Wimbo: Wanyama (Ni Life Tu)
Toka kwa: Black Ninja ft. Ghetto Ambassador
Mradi: Ilolo Confirmed 2
Tarehe iliyotoka: 15.04.2023
Mtayarishaji Mixing & Mastering: Black Ninja
Studio: Boom Bap Clinic

Ghetto Ambassador

Beti Ya Kwanza

Wanakula wanasex, si unajua human nature/
Ila wanyama,kiroboto anayewasumbua Juma Nature/
Kuzidi Wadudu Wa Dampo,kama nzi chawa funza/
Ama wale watu pori wanaoishi ndani ya mbuga/
Yeah
Inachekesha kuna Spiderman na buibui/
Wanyama ndani ya mbuga wa aina mbali mbali hujui jui/
Zaiid hajulikani mnyama wa aina gani husui sui/
Kweli unyama unyamani uadui dui/
Sikia
Wawindaji wanawinda kwa machale/
wanamuhofia sana Platinum Simba wa Madale/
Harmonize Tembo yupo na Ibra mtoto wake…/
Mdudu Mbaya Mamba chunga usijepita chocho zake/
Yeah
Mbugani Young Lunya ni Mbuzi/
Ila Beberu ni Wakazi Wa Kanda Maalum kubwa ukumbuki/
Yeah Soggy Dog Hunter/
MB Dog, Dog hustler/
ChindoMan Umbwa Mzee, Spack Dawg dog gangster/

Kiitikio

Ni life tu na vibe tu...(scratch)
Ni life tu na vibe tu…za wanyama mbugani na wanyama nyumbani x2

Beti Ya Pili

King Kong kwenye hii mbuga Chid Benz/
Ila Nyegere Nikki Bbishi Baba Malcom/
Ndani mbuga since enzi/
Pingu na Deso Gollilar Killers/
Ila ndani ya mbuga Zizi ni Godizilla Zillax/
Yeah
Rayvanni Chui/
Mbugani mi ni nani hujui/
Mnyama nisiye na chanjo nitazame mabegani ndui/
Bonge la Nyau a.k.a Big Pussy/
Young D Paka Rapa Panya Road sijui ni Weusi/
Likokola Ndege Tausi/
Sikia anamvuto wa kuvutia kuanzia mkia wake unywele mpaka sauti/
Mbugani Kipepeo Mweusi Mwasiti/
Mzee Mbuzi Faridi/
Ila Country Boy ni kiongozi Wa mafisi/

Stamina Ndege Shorwebwezi/
Ila Samaki mwenye kiu ndani ya maji Songa hata perege tope hamwezi/
Mnyama T.I.D/
Anajifanya V.I.P/
Baada ya kufa Faru John mi ndo Mnyama B.I.G/

Kiitikio

Ni life tu na vibe tu…(scratch)
Ni life tu na vibe tu…za wanyama mbugani na wanyama nyumbani x2