Wimbo: Hawa Watu
Toka kwa: Jemedari ft. Juveh
Albam: Single
Tarehe iliyotoka: 20.01.2021
Mtayarishaji: Juveh
Studio: Kali Sana Studios

Jemedari

Kiitikio:

Hawa watu *3/
Wanatubeba ka mafala hawa watu/
Wanatuona vichwa mala hawa watu/
Sijui ni nini sisi hufuata hawa watu/

Hawa watu *3/
Ni kitu gani wamekupa hawa watu? /
Wana ulafi juu ya pupa hawa watu! /
Wanakula wanatuacha na mifupa hawa watu!/

Beti Ya Kwanza:

Tumezaliwa tukiabudu hawa watu/
Kwa society imependa kusujudu hawa watu/
Ushuru wako unaruzuku hawa watu/
Na pesa zikipotea mbona hamshuku hawa watu?/
Makanisani tunapisha hawa watu/
Pale kwa kiti cha mbele, karibisha hawa watu/
Tukimaliza tunaombea hawa watu/
Kisha wapewe nafasi ya kuongea hawa watu/
Tunakanyaga kugotea hawa watu/
After kuchapwa na solar ukingojea hawa watu/
Mnakatishwa maji na hawa watu/
Na mtaani mmekatiwa maji, si nyi mafyatu?/
Kwa mtandao mnasifu hawa watu/
Mtanitusi juu mimi nakashifu hawa watu/
Nyi hupewa nini na hawa watu?/
Yaani mpaka hamjiamini, mnaamini hawa watu?/

Beti Ya Pili:

Ee Mungu nguvu yetu inaliwa na hawa watu/
Na dada zetu wanaliwa na hawa watu/
Na mali yetu inaliwa na hawa watu/
Nacheki ni kama hawatoshekangi hawa watu!/
Hutajiriki kwasababu ya hawa watu/
Na Kenya haikaliki sababu ya hawa watu/
Ukipata, inatolewa ushuru na hawa watu/
Vipofi na viziwi? Hawajali hawa watu!/
Kuna boyz amepigwa risasi na hawa watu/
Akabebwa ka gunia la viazi na hawa watu/
Sheria inafaa kutulinda na hawa watu/
Inafanya tunazidi nyanyaswa na hawa watu/
Itabidi muanze soma ufala ya hawa watu/
Waache kutuona vichwa mala hawa watu/
Juu ile siku we can see how they be, hawa watu/
Itabaki wametii hawa watu/