Jerry Mtata Kazini

Unapokuja kwenye maswala ya muziki ma producer huwa ni watu wanaosahaulika sana. Wengi wanaposkia muziki mzuri huishia kummwagia sifa muimbaji au mchanaji na kumsahau mtu aliyeweza kufanikisha ndoto za msanii huyo.

Leo kwa mara nyingine tumetimba studio ili kuweza kukutana na mtayarishaji mmoja mahiri ambaye japokua yupo chini ya maji midundo yake imeweza kupenya kutoka studio yake ya Soweto Records kule Kahama hadi kutufikia sisi hapa Micshariki Africa.

Simzungumzii mwingine bali ni Jerry Mtata ambaye kwa upande wangu amebobea katika utumiaji mzuri wa kinanda pamoja na kutumia sampuli vizuri wakati anapoandaa muziki wake. Karibuni ili tuweze kumfahamu mtayarishaji ambaye ni mwenyeji wa Sengerama, Mwanza ila kikazi anapatikana Kahama, Tanzania.

NB: Kama ungependa kuskiliza Podcast ya gumzo yapo mwisho wa makala haya.

Karibu sana Micshariki Africa kaka Jerry. Kwanza kabisa tuanze kwa kukufahamu unaitwaje, unatokea wapi na ujishughulisha na nini?

Naitwa Jerry Mtata, ni music producer katika studio ya Soweto lakini pia najishughulisha na uuzaji wa nguo za mitumba hizi. Ni mwenyeji wa Mwanza, wilaya ya Sengerema, mtaa wa Soweto.

Soweto Records

Tueleze kuhusu jina lako la kazi, Mtata lilikujaje na lina maana gani?

Jina la Mtata ni jina kama mengine ila kidogo lina historia yake. Nakumbuka nilikua Form 5 shule flani mkoani Manyara. That day nilikuwa nimetumiwa hela na mzee wangu so katika purukushani za kutoroka shuleni niende nikachukue hela mjini nikiwa natembea nikamuona mwalimu mkuu msaidizi wa ile shule. Ilikuwa ni kosa ukionwa uko nje ya fence ya ile shule otherwise uwe na permit. So nakumbuka nilipomuona yule teacher nika pretend kama nilikuwa nafanya jogging, nikakimbia, nikakimbia, nilipofika dormitory nikageuza tena, nika pretend kama bado nafanya mazoezi kidogo, nikampita kidogo nikageuka tena nikarudi. Ile ya tatu ile ndio nikawa nimepitiliza moja kwa moja hadi town.

Baada ya kuwa nimetoka town tuko pale prep ile usiku ndio nilikuwa naongea na washikaji zangu, kwamba daah, mwanangu leo nimekutana na huyo mwalimu mkuu sasa. So katika kupiga story story jamaa wakasema mwanangu imekaa kitata hiyo, mwanangu mtata wewe. So hiyo mtata ikawa kama jina limeanza kuwa linazoeleka sana kwa washikaji.

So from there nikaanza kuwa nalitumia lakini nilivyofika chuo ndio jina lilikua maarufu zaidi pia nilianza kuchana chana lakini baadae nikabobea zaidi katika kufanya beats.

Hebu tuambie kidogo kuhusu historia yako ya nyuma ya ki mziki. Ulianzaje hadi kufika hapa ulipo?

Kutopata content kutoka kwa producers by that time ndio kichocheo kikubwa ambacho kilifanya mimi nifkirie kuanza mziki na baada ya kuwa na idea ya kuanza kufanya mziki, nilipita kwa producers mbali mbali kama njia ya kuweza kuwa vizuri katika music production.

Binafsi nimeanza kuskia kazi zako kwenye mradi wa Wabeti, Ukubwa EP, kwenye wimbo Ukweli. Hapa ndio nikaona ubunifu wa midundo yako. Midundo yako unawezaje kuiunda kwa viwango vya juu ?

Actually nilifanya track ya Ukubwa ya Wabeti kama representation ya EP yote nzima. Kuhusu production yangu nadhani ni ubunifu plus hisia ndio kinachofanya kazi zangu zionekane ni za viwango hivyo ambavyo wewe umesema.

Hebu tueleze kidogo kuhusu Soweto Records. Umeajiriwa pale au wewe ndio mmiliki wa studio hii? Mbona ukaamua kuiita Soweto Records na kuiweka Kahama na sio Dar au mji wowote mkubwa ili muweze kuonekana na kujipatia soko zaidi?

Jerry Mtata au Mtata kama wengi mnavyoniita, mimi ndio mmiliki pekee wa studio hii ya Soweto. Iliitwa Soweto studio kwa sababu ya kuwakilisha mtaa wangu ambao natokea ambao ni mtaa wa Soweto.

Kuhusu kwanini tuliamua kuweka studio huku na sio labda sehemu nyingine kwenye miji mikubwa nafkiri sababu kubwa ni ndipo ambako tunapoishi.

Pale Soweto mnajihusisha na shughuli zipi? Na nyie mmejikita kwa mziki wa Hip Hop pekee au unaanda kazi za mziki tofauti na Hip Hop, iwe ni RnB, iwe ni ngoma za kitamaduni, ngoma za Lingala au kwaya au mmejikita kwa Hip Hop tu peke yake?

Soweto studio tumekua tukijihusisha na production ya muziki tofauti tofauti lakini project nyingi ambazo tumekua tukipata kutoka kwa kwa wateja wetu ni project za mziki wa Hip Hop.

Nilipotaka kuskiza kazi zako vizuri nilipopata EP ya Nyenza iendendayo kwa jina Overdose ambayo uliiunda asilimia 100. Midundo na viwango vya kazi vilikuwa vya juu sana. Hebu ongelea ubunifu wa midundo, inakuaje toka upate wazo hadi mdundo ukamilike?

Kitu kikubwa katika production ni kama nilivyoongea mwanzoni ni hisia. So nikizungumzia project ya Vichwa Vya Habari (VcW) iliyotambulika kama Overdose kweli ni EP ambayo nilifanya mimi mwenyewe na kilichosababisha iwe vile ambavyo umeskia nadhani ni chemistry kutoka kwa msanii aliyerap, Nyenza Emcee, lakini pia na uongozi wake wa Vichwa Vya Habari (VcW) coz pia walishiriki katika ku select baadhi  ya midundo ambayo mimi nilikua nimekwisha ifanya lakini beats nyingine ndio kama hivyo nili compose pale pale on the spot.

Kahama inapokuja kwa upande wa mziki wa Hip Hop je ipo kwenye ramani? Ma emcee gani wanapeperusha bendera ya Hip Hop kutoka Kahama?

Aaah tukizungumzia Kahama kuhusu ma emcee wa Hip Hop wapo wengi sana lakini waliofanikiwa kuwa kwenye Apex ni wasanii kama Nacha, Bad Ngundo, kina Papaa Frege na wasanii kama Jos P, ni wengi sana. Hao ni baadhi ya wasanii ambao wanawakilisha vyema kwa upande wa Kahama.

Kwa mfano akitaka kuja mtu kufanya kazi na producer Mtata ni vigezo gani mtu huyo anatakiwa awe navyo ili muweze kufanya kazi vizuri na kazi itokee yenye viwango vya juu?

Kigezo cha kwanza nadhani ni ile gharama ambayo tunaichaji studioni lakini cha pili ambacho ni cha msingi kabisa ni msanii yeye awe anajua anachokifanya ni kitu gani. So upatikanaji wa chemistry kati ya msanii na producer ndio kinachosababisha uskie kazi zinakua nzuri na zenye viwango vya juu.

Signature tune yako na ya kazi zako hua inasema " Soweto Records" ilikujaje maana kwa kazi zako nilizopata kuziskia signature tune hiyo ndio humtambulisha mtu kuwa hii ni kazi yako. Uliipataje pataje hii signature tune?

Idea ya signature au jingle ya Soweto Records ilikuwepo lakini kuna rafiki zangu ambao walikua wana NGO ambayo ilikua inapokea hawa watu wa kigeni na walikua wanafanya kazi hapa hapa nchini kwetu so nilibahatika kutembelewa na hao rafiki zangu wakiwa na hao wageni wao

So kuna dada mmoja alikuwa anaitwa Nicole, nadhani alikua ni raia wa Canada, so ndio aliweza kuweka hiyo signature au jingle na from there tukaanza kuitumia kama official jingle ya Soweto studio.

Mtata una uwezo wa kupiga chombo gani cha mziki? Je wewe mwenyewe unachana?

Nina uwezo wa kupiga kinanda. Kuhusu kughani nowadays sifanyi hicho kitu lakini nimekuwa nikiwasaidia wasanii kuwapa idea za chorus.

Kando na mziki Mtata unajishughulisha na nini ili kuweza kuweka msosi mezani?

Nje na music production ninajihusisha pia na uuzaji wa nguo za mitumba.

Wakati unapomuundia msanii wimbo ni nini kinatakiwa ili wimbo uweze kusema umekamilika vizuri?

Kikubwa hapa ni process yote ya utengenezaji wa mziki kua imefanyika vizuri. Hapa nazungumzia katika beat making, lakini pia beat hiyo hiyo kuwa imefanyiwa mixing vizuri lakini pia kwenye upande wa vocal kuwa imerekodiwa vizuri na ikawa edited vizuri.

Na finally ikawa hiyo ya mixing na mastering kuwa pia zimefanyika vizuri unaweza ukasema kua kazi imekamilika.

Kama unavyojua ma emcee wengi hawana shule rasmi ya kwenda kunoa vipaji vyao. Je producer hali ni ile ile au vipi? Je wewe mwenyewe ulienda shule rasmi ya mambo ya muziki ili kuweza kuboresha kipaji chako? Je kuna umuhimu wowote wa kujiongezea masomo hata kama umeshaiva vizuri kwenye udundishaji wako?

Maisha ya mziki ni process kwa maana kama unataka kuwa producer mzuri jitahidi atleast kila siku kuwa unaingiza kitu kipya katika kujifunza mziki.

So far kuna tutorials mtandaoni, kuna vitabu ambavyo vimeelezea concept mbali mbali katika mziki. So kwa kuzifahamu utakuwa umeongeza wigo zaidi wa kufahamu zaidi kuhusu mziki.

Kwenye maisha yangu ya kujifunza nilibahatika kukaa na watu kama akina Duke, nimeweza kukaa na producer kama Adolf Beats, nimekaa na producer kama T- Joe, Estino One, Shaky, Nice Flavor na wengine kibao.

Lakini urasmi nilikuja upata ilikuwa ni 2009, nilipata course ya miezi mitatu kutoka kwa jamaa mmoja kutoka New Jersey, United States (Of America). Yule ndio alinifungua katika ulimwengu wa music production na ndio nikaanza pia kupenda muziki zaidi.

Kwa shughuli zako za production wewe hutumia software na hardware gani ili kuweza kufanya shughuli nzima ya utayarishaji wa muziki?

Aah tukianza na software mara nyingi katika beat natumia sana FL Studio na kwenye vocal natumia Cubase.

Tukirudi kwenye hardware nina computer, natumia kinda//keyboard, speaker KRK Rocket 6 generation ya tatu, natumia soundcard 2y2, natumia headphone ya Focus Light, natumia microphone ya Scarlet.

Mtata na Soweto Records mnapatikana wapi na mtu akitaka kufanya kazi na nyie atawapataje?

Mtata na Soweto Studio tunapatikana Kahama, hapa maeneo ya Soko La Mkulima la zamani. Aah kwa mawasiliano unaweza ukatupata kwa namba +255 753 921 084. Lakini tuna
Email: sowetorecordstz@gmail.com
Instagram: Jerry Mtata
YouTube: Soweto Records

Ungetoa ushauri gani kwa mtu yoyote yule ambaye angependa kuzama kwenye shughuli za production ya muziki?

Ushauri wangu kwa mtu au watu wanaotaka kuingia katika music production, kikubwa kabisa ni kujifunza mziki at least uweze kuwa unapiga hata chombo kimoja cha mziki.

Na je kazi hii ya utayarishaji huwa inakulipa na pia gharama zako zikoje wakati unapofanya kazi na msanii kutoka kumtayarishia mdundo hadi pengine kumfanyia mixing and mastering?

Kuhusu kunilipa, binafsi mziki unanilipa. Gharama ambazo mimi nazichaji katika mziki na gharama kwa sasa studioni ni laki moja(100,000 Tshs) kwa project moja. Japo ni wachache ambao wanafika kwa hiyo bei walio wengi wanakomea kwa 80,000Tsh, 70,000.00Tshs kwa project moja.

Shukran sana Jerry Mtata kwa wakati wako nakutakia kila la heri kwenye shughuli zako za utayarishaji na mziki ki ujumla. Asante.

Skiliza Podcast ya gumzo hili hapa