Nilikua mtumiaji wa vilevi kama pombe, bangi na mara kadhaa sigara kwa muda mrefu kwenye huu ujana wangu. Jinsi nilianza ilikua ni curiosity na makundi rika ambayo niliwahi kuwa nayo au kujihusisha nayo. Mara nyingi niliwaza ni jinsi gani nitaweza kuacha lakini nilishindwa kwa sababu nilikua bado siko tayari kuacha matumizi. Uhalisia ulivyo ni kwamba jinsi unavyoanza ni tofauti na itakavyokua kwenye kuacha maana uraibu wowote ule ni rahisi kuanza na ngumu kuacha.

Anyways tuendelee, nilianza kuvuta mpepe nikiwa na marehemu kaka yangu, alikua ni mtu wa kwanza kunipasia mmea nami nikaujaribu na kuupenda kisha nikanogewa nikawa mtumiaji kuliko yeye. Miaka imeenda nikiwa mtumiaji wa siri bila wazazi au ndugu kujua. Nakumbuka wakati nipo A Level ilikua ni ngumu mtu kuweza kujua kama natumia kwa sababu nilikua situmii mara kwa mara hivyo sikua na mabadiliko yoyote kwenye mwili wangu.

Fast forward chuo, huku ndipo mambo yalipopamba moto. Maisha ya uhuru yakachochea matumizi na kunifanya pia kuwa mtumiaji mzuri wa pombe japo haikua mara kwa mara. Nilipokua nikirudi likizo home marehemu baba alikua ananishtukia mara kadhaa na kusema mimi ni mvutaji lakini nilikataa. Maisha yaliendelea, nikawa naenda chuo tukifunga narudi. Ule uhuru asikwambie mtu unalevya, ni kipindi hiki ambacho nilikua chronic user na kusababisha hata personality yangu kubadilika.

Wengi walionifahamu walishangaa na kujiuliza kwanini nimekonda/kupururuka. Nilijua sababu lakini wao wasingeweza kuelewa kabisa. Wengi akiwemo mama walijua ni masomo tu kumbe mashada. Kwanini sababu ilikua mashada? Mashada bwana yana tabia ya kuwa appetizer kwa hiyo ukivuta halafu ukawa huli na kunywa maji utakiona cha moto. Ukitumia halafu ukala vizuri utanawiri pia. Huo ndio ukweli, basi kutokana na hali niliyokua nayo nilikua na uwezo wa kupata mashada halafu menu usipate/usizingatie. Lilikua ni kosa kubwa sana.

Matumizi ya pombe kali haswa mwaka wa mwisho chuo nayo yalinifanya nikadhoofika sana mwili. Nakumbuka ilitakiwa nimalize masomo yangu ya chuo 2018 lakini kutokana na mambo kuwa magumu nyumbani ikabidi nije kumalizia 2019. Huo mwaka ambao nilikua nasubiri kuja kumalizia semester yangu moja iliyokua imebaki, ulikua ni mwaka wa miwako ule. Nashukuru nilijitahidi kuwa bora kwenye baadhi ya vitu navyofanya kama mziki na kujifunza mambo mbalimbali. Miwako ikaendelea kama kawaida, maskani na maghetto tofauti tofauti. Nilitamani sana kuachana na maisha yale.

Lakini bado muda ulikua haujafika maana nakumbuka mara kadhaa nili declare kuacha kuwa mtumiaji lakini nilijikuta baada ya wik nimerudi kundini. Ikawa kawaida, unaenda unarudi unaenda unarudi. Muda haukua muafaka. Moja ya vitu vilinifanya nishindwe kuacha ilikua ni circle niliyokua nayo maana usitegemee utakua Simba kama bado uko na Swala. Kiukweli na ukweli kutoka moyoni uraibu wa vitu tajwa huko juu una athari mbalimbali zikiwemo,

Kubadilika kwa personality ya mtu

Kudhoofika kwa mwili

Kushindwa kufanya majukumu au mambo kwa ustadi.

Kuchukulia vitu poa

Kuskilizia sana

Jeuri

Kukataa uhalisia na kujifariji

Kuamini ndivyo kumbe sivyo

Na athari nyingine chungu nzima. Lengo la uzi sio hilo, ni kuonyesha jinsi gani niliweza kuacha.

Jordan "Fivara" Wilson

To cut the story short, baada ya struggle za kuacha na kurudi kuacha na kurudi. Mwaka 2020 tarehe 4 February siku ambayo baba mzazi alifariki, tulikua tunawaka na wana. Yale maumivu nilijitahidi kuyapoteza kwa miwako lakini haikuwezekana. Msiba ulinikuta nikiwa Dar baada ya kuwa nimemaliza chuo 2019. Hapo nilikua naskilizia harakati za kuajiriwa au kujiajiri ila ATM ilikua ni miwako tu. Nikajipanga kwa safari siku hiyo hiyo, nikakata tiketi ya kurudi Mwanza kwa ajili ya mazishi.

Niliondoka asubuhi ya tarehe 5 ambayo ni siku yangu ya mwisho mi kuvuta mpepe, nilikula joint moja asubuhi sana na hata sikumaliza. Safari ikaanza mpaka Mwanza tukawa tumeingia usiku sana, nikapitiliza hadi home. Kufika home tukaendelea na taratibu za msiba na maziko.

Nakumbuka mzee alifariki Jumamne, Jumatano nikasafiri na kufika usiku sana ikiwa tayari ni Alhamis, nikashinda hiyo siku yote na tukazika Ijumaa. Wakati nipo safarini kuja Mwanza nilikua nawaza na kufikiria mambo mengi sana kichwani. Moja ya vitu niliwaza ni kukatia (kuacha) matumizi ya weed na pombe.

Mpaka nafika nilikua nishaamua moyoni kwamba naacha masuala, kweli tukamaliza maziko na vikao vya kifamilia. Hizo siku zote toka tarehe 5 nikawa sijachoma and I was getting along kwakweli. Mwanzo ilikua ni ngumu kwa sababu ukiwa umeshazoea au umekua mraibu haswa wa mashada, kula bila kuchoma ni kazi kweli kweli ila niliweza.

Ikapita siku, ikapita week, ukapita mwezi mpaka ukafika mwaka nikiwa clean. Thank God kwa hii safari. Sasa twende kwenye kiini cha hii story,

  1. Ili ufanye/uache jambo lazima ujue kwanini ili upate jinsi gani. To do/abstain from something you must have a “Why” to get a “How To”. Mimi sababu za kuacha tayari nilikua nazo maana nilishajaribu mara kadhaa na nikashindwa ila round hii nilijizatiti na nikaweza.

Sababu zenyewe ni hizi,

  1. Niliacha kwa ajili ya afya yangu na future yangu.
  2. Niliacha kwa ajili ya familia yangu haswa wadogo zangu maana ilibidi niwe mfano kwao.
  3. Niliacha kwa ajili ya mama yangu. Sikupenda nimrudishe katika madhila aliyopitia ye na marehemu baba, maana alihangaika nae kwa miaka mingi kuhusu suala la ulevi.
  4. I had to break the generational curse. Kwanini? Ukoo wetu wanaume ni walevi na imekua ni moja ya sababu ya umaskini.
  5. Kuondoa personality ya uhuni niliyokua nimeipata. I think I’m better than that, mambo ya kutokea tu na mtu kujua unakula kitu sio nzuri kimichongo.
  6. Unahitaji nguvu/sababu kubwa kuacha jambo flani ambalo sio zuri. Tabia hujenga mazoea Hivyo kuweza kuacha mazoea uliyoanza unahitaji nguvu kubwa kutoka ndani kwako na nje kwako. Inabidi uamue kwanza wewe na kisha upate influence kutoka nje kuweza kuacha mazoea uliyojijengea.
  7. Maamuzi yanaanza na wewe mwenyewe. Binafsi niliamua bila kushawishiwa na mtu yoyote.
  8. Don’t be selfish. Kuna muda tunafanya mambo kwa kujiwaza sisi tu, hivyo ni vyema kuwawazia watu wengine haswa wa karibu yako kama familia nk.
  9. Sio lazima kufanya kama wanavyofanya watu wengi. Baada ya kuwa nimeacha kuna wana wanashangaa imewezekanaje na wengine kunikejeli. Kikubwa nachojua kila mtu ana safari yake na maisha yake kwa hiyo sio lazima tufanane. Nakumbuka kuna siku nilikua na washkaji wakawa wanazungusha tu, siku hiyo nilikunywa soda tatu kwenda nao sawa. Walinidiss sana pale mezani lakini nikaona fresh tu sio kesi.
  10. Badilisha circle yako. Moja ya vitu vilivyofanya iwe rahisi kwangu kukatia mazaga ni kuwa na circle tofauti na ile niliyokua nayo. Baada ya msiba wa mzee nilikaa sana home na nikapiga online course ya Digital Marketing pia nikakomaa sana mziki wangu kwa hiyo nikawa adimu maskani na kwa wana. Pia wanangu ambao nilikua najiachia nao sana nilikua nishawaacha DSM kwa hiyo ikawa rahisi.
  11. Kuwa wewe. Fanya mambo kwa maamuzi yako, matakwa yako na motisha yako mwenyewe. Kitu ukiona ni kizuri endelea nacho na ukiona ni kibaya acha. Usijali utaonekanaje. Kwenye kitabu cha Atomic Habits kilichoandikwa na James Clear, anasema tabia huwa ina hatua nne nazo ni
  • Cue (Ishara)
  • Craving (Hamu)
  • Response (Majibu)
  • Reward (Zawadi)

Kwa hiyo ili tabia ianze au ikamilike inapitia hizo hatua hapo juu. Sasa basi ili kuacha pia tabia inahitajika kufanya kinyume na hizo hatua hapo mfano,

Ishara: unataka kuacha kuvuta fegi usihisi harufu yake wala kuiwazia yaani usipate ishara yoyote itakayokufanya ukatumie.

Hamu: umepata ishara ya kitu flani basi jitahidi usipate hamu mfano unataka kuacha kula kiepe inahitajika kufanya kinyume na hizo hatua hapo mfano, umeskia harufu usipate hamu.

Majibu: umepata ishara na hamu basi usichukue hatua kuijibu ishara/hamu uliyopata mfano umeona video ya ngono (pornography) ukapata hamu ya mapenzi usiende kufanya ngono au kupiga punyeto.

Zawadi: jitahidi uone tabia uliyofanya haina faida mfano umekunywa pombe utoe mawazo lakini ukaona hayajatoka na ukaamua kuiacha.

Kuzifuata hizo hatua nne kunasababisha tabia ikue na kutokuzifuata kuanasababisha uiache tabia flani. Kuwa mbali na hizo hatua nne kama James Clear anavyosema kwenye kitabu chake kwamba

Cue/Ishara: make it invisible/Ifanye isionekane

Craving/Hamu: make it unattractive/Ifanye isivutie

Response/Majibu: make it difficult/Ifanye iwe ngumu

Reward/Zawadi: make it unsatisfying/Ifanye ionekane hairidhishi

Nimalizie kwa kusema naendelea vizuri na safari hii japo changamoto ni nyingi ila nakaza. Nipende kusema lengo sio kukufanya uache au uanze vitu nilivyoacha lakini lengo lilikua ni kushare experience yangu ndogo niliyo nayo. Kama nitamkwaza mtu anisamehe na nitakaemfurahisha anipongeze. Sio kwa ubaya hata, nimeshare story yangu tu.

Wenu mtiifu katika kulipa Tozo, Jordan “Fivara” Wilson. Ahsanteni.

Wasiliana na Fivara kupitia;

Facebook: Fivara
Twitter: Fivara_
Instagram: Fivara