Wimbo: Rudi Africa
Emcee: Ghost The Living
Mradi: Mask On presented by DM Music Laboratory
Tarehe iliyotoka: 28/03/2022
Mtayarishaji: Ventalon
Studio: Neptone Records

Ghost The Living

Beti Ya Kwanza

Iwe mliondoka kwa amani au mliondoka kwa Visa/
Wengine ni bila kutaka mliondoka kwa vita/
Hamjui muanzie wapi huku mkihaha kila siku/
Na mtarudi vipi wakati mliacha utawala wa ma chief/
Mliacha ardhi yenu je mkirudi mtaikuta? /
Na mlisha sikia mkirudi hamumkuti Lumumba/
Wala Nkwame Nkuruma wamelala mashujaa/
Na mtarudi vipi wakati wale wanawakataa/
Asili yenu mnaipenda shida ni mapokezi/
Mliko hamna raha kila kukicha ni uonezi/
Ubaguzi wa rangi mateso amani hakuna/
Kwenye huduma za afya ni mko mstari wa nyuma/
Na serikali ina chuna ina kausha inavunga/
Haina habari na askari wala rushwa wakuda/
Wanao ua black people bila hofu/
Wanao ibua uonezi chuki na hila mbovu/

Kiitikio

Rudini Nyumbani wewe Mwana wa Africa, Africa, Nyumbani kumenoga Rudi tudumishe Mila tutambike x 2/

Beti Ya Pili

Rudini mkifika msihofu tutajadili/
Tutawafundisha mambo mengi mpaka tiba za asili/
Mila na desturi najua mtaishika asili/
Maombi na dua zetu njooni mtafika wasafiri/
Kuhusu makazi kuna viwanja vya kutosha/
Mpaka nyumba zipo msije waza nakuogopa/
Rudini Africa yetu ndo kwanza imepamba moto/
Japo Mabeberu washamba wanatugawanya hovyo/
Hawataki umoja wetu wanaibua vikwazo na maradhi/
Wanatuzuga kiboya eti mipango na miradi Mipango na miradi?/
Wajinga wanaing'ang'nia Congo/
Na vita visivo isha wanatu kanyagia hovyo/
Ma soldier rudini kwanza tuungane kuwatawanya/
Nyumbani kumeisha noga tuungane kuwa changanya/
Africa bara la amani wasingekua hawa/
Rudini Nyumbani mpaka waje washindwe kutugawa/

Kiitikio

Rudini Nyumbani wewe Mwana wa Africa, Africa, Nyumbani kumenoga Rudi tudumishe Mila tutambike x 2/

Beti Ya Tatu

Fungua akili na hiyo tamaaa ya muda mfupi/
Asili ni asili Kwa wewe unae kataa kurudi/
Kuna faidaa gani kuteseka ugenini/
Unadhani bila kujitambua hivi tungeweza nini/
Halafu sio sisi mpaka Asia wana baguliwa/
Wamegundua baada ya hizi sautii kuamuliwa /
Nakupaza kuhusu Africa /
Hatuwazi umbali safari ni kuhusu kufika /
Kurudi sio kazi niaminini ni simple/
Vizazi vimezaliwa kuna uzawa wakina Steven Biko /
Msihofu Kila kitu kipo sawa/
Hakuna unyonge mihimili imara tambueni ipo power/
Hivi huko hamchoki kuitwa wakimbizi /
Mshawaza nini watoto mkifa urithi/
Ya nini kuishi kwa mashaka hamna uhakika wa ulinzi /
Mnapigika na viwanda hamna uhakika hamlipwi /

Kiitikio

Rudini Nyumbani wewe Mwana wa Africa, Africa, Nyumbani kumenoga Rudi tudumishe Mila tutambike x 2/