Toka kwa: Javan (Chuna Ngozi) ft. Adam Shule Kongwe
Wimbo: Lugha
Albam: Fasihi Simulizi
Tarehe iliyo toka: 2016
Mtayarishaji: Bin Laden
Studio: AJ Records

Beti ya kwanza – (Javan)

Habari Za Saa Hizi Jamani Wazima /
Naitwa Said Javan Kwa Majina/
Najivunia Mbuga Za Wanyama/
Uoto Wa Asilia ,Milima Mikubwa Sana/
Pia Na Lugha Mama Ya Kiswahili/
Naiwakilisha Ili,Afrika Duniani Na Pote Kishamiri/
Kama Ilivyo Pwani Ya Afrika Mashariki/
Wageni Majirani Mngefika Anga Hizi/
Kiswahili Ndiyo Sauti Makini/
Iliotoa Tofauti Za Kidini/
Na Ubaguzi Wa Kikabila Kati Ya Wewe Na Mimi/
Natulia Bwana Najifunza Kiswahili/
Nakitumia Sana Ninapotunga Mashairi/
Hata Mniamishe Dunia/
Kiswahili Lugha Yangu Mpaka Mnivishe Gunia/

Kiitikio -(Adam)

Nimefika Mataifa Mbalimbali/
Hesabu Kilomita Zisizo Na Idadi/
Mimi Ni Jasiri/
Siachi Asili/
Daima Sibadiliki Na Lugha Ni Kiswahili/
Nitakuenzi/
Sababu Mimi Na Wewe Ni Tangu Enzi/
Toka Jana Kesho Na Muda Huu/
Kiswahili Kiswahili Wewe Ndo Lugha Kuu/

Beti ya Pili -Javan,

Kiswahili Cha Mtaa/
Ama Fasaha/
Ninaweza Kutumia Kufikishia Hii Sanaa/
Nikisema Vichaa/
Simaanishi Wakosefu Wa Akili/
Ni Rejesta Na Misimu Na Huku Kwetu Ni Asili/
Kiswahili Mie Ni Wako/
Popote Niendapo/
Takutangaza Wakusikie/
Sifa Zako Wakusifie/
Kiswahili Cha Watu Na Watu Ndo Sie/
Hamasisha Askari,Vitani Waende/
Vumisha Habari Vitali Maembe/
Weka Mbwembwe/
Mistari Ipendwe/
Kiukweli Kiswahili Nakuhitaji/
Ndomaana Kwenye Sanaa Nakuhifadhi/
Watu Wa Mtaa Tunakutaka/
Unatufaa Tunakufuata/
Hata Mniamishe Dunia /
Kiswahili Lugha Yangu Mpaka Mnivishe Gunia/