Toka kwa: Jedikouga Mtawala (R.I.P)
Wimbo: Sauti ft Jadah MaKaNTa
Albam: HURU
Tarehe iliyo toka: 24/07/2017
Mtayarishaji: Aziz Midundo, Burnbob(R.I.P)
Studio: MaKaNTa JR Records

Beti ya kwanza:

Imeandikwa mwenye haki/
Ataishi kwa imani/
Na kweli dhati ruhusu nuru gizani/
Uhuru wenu ombeni/
Mkinisoma yakini/
Nini wasichobaini kupoteza kiini/
Elekeza tathimini/
Rudisha madini fungua kanuni/
Katiba mezani/
Ubepari ushetani, mwanasiasa jukwaani/
Hashikiki hasirani, keshatutosa zamani/
Kuwakosha wahisani/
Alishatabiri Saadani/
Sirikali kwenye mboni,sirikali ya maono/
Vipi punguwani, kwa dini zao mdomoni/
Wameleweshwa pomoni/
Wanatuteka kiimani/
Juu ya kibanzi jichoni/
Nasikiliza sauti za watu msururu/
Gizani shuruti wanaitaji nuru/

Beti ya pili:

Wape kondoo malisho mema/
Ikiwa bado mapema/
Ikiwa bado unahema/
Tema kwa hekima/
Kinachotoka kwenye kinywa/
Elewesha kwa unasaha/
Wape kweli ya ufasaha/
Bendera zinapepea kwa itikadi bandia/
Soma viashiria anguko la dunia/
Muadhini anaashiria/
Sali kabla haujasaliwa/
Naitazama Faruja kwa taswira ya Abuja/
Sauti gonga hoja/
Naziguza idhara kufungua ibara/
Wanaojiita vinara,hawanivuti fikara/
Naisoma kemet, peo zinagusa piramidi za teth/
Nini mapokeo,kwa hivi vyanzo vya leo/
Vipi matoleo kukubali mamboleo/
Wanalinganisha mizani na usawa hauwiani/