Toka kwa: Fivara
Wimbo: Zao
EP: Fikra Ni Vazi La Rap
Tarehe iliyo toka: 25.09.2017
Mtayarishaji: Prof. Ludigo na 9th Baba
Studio: Touch Music

Beti ya kwanza

Zao la Prof. Jay, zao la Mr. II/
Zao la Kwanza Unit, kwa kifupi KU/
Nadata kwa ushairi sio mapozi ka’ Bluu/
Zao la Chindo man kutoka Kijenge juu/
Zao la J.C.B acha nilenge tu/
Ukiskia Pah! Imekukosa panda taxi twenzetu/
Zao la Fid Q, zao la Dandu/
Sina makosa, unauaa gemu ndio masomo yangu/
Zao la Hasheem Dogo, zao la Kikosi/
Sao la Salu uandishi nilionao mikosi/
Usiulize zao la nani? Hili zao la Rado/
Chem chem ya maarifa sio mitambao ya chabo/
Zao la Zay B ona sasa nipo gado/
Zao la Nature na vina ka' msitu vipo bado/
Zao la Sister P, zao la Rah P/
Kazi ya Mola haina makosa, mi sio zao la Madee/

Beti ya pili

Usilete za kuleta, hili zao la Dudu Baya/
Kitaani Most wanted kisa nahusudu kaya/
Nageuka zao la Vinega, siwezi abudu hawa/
Kuipigania haki, hawawezi kutugawa/
Zao la Imam Abbas na mitaa ya kati/
Inatuokoa sanaa, sina mizaha na kazi (yes)/
Zao la Adili Chapakazi/
Staki mambo ya kuwa busy huku sijapata kazi/
Zao la Mangwair East Zoo/
Ku'switch ni easy, usidhani style ni hizi tu/
Zao la A.Y, commercial nakidhi tu/
Zao la Nako pia la Binamu, usidhani na'bang machizi tu/
Zao la Saigon, Sinza Oi Oi/
Kibongo, kinyamwenga kipi utanishinda goi goi?/
Mtetezi wa wanyonge, zao la Langa/
Fikra chanya na nzito tofauti na zao la pamba/