Uchambuzi wa EP: Nocturnals
Msanii: HR The Messenger & Sewersydaa Mkadinali
Tarehe iliyotoka: 16.06.2022
Nyimbo: 8 + Outro
Mtayarishaji, Mixing & Mastering: HR The Messenger
Studio: Philosophy Recordz, Zozanation

Nyimbo Nilizozipenda: Degree, Mind, Nayo Nayo, DOD, JYK, Haters, Reuters, Nike

Sewersydaa Mkadinali na HR The Messenger

Ni furaha kwa game la Hip Hop pale watu wenye vipaji vyao wanapoweza kufanya kazi pamoja ili kuweza kutupatia miradi mizuri. Sewersydaa Mkadinali ni mmoja ya washairi bora kuwahi kutokea Nairobi, Kenya (cheki Mixtape yake Jeshi Ya Katululu) ilhali HR The Messenger ni bora inapokuja kwa utayarishaji ila kama alivyowahi kusema hapo awali hata kwa kinasa yote freshi tu kama tulivyoona kwa LP yake classic Reign.

Wawili hawa wamefanikiwa kufanya kazi hapo awali iwe ni kwenye singles kama vile Mau Mau au kama mtayarishaji na emcee kwenye mradi wa Sewersydaa WADA –The Healing Of A Nation. Mwezi wa sita mwaka huu wawili hawa walizama studio pamoja na wakati huu wakatuletea mradi wao wa pamoja EP kwa jina Nocturnals.

Mradi huu ulitambulishwa rasmi kwa mashabiki na single ya kwanza Nayo Nayo. Ngoma hii ambayo naona ilikuwa kama muendelezo wa Nayo Nayo ambayo hapo awali walikuwa HR The Messenger na Lord Arnold pamoja na Danytox Intronix ni ngoma inayotuhamasisha kusaka wera ili tuweze pata senti za unga. Anakwambia Sewersydaa kuwa “Sionekani streets labda nikitembeza products” ilhali HR nae akikwambia “Ngware raukia meda kitu saa tano nishatinga hustle”… “Hatuiacha iende/Nayo Nayo….”

Hapo mwanzo mradi huu unafunguliwa rasmi na ngoma mzuka sana Degree ambapo ma emcee hawa wanaongelea hali halisi ya maisha ya vijana wengi nchini Kenya na pengine Africa ki ujumla ambapo watu wamepiga buku sana na kupata shahada ambayo wameshindwa kuitumia. Wimbo wa kusikitisha wa kukufanya ucheke na pia kukutia moyo kuwa wauza degree tupo wengi ilhali mdundo ni noma sana; vinanda wazimu sana. Checki mashairi ya HR The Messenger hapa noma sana.

Wimbo unaofuatia Mind ni wimbo unaokuonesha vile kila kitu maishani mwako kama vile kushinda au kushindwa vinaamuliwa akilini mwako. Sewersydaa kwenye wimbo huu anatema madini si haba akisisitiza kuwa kauli yako ndiyo inakupa unachopata au kama wanavyosema kwa kimombo your confession is your possession….

“Ukidhani we ni mgonjwa ndio utakua mgonjwa/
Nilisema sitasota hivyo ndio nikaomoka/”

Kwenye Haters mtayarishaji/emcee HR anachana akiwa pekee yake akiwakanyagia wabaya wake kwenye ngoma ya ubeti mmoja ilhali Sewersydaa anachana solo kwenye Nike na pia kwenye JKY ambao ni drill flani akisema amekuja ubaya kwa yeye ni Jeshi Ya Kuharibu.

Changamoto za madawa ya kulevya wanaziongelea kwenye DOD ambapo wawili hawa wanabadilishana kinasa kwenye gumzo flani kati ya teja na muuzaji wa midaharati (pusha) ambapo unaona vile wote wanataka kupiga biashara ila wote hawaaminiani hadi ma mwera wanakuja na dili linaharibika.

Reuters ni wimbo ambao unaendeleza ile mada ya Nayo Nayo ya utafutaji iwe ni usiku au mchana hadi waonekane kwa magazeti japokua bei ya maisha imepanda kushinda bei ya mafuta.

HR The Messenger na Sewersydaa Mkadinali waliamua kujifungia studio mchana na usiku ili kutupatia mradi wao wa kwanza wa pamoja na ushirikiano huu umewawezesha kutupatia mradi ambao unanuia kuonesha vile inabidi ukeshe ili kuweza kuhakikisha unafanikisha ndoto zako. Wawili hawa inapokuja kwa maswala ya utafutaji wanatuhimiza tuwe mabundi na mapopo, Nocturnals. Mradi chanya sana.”

Wafuate wawili hawa ili upate nakala yako ya EP hii kwa Tsh 20,000.00/Kes 1,00.00 pekee. Wacheki kupitia;

HR The Messenger

Facebook:Njuguna HRenaissance Kimemia
Instagram: hr_the_messenger
Twitter:Hi_Reinassance

Sewersydaa

Facebook: SewerSydaa Mkadinali (ManAdriller)
Instagram: sewersydaa
Twitter: sewersydaa