Ahmed Allly Upete alifariki dunia Novemba 11 2014.

Taarifa za kifo chake zilianza kusambaa mapema tu kwenye mida ya Saa 3 Usiku ikathibitishwa na kuanzia mida hiyo kikawa kiza kinene.

Miaka 7 na Ushee leo bila uwepo wa Ahmed,

Pindi Ahmed anajihuisha na kujipa uhai kwenye fasihi akawa zaidi ya mtu; akawa tungo, akawa jumbe, akawa punch na michano na kiufupi sasa akawa Geez Mabovu.

Kwa miaka kadhaa akaishi Upande Ahmed Ally Upete upande Geez Mabovu.

Nov 11, 2014 Ahmed Ally Upete akasimama na tukabaki na pande moja tu ya Geez Mabovu mpaka leo. Geez ameendelea kuishi na ataishi milele na milele ndani ushairi wake

Mwaka jana 2021 albamu ya Geez Mabovu iliingia kwa mtaa, albamu hiyo inayokwenda kwa jina la Mbwa Mchafu Wa Kusini  imetoka kwa ushirikiano wa Studio ya FishCrubMusic na BongoRecords.

Albamu hiyo ni uthibitisho kuwa fasihi inadumu kwa vizazi na vizazi na humo ndimo uhai wa Geez utadumu daima.

Geez Mabovu (R.I.P)

Taarifa:

Geez Mabovu

Albamu: Mbwa Mchafu wa kusini.

Track Listing:

  1. Nilikotoka ft. Joh Makini
  2. Dakika 0 ft Ngwair
  3. Mtoto Wa Kiume
  4. Party Ya Wajanja ft Squeezer
  5. Chausiku ft. Daz Baba
  6. Party ft. AY, Kabarani & Prof Jay
  7. Ugali Dagaa ft. Enika & Mansu Lee
  8. Haters ft. Joh. Makini
  9. Queen Of My Heart
  10. Easy ft. Dully Sykes
  11. Party Flani ft. Ngwair

R.I.P Ahmed,

ISHI MILELE GEEZ MABOVU.

Makala yameandikwa na Iddy Mwanaharamu.