High Smoke

Producer High Smoke Beats ni mtayarishaji anaetokea kule Arusha, Tanzania. Jamaa huyu walishirikiana freshi sana na JCB na wakatu bariki na kazi moja murwa sana ilioonesha vile kila mmoja wao ni Fundi Mitambo, JCB kwenye kinasa ilhali High Smoke Beats kwenye midundo.

Dunda nasi tukiingia studio za mwana ili tupige gumzo kuhusu moshi unaotoka studio kwani dalili hii inaonesha ndani kuna moto…

Karibu sana kaka High Smoke Beats hapa Micshariki Africa. Kwanza kabisa tuanze kwa kukufahamu jina lako rasmi, unatokea wapi na unajishughulisha na nini?

Shukran sana, naitwa Ally Muhsin, natokea Arusha na ni mtayarishaji wa muziki pamoja na mtaalam wa TEHAMA.

Tueleze historia yako, ulizaliwa wapi, ulisomea wapi na umefikia wapi kimasomo? Utoto wako ulikuaje wakati unakua?

Mimi nimezaliwa Arusha na nilisomea Arusha Primary School na kisha baadae kwenda Edmund Rice Secondary School. Baada ya hapa nilienda college ambapo nilisomea maswala ya I.T (TEHAMA).

Nashkuru, wazazi wangu walinipa malezi mazuri hivyo utoto wangu ulikua mzuri.

Tueleze historia yako ya muziki, uligunduaje kua una karama hii ya utayarishaji na umewezaje kukuza hiki kipaji hadi hapo ulipofikia kama mmoja wa watayarishaji wazuri kuwai kutokea A-Town, Arusha?

Nilianza muziki baada ya kumaliza chuo ingawa pia kipindi cha sekondari watu walikua wanajua napiga beat ila kurekodi ilikua bado.

Motisha ilikuja zaidi baada ya kuwafata ma bro Watengwa, ChindoMan akiwa anafanya kazi na kuangalia tu, Wa Knowledge kua naye akiwa studio studio pamoja na bro Sam Feeez wa Majeruhi. Kufikia nilipo fika ni kuwa na nia zaidi, hiki ni kitu kipo ndani yangu so it can’t die.

High Smoke Beats, jina lilikujaje na linamaanisha nini?

High Smoke Beats ilitokea nikiwa na mwana tulianzisha crew 182 ilikua inaitwa, so tuka jiuliza je majina yetu inakuaje ye akawa Non Stop na mimi High Smoke. Maana ya High Smoke ni endless energy iko hapo in air in the sky, kila vibe ninayo has to be high.

High Smoke Beats niliona sehemu flani pia una talanta zingine kando na utayarishaji...

Talents; mi pia ni artist, naweza kuigiza, naweza kua host presenter

We pia ni music writer na wakati mwingine ghostwriter. Kwa aina zingine za muziki mie naona kuandikiwa wimbo sawa ila kwa wachanji naona kama mchanaji huyu atakua na walakini. Wewe unazungumziaje swala la ghostwriting kwenye Hip Hop na umeshawaandikia wachanji gani ngoma zao?

Ghost writers wapo na ni kitu kipo na watu wanao andikiwa siwezi sema ni walakini kwangu naona ni  swala la uwezo. Kwa mfano kuna mtu ni mkali wa freestyle but hawezi andika verse ya kueleweka, nafikiri umenisoma, kila mtu anajua talanta yake na limits zake.

Tueleze kuhusu ushirikiano wako na Vichwa Vya Habari upoje?

Vcw tunajuana mda, kipindi nina home studio yangu OVAR KODZ. Link ilianzia hapo. Jeremy ni mtu poa sana anajua ku deal na artists and we need more people like him. He is our Ruge.

Fundi Mitambo ya JCB Watengwa ndio mahala binafsi nilianza kukuskia vizuri kama mtayarishaji. Nieleze kuhusu historia yako na JCB, mlianzaje kufanya kazi na experience yako ilikuaje mlipokua mnaanda mradi wake Fundi Mitambo?

Connection kati yangu na JCB ilitokea wakati Jeremy alikua na artist wake anataka fanya kazi na JCB na mdundo ulitakiwa uwe wangu. Baada ya kazi kufanyika bro akaniambia amepata motivation ya kufanya album na mimi. Experience iko poa kufanya kazi na legend coz ni learning curve…

Fundi Mitambo ilikua ni project ilio pangika tukiwa na bro Chaca Kichacani, haikua tu album ya hivi hivi ila tulikua na mipango ya kuifanyia mauzo (sales plan), kulikua na siku ya kupiga beats tu, siku ya recording sessions na mixing n mastering days.

Pia umahiri wako nilizidi kuuona kwenye EP yako Spit EP ambayo ilikua na wachenguaji kama vile Kaa La Moto, Ibrah da Hustla, Chaca, JCB na D Maujanja. Maudhui ya mradii huu yalikua nini na mbona ukaamua kuachia EP yako kama mtayarishaji?

EPs ni mpango wa kutoa ngoma tofauti na albums ukiacha na zile single track nilizo achia ndo maana zinakua na mixture ya watu tofauti.

Wimbo wangu pendwa kwenye mradi huu Spit EP ni Masaai uliomshirikisha Dazzle. Nini kilicho ku inspire kuanda ule mdundo na kutumia sampuli zile za ki Maasai?

Maasai, Dazzle si unajua ukikaa kichakani  unapata vibe tofauti. Bro Chaca alikua na kazi na wa Hadzabe so si tukasema why not Maasai vibes kwa song ndo tuka fanya ile.

Kando na miradi tajwa hapo juu, umeshahusika kwenye kazi za wasanii gani iwe ni single, EP, Mixtapes au albums?

Miradi mingine ni kama mixtape ya The Mix moja ya kazi zang za mwanzo kutoka North Block EP ya All Day ya Pax Kweli, OS Studio EP ya Bad Girl ya Letishersk, OS Studio na EP ya Kila Day ilifanyika A Town Records.

Hali ya Hip Hop Arusha vipi maana inasemekana wana Chuga mpo resi sana kukumbatia mainstream Hip Hop, hili unalizungumziaje? Je Hip Hop ya handaki ipo hai na wachanaji gani tuwafautilie kwa ukaribu?

Main digital world kila mtu anapambania kwa style yake.  Artist wapo kama Slim Dawg, Niger P Dizzy, wote kutoka Mgeez Gang, kuna Chuga kutoka Toje Clan, Pax Kweli, Waladi Family Dey also coming good kuna Ollachuga.  Pia kuna Ramcy na Digala ao pia wako poa…

Kuna chochote tutarajie kutoka kwako mwaka huu 2023?

2023 ntaachia album mbili nyingine, moja ikiwa ni ya OS nyingine siwezi kuitaja kwa sasa.

High Smoke changamoto unazokumbana nazo kwenye mbanga za utayarishaji ni zipi na unakabiliana nazo kwa njia ipi?

Changamoto ziko kila siku, mi naona ukiwa na mfumo mzuri wa kazi na uliopangika mambo yanaenda tofauti na hapo hayaendi. Kama Micshariki mko organized kazi zina songa maana kuna Ally na High Smoke wote wanahitaji kusonga na ndo mana napenda fanya kazi na  watu ambao wana mpangiio ya kazi.

Niliona siku hizi umekua mtangazaji wa habari/podcaster. Kipindi chako kinapatikana wapi na kina maudhui gani?

Kuhusu kipindi, ile ni kwa ajili ya taarifa za wasanii kuweza kujulikana, kujieleze na zaidi na wao kutoa insights zao na pia nataka kuja na kingine kitacho itwa The Process.

Pia nieleze kuhusu Ololoo Media mnajihusisha na nini?

Ololoo media kuna studio, audio, matangazo ya kazi za audio zote, graphics, T-shirt printing. Pia kuna Silk Willy private lounge na OS shop phone accessories…

Kipi cha mwisho ambacho sijakuuliza ambacho ungependa kutuambia.

Mpango ulikwepo kuna swala linajadilwa na Wcw likikamilika utalitambua mkuu. Mengine zaidi nitakupa info mkuu…

Mawasiliano yako na anwani ya mitandao ya kijamii?

Simu: +255 711 78 33 82
Email: highsmokebeats@gmail.com
Instagram: highsmokebeats

Shukran sana kwa mda wako High Smoke Beats.

Shukran