HR The Messenger akiwa kazini

HR The Messenger ni mjumbe na kama waswahili walivyo nena, “Mjumbe hauawi”. HR ni mjumbe wa Hip Hop ambae madhabau yake ni kinasa, mashairi na midundo anayoyaunda mwenyewe ilhali waumini wake ni wana Hip Hop wanaoungwanishwa na upendo wa Hip Hop.

HR The Messenger ni mshindi wa matuzo matatu ya Unkut Hip Hop awards 2019 kule Kenya akifanikiwa kushidha matuzo ya Msanii Bora Wa Kiume, Msanii Chipukizi wa Mwaka pamoja na Kandamseto/Albam bora ya Mwaka.

Baadhi ya kazi za HR The Messenger:

Gwantana ft Scar Mkadinali - https://www.youtube.com/watch?v=lmRG8xWKs9A&t=71s
Daytox Intronix ft. HR The Messenger, Lord Arnold – Nayo Nayo - https://www.youtube.com/watch?v=jmnoJDxmla0
Waridi - HR The Messenger ft Markus Is Ill, X-ray King - https://www.youtube.com/watch?v=BkjYZqDxOmI
Lord Arnold - Levels - https://www.youtube.com/watch?v=vJUmKuoGzFg

Tulipata fursa yakuongea nae kwa njia ya WhatsApp na haya ndio mazungumzo yetu,

HR The Messenger ni nani,kazaliwa wapi na anatokea/kupatikana wapi?

HR ni msanii, mbunifu wa sanaa, mtayarishaji wa rekodi, mhandisi wa sauti na mjasiriamali. Nilizaliwa K South lilipotokea kundi la Hip Hop la K-South Flava (Bamboo na Abbas Kubbaf) kabla ya kuhamia Rongai ambapo nipo hadi leo.

Jina lako rasmi ni nani?

Rasmi naitwa Njuguna Kimemia.

Kwanini wajiita au waitwa HR The Messenger? Jina lilikujaje?

HR ni kifupi cha High Renaissance na kihistoria ni wakati ambapo sanaa kule nchini Italy ilikuwa imetawaliwa na magwiji wa sanaa kama vile Michelangelo, Raphael na Leonardo Da Vinci. Pia nilizaliwa June 16 kama vile Tupac Shakur na Femi Kuti

Na katika unajimu, sayari inayotawala ya Gemini ni Mercury na katika hadithi za Kigiriki na Kirumi Mercury alikuwa mjumbe wa miungu. Nikaamu kujiita High Renaissance The Messenger.

Wewe ni muunda Midundo(beat maker) tu au producer?

Mimi ni mtayarishaji kamili wa rekodi. Kutoka  utengenezaji midundo hadi  uandishi wa nyimbo na pia mix and mastering pamoja na kuongoza video.

Historia yako ki mziki ipoje?

Nilianzia mziki  kanisani kwa kupiga kinanda wakati wa ibada japokuwa toka awali nilikuwa mpenzi wa muziki wa Hip Hop.

Pia tulikuwa shule moja na Domani Munga wa Wakadinali na nilikuwa nampigia kinanda wakati alipokuwa akichana tukiwa shule ya upili. Baadaye nikaanza kughani nikiwa shule ya upili pia

Nilianza kujifunza kuwa producer rasmi nikiwa chuo kikuu na ndipo nilipojipatia jina langu la kisanii na kutoka hapo ni kazi kwa kwenda mbele!.

Ulianzaje shughuli ya u producer na ni kipi kilichokupatia motisha kubaki hapo?

Nilianza kwa kucheza kinanda kanisani kisha kuendelea kutengeneza midundo nikitumia softwares za midundo na kwa kupata elimu toka kwa ma producer wengine  hapa na pale pamoja na kujifunza mengine kwa njia ya YouTube hadi nikawa stadi.

Motisha ni kujisukuma mwenyewe tu na pia kushikilia maono na ndoto zangu bila kuziachilia iwe kunanyesha au jua linapiga.

Ukiangalia hawa ma producer waliopo kwenye game ya Hip Hop Kenya na duniani ni nini kilicho kufanya uamini utafanikiwa kama producer ?

Thubutu kuwa tofauti ndio kauli mbiu yangu! Pia naamini kuwa naleta mdundo wa kipekee toka kwangu wenye mtindo wa kipekee kwa hiyo lazma ntaskika tu.

Je unatengeneza aina gani ya miziki?

Kwa upande wa midundo mie nahusika kwa kuunda midundo kwa ajili ya miziki tofauti ila kwa upande wa usanii mie ni mwana  Hip Hop kindakindaki!

Ulishawahi kuwa na shaka kuwa utafanikiwa kwenye hili?

Once in while mambo huenda mrama ila kama nilivyosema hapo awali kikubwa ni kujiamini na kuhakikisha macho yako yapo kwa malengo yako kila kuitwapo leo. Usisahau maisha ni kama mbio za masafa marefu(marathon) na sio mbio za mita 100 au sprint.

Ni kipi kilicho kusukuma usiache fani hii ?

Nilipoanza kuona matunda ya kazi yangu pamoja na kuanza kupata wateja wengi, na mashabiki pia kunikubali na kukubali kazi zangu sanasana pale YouTube pamoja na kazi hii kuanza kuniingizia hela pamoja na upendo toka kwa mashabiki zangu.

Ilichukua muda gani hadi HR The Messenger aanze kusikika ?

2019 niliangusha mradi wangu albam yangu ya kwanza Reign ndo nikaanza kujulikana rasmi na wana Hip Hop.

We hupata vipi wateja wako?

Kwa kupitia mitandao ya kijamii pamoja na kazi yangu kuongea yenyewe.

Ungetoa ushauri gani kwa yoyote anayependa kufuata nyayo zako?

Weka kichwa chako juu na  kisha piga kazi! Piga kazi! Piga kazi na pia uwe na shughuli nyingine kando na mziki za kujiajiri zinazokuongezea kipato. Pia hakikisha hauweki mayai  yako yote kwenye kikapu kimoja.

Ushawahi kuwaza kutoka Kenya ili kujipatia kazi zaidi?

Kazi zangu zimeskika Malawi, Burundi, South Africa na kwa uchache kule Uingereza. Ni mdogo mdogo tu.

Umeshafanya kazi na ma emcee gani kwa miradi gani?

Nimefanya kazi na kundi la vijana wenye talanta kama vile Scar Mkadinali, Boutross, Silverstone Barz, SewerSyda Mkadinali, Trabolee, Lord Arnold, Cafu Da Truth, Bantu Slim, Fikra Teuleh miongoni mwa wengine Wengi.

Wee upo chini ya umiliki wa studio ya mtu au unamiliki studio zako mwenyewe?

Tukishirikiana na mwanangu Lord Arnold tumefanikisha kufungua studio yetu Philosophy Records pamoja na Frames Avenue na Intronix Media.

Je unaelezeaje mtindo wako wa kufanya kazi na msanii ?

Mradi msanii ana kitu ndani yake cha kipekee ambacho anaweza kuweka mezani na pia ni msikivu na anapenda kuskia  ushauri na maelekezo na pia ni mbunifu basi naweza fanya naye kazi.

Ni wimbo gani au mradi gani unaoupenda sana ambao uliufanyia kazi?

Kuna miradi  kadhaa kama albam ya Fikrah Teule Azania na Wanawe ambayo binafsi naipenda sana!Pia kuna mradi wa Lord Arnold, Antidote For The Soul.

Gharama zako kwa kazi hii ni kiasi gani?

Kama msanii anataka ku record wimbo kisha afanye mixing and mastering akiwa na mdundo wake hua nalipisha Kes 5,000.00 lakini nikikuundia mdundo na kufanya shughuli zote hadi wimbo wako ukamilike gharama hua Kes 8,000.00 tu!

Ila msanii akiunda albamu yote nasi basi anapewa discount ya asilimia kadhaa na vile vile tunaweza kuwa nae na mkataba au split sheets itakayoonesha jinsi gani twaweza kubaliana kiasilimia kazi hii tutagawanya vipi mapato.

Umekuwa ukiskiliza mziki wa aina hivi karibuni ?

Nimekuwa nikiskiza albam ya Liquid Flows na pia deluxe albam ya Asum Garvey.

Je ni jambo gani moja kila wimbo lazima uwe nalo ili uwe thabiti?

Producer tag/sign tune yangu ya, "HR pump hio track bana. Hehehe

Ni nani mtayarishaji bora wa muziki anayefanya kazi katika tasnia hii leo unayemkubali?

Kevin Provoke, Akili Blaq, So fresh , Dunga , Chizen Brain , Clue ashaivisha track , na wengine wengi!.

Nje ya muziki HR The Messenger hujishughulisha na nini?

Biashara za hapa na pale nikianza na biashara ya kuuza mishumaa yenye harufu nzuri pamoja na kujishughulisha na huduma za courier au usafirishaji wa mizigo  na pia kufanya biashara ya maduka.

Ni watayarishaji gani,waimbaji au wasaniii waliokupa motisha yako ya msingi?

Nampenda sana Russ toka USA , Priddy Ugly na A Reece toka South Africa,  Eric Elliot , Jake One na kadhalika.

Unazungumziaje game ya hip hop underground/handakini toka Kenya na Africa Mashariki?

Game limeanza kupata thamani ila bado tuna safari ndefu ya kwenda. Pia ishu za umoja kwenye kazi zetu ndio kitu kimoja ninachoona ni muhimu. Pia ni muhimu kuondoa vile vizuizi vinavyotaka kukwamisha maendeleo yetu.

Shrap au Boombap ?

Zote zina vaibu yake mi nazichana zote bila tatizo.

Je ni masomo gani muhimu ambayo umejifunza juu ya kutengeneza midundo ambayo ma producer pamoja na wasanii chipukizi wanaweza kujifunza?

Unatakiwa uwe na subra na mikakati kwa ajili ya shughuli zako. Pia fanya kazi kwa busara sio kwa kutumia nguvu. Jitahidi pia uwe na biashara za kando zitakazo kuwezesha kuongeza kipato chako pia na hakikisha hufanyi kazi kama mkwanja haujawekwa mezani!.

Ni nini cha mwisho unachoweza kutuambia ki ujumla ambacho sijakuuliza?

Hip hop ni culture ya love na ni culture ya bag pia usisahau.

Msanii apange mzuka wake akitambua kuwa game ni kubwa na kila mtu anaweza kula au pia  anaweza kosa ikitegemea vile anavyofanya shughuli zake.

Tutegemee nini toka kwa HR The Messenger hivi karibuni na baadae?

 Nina projects kibao kama vile visuals, singles na pia beat tape ambazo natarajia kuachia. Pia natarajia kuachia albam yangu ndani ya mwaka huu pamoja na Ep kadhaa na pia nina matumaini ya kufanya kazi na wasanii wengine.

Wasiliana na HR The Messenger kupitia mitandao ya kijamii:

Facebook: Njuguna HRenaissance Kimemia
Facebook: Philosophy recordz
Instagram: hr_the_messenger
YouTube: HR The Messenger