Binafsi nilianza kuona kazi za Vichwa Vya Habari (VcW) kwanza kwa kupitia kazi waliyofanya pamoja na producer Abby MP wa Digg Down Records. Kutoka kwenye mradi wa Abby Heshima singo ya kwanza Dhamira iliwashirikisha ma emcee toka VcW.
Kilichonivutia haswa kando na uchanaji kwenye wimbo huu ni pia artwork iliyoundwa ki ustadi. Kutoka hapo nikaanza kufuatilia kazi za VcW hadi nikafanikiwa kuwasiliana na mkurugenzi wa VcW bwana Jeremy.
VcW inajihusisha na mambo kibao ikiwemo ubunifu wa artwork, kuandaa matamasha na pia wana wasanii waliosajiliwa chini ya kampuni hii ya sanaa.
Leo nimepata fursa ya kufanya maongezi na Jeremy ili kufahamu mpango mzima unaoendana na uendeshaji wa VcW.
Karibuni sana!
Karibu sana kaka Jeremy hapa Micshariki Africa. Kwanza kabisa tuanze kwa kukufahamu, unaitwaje kwa majina kamili, unatokea wapi na ujihusisha na nini ?
Ahsante sana Mr Kefa, wana Micshariki na hip hop community. Naitwa Jeremy Tumgonze Evans, natokea Arusha na mimi nina deal na masuala ya project management, marketing, ila nafanya graphic designing na pia ni content creator.
Vichwa Vya Habari mnajihusisha na nini na jina hili lilikujaje?
Vichwa Vya Habari tunajihusisha na sanaa ya muziki kama wasanii wa Hip Hop, Trap, Rnb, ila kuna Hype Men, Djs and Music producers na break-dancers. Tuna operate as a music group ila pia as a record label. Mwanzo kabisa idea ya Vichwa Vya Habari ilikua ni wimbo wa kurekodi, ila tukai upgrade idea zaidi na kuwa music group. Wimbo ulifanyika ila mpaka leo haujawahi kutoka.
Japokua hamfahamiki sana kwenye vyombo vya habari handakini kuna vitu mnafanya kule ambavyo wenye macho wameviona na kuvitambua. Tueleze mmewezaje kulifanikisha hili?
Kikubwa tunafuata mission na vision na goals tulizojiwekea toka mwanzo, maana vitu hivyo vinasimama kama dira au miongozo ya kufanikisha malengo yetu tuliyojiwekea.
Nimeskia baadhi ya kazi zenu kwanza kwa kupitia mradi wa Abby MP, Heshima. Je wewe unachana au mlihusikaje kwenye mradi huu ?
Mimi sichani ila ni muandishi, lyricist. Kama muanzilishi wa Vichwa Vya Habari, nahusika moja kwa moja katika utekelezaji, upitiaji, uhakiki, kutoa ushauri na muongozo wa project zote za label yetu.
Nimeona mojawapo ya huduma mnazotoa ni Artist Management. Je hili linafanya kazi huku bongo ambapo watu wengi wanapenda kufanya kazi wakiwa huru? Tueleze kidogo kuhusu vile mnavyofanya shughuli zenu kuhakikisha sio tu msanii bali hata nyinyi mna nufaika kwenye maelewano haya
Artist management ni moja ya vipengele muhimu katika kumpa artist guidance na kurahisisha shughuli zake kwa maana ya mgawanyo wa majukumu. Ni professional work kama kazi nyingine kama project management kwenye mashirika au NGOs. Msanii hanufaiki yeye tu manake ukiwa artist manager unakuwa muajiriwa wa msanii, kwamba msanii anakulipa ili uweze ku manage shughuli zake ikiwa ni ziara, interviews, PR, marketing, endorsement issues, concerts, collaborations, appointments na mambo mengine mengi ambapo msanii kusimamia yote hayo kwa wakati mmoja inachosha sana.
Ikumbukwe tuu kwamba kuwa manager wa msanii haimaanishi manager amewekeza kwa msanii kama ilivyozoeleka hapa bongo.
Artwork za VcW ni ya viwango vya juu sana. Nani hufanya shughuli za artwork kwa niaba ya VcW na je mlifanikisha vipi kuweza kuandaa artwork nzuri hivi?
Artwork zote za Vichwa Vya Habari zinafanywa na mimi, kama nilivyoeleza hapo awali. Mimi ni graphic designer kwa hiyo jukumu hili nalisimamia mwenyewe. Kikubwa ni kuweza kuwa na ubunifu na maono ya kutengeneza kazi yenye utofauti na nyingine zilizozoeleka.
Vichwa Vya Habari pia naona ni record label. Je mtu akitaka kufanya kazi na nyinyi utaratibu ukoje ? Je kwa sasa ni wasanii gani wanafanya kazi chini yenu? Anayekuja kwenu kwa nia ya kufanya kazi na VCW anatakiwa awe na vigezo vipi?
Mtu akitaka kufanya kazi na sisi kikubwa ni maelewano mazuri baina ya pande zote mbili yakiwa yanazingatia kila pande kunufaika na fursa zilizopo, yaaani win-win situation, then baada ya hapo tunakuja kwenye agreement (oral or written).
Kwa sasa wasanii wanaofanya kazi chini ya VcW ni Experience, yupo Zungu Pori, yupo producer High Smoke, yupo Francopollah, yupo Tryphone, yupo Gypsie, yupo Polonium, D One, Seven Diss, yupo pia na Magneto.
Kigezo kikubwa cha kufanya kazi na VcW ni nidhamu in general, kwa maana nidhamu ya kazi na nidhamu kwa wengine wakubwa kwa wadogo, awe focused yaani awe na malengo, na pia talent iwepo.
Mimi binafsi nimefurahishwa na viwango vya kazi zenu ki mziki na upande wa artwork. Mnawezaje kuhakikisha kuwa viwango vya kazi zenu vipo juu kila mara?
Ahsante sana. Ni kujitahidi kuwa bora na tofauti kila mara kwa kujifunza kila siku vitu vipya.
Vichwa Vya Habari pia inasemekana ni Content Creators na Event Managers. Hebu tueleze kuhusu hili na pia tupe baadhi ya kazi zenu mlizozibuni pamoja na matamasha mliofanikisha kuyaandaa.
Mwaka 2017 tulifanya concert ya kwanza chini ya African Music Now ambayo ni label ya msanii nguli wa hip hop tanzania Mr Chindoman. ?Concert ilifanyika Arusha Via Via. Team ya Vichwa Vya Habari ilisimamia mradi wote ukaenda sawa.
Vichwa Vya Habari pia iliweza kufanikisha kuundwa kwa Arusha Open Mic iliyokuwa inaongozwa na mwana hip hop mashuhuri kutoka Arusha kwa jina la JCB.
Vichwa Vya Habari pia iliunda campaign ya #VomRapChallenge. Haya yalikuwa ni mashindano ya ku rap ya mwaka 2020 ambapo mshindi aliibuka na kitita cha shilingi millioni moja za kitanzania.
Mwaka jana 2021, Vichwa Vya Habari ilisimamia #VomDanceChallenge yakiwa ni mashindano ya dance ambapo mshindi pia aliibuka na kitita cha Shillingi za kitanzania milioni moja.
Mpaka sasa VcW mmeshatoa miradi mingapi na wasanii gani nikiwa na maana ya EP, Mixtapes au albums? Je kazi zenyewe zinapatikana wapi?
Mpaka sasa tumekwishatoa Ep ya Nyenza Emcee inayojulikana kama Overdose yenye nyimbo nne. Ep inapatikana kwa kutuma Tsh 5,000/= tu za kitanzania kwenda namba 0743 884 065 (Mpesa) na kisha utatumiwa mradi wako aidha kwa njia ya email, WhatsApp au Telegram.
TeHaMa ni muhimu sana kwenye ulimwengu wetu. Nyie kama VcW mmefanya nini kuhakikisha kua hamuachwi nyuma na kuwa mnaenda na wakati? Je kazi zenu mmeziweka kwenye platform za mziki kama vile Boomplay ?
Tunatumia Tehama zaidi katika usambazaji wa kazi zetu, kupitia mitandao ya kijamii kwa kutumia hizi music distribution platforms pia kufanya networking. Kazi zetu nyingi zinapatikana kwenye platform za YouTube, Audiomack, Bandcamp, Mdundo na Immiter. Tupo kwenye mazungumzo na Boomplay ili kuweza kuweka kazi zetu huko pia.
Tofauti yenu VcW na hizi kampuni nyingine za miziki nini?
Kikubwa ni mission yetu ambayo imejikita kwenye kuinua na ku support muziki na vipaji zaidi kuliko kutanguliza matamanio ya mafanikio ya kipesa kwanza. Kitu ambacho huleta migogoro miongoni mwa wahusika na wadau wengi. Tunaamini misingi ikiwa mizuri hata mafanikio ya kifedha kwa msanii yatakuja kirahisi zaidi.
Tutarajie nini kutoka kwa VcW hivi karibuni ?
Escape album inakuja mwezi wa February. Escape ni album ya Experience iliyosheheni vichwa nguli wa Hip Hop Tanzania, wakali wa Rnb, Soul na traditional African music.
Ushauri gani unao kwa yoyote yule ambaye angependa kujitosa kwenye tasnia ya mziki iwe ni producer, msanii au hata promoter?
Kikubwa ni uvumilivu, bidii na kutokukata tamaa. Ukizingatia haya ipo siku kazi yako itaonekana na utapata recognition na hata mafanikio ya kifedha pia.
Ni kipi cha mwisho ungependa kutuambia ambacho sijakuuliza ?
Labda naomba niongeze tu kwa mtu yoyote atakayependa kufanya project na sisi atucheki kwa namba 0743 884 065.
Iwe ni kufanya music project, kutengeneza singles and collabos, project and artist management, media promotions, kutengeneza events au campaigns, artwork, kutengeneza logo for t-shirt printing, networking, kubadilishana uzoefu na kadhalika.
Nashukuru sana tume cover yote yenye umuhimu na uzito kwa uzuri zaidi.
Shukran sana kwa kukubali wito wetu wa kuhojiwa.
Shukrani sana wana Micshariki na wana handaki wote, tuendelee kusukuma gurudumu letu hili la sanaa ili tufike mbali zaidi. Ahsanteni sana.
Unaweza kuwasiliana na Jeremy kwa kupitia;
Instagram: jeremy_vcw
Instagram: vichwavyahabari