tupige dua mwenyezi ata take care/
Tukiaminia sayari mema itatuletea/
Vyote mnavotupa twaweza share/
Mezeshea mwanzo wangu wa usemi utakapomalizika/
Kama si haki na usawa ni kipi tunachopigania/
Maskani ya Altari! injili ya Hip-Hop/
Nawatuma now Go tell em you don't stop!!!/”

Mradi huu umejaa ubunifu sana ki mashairi toka kwa Teule na ki midundo toka kwa ma producer husika kwao, big up kwa wote. Nyimbo zilizosimama na nilizo zipenda ni kama Nikitizama Nje ambao mdundo wake ulinikumbusha Toy Soldiers wa Eminem , Same Language ambapo Black Psalmist toka Sauzi anatema kwa ki Xhosa pia kuonesha kuwa sote ni watu tunaoongea lugha moja kwenye Same Language.

Nyimbo nyingine ambazo nilizependa ni kama Hewa, Alfajiri akiwa na Musa Kiama, pamoja na wimbo mzuka sana Madini Yetu, Dini Yao akiwa na K Lama na Young Njita kwenye mdundo mzuka sana ambao unaskia violin inapiga safi sana. Nash, pamoja na Azma, Assum Garvey pamoja na Kayvo Kforce wanashirikiana kutukumbushia kuwa Tubadilike Ikibidi.

HR The Messenger anabariki mradi huu na mdundo mmoja mzuka sana kwenye wimbo unao tuhamasisha kuhusu utafutaji wa mkate wetu wa kila siku kwenye All Day akiwa na the Ill Dada Monski. Kwenye wimbo huu Fikrah Teule anatema mistari mzuka sana ambapo anatukumbusha kuhusu gwiji wa mpira marehemu Joe Kadenge akisema,

“Uta rap na skills in circles but tuna ku kill with simplicity/
Sako kwa bako sisi tukiangusha bars huku sin city/
Nimeshapata part yangu tusiongee mengi/
To hell opinions hazinijengi/
Maoni genuine naskiza/
Chuki haijawahi niumiza/
Nayo simu haitulii utadhani mi nabii/
Nimewaacha so far siezi geuka kuwaangalia/
Matawi ya juu Twiga pekee hufikia/
Tume come na Joe Kadenge flow/
Check score say no more/
Sina rende wala back up aminia solo/
They still got my back wana ni follow/”

Wazalendo Raia ni wimbo uliobeba jina la mradi huu ni wimbo ambao unamkuta da’ Viquee akiimba kiitikio kwa hisia zote akihamasisha uzalendo kwa nchi tunazotoka ambayo ndio mada kuu ya mradi huu. Tujithamini na tuthamini vya kwetu. Kama wewe ni mzalendo basi mradi huu Mzalendo Raia ni wako.

Kupata nakala yako ya mradi huu Wazalendo Raia wasiliana na Fikrah Teule kupitia

WhatsApp: +254720674886
Facebook: Fikrah Teule
Instagram: eugeneorangi