Metadata tafsiri yake kwenye upande wa muziki ni taarifa zinazotambulisha wimbo iwe kwenye kifaa cha kusikilizia au kwenye majukwaa mbalimbali.

Taarifa hizo zinaweza kujazwa moja kwa moja kwenye file la wimbo ili mtu atakaposikiliza kwenye kifaa chake zionekane. Hapa unaweka taarifa kama jina la msanii husika, jina la wimbo, jina la mtayarishaji, album, mwaka wa wimbo kutengenezwa, mahadhi na ikiwezekana hata lyrics. Kwa kufanya hivyo husaidia mtu anaposikiliza wimbo kwenye kifaa chake iwe ni simu, computer na kwingineko aweze kujua kiurahisi.

Faida nyingine ni hata unapoweka kwenye majukwaa baadhi ya muziki hizi taarifa huwa zinatokea pia mfano Audiomack, wimbo ukiwa na taarifa zake inakua rahisi ukiwa unapandisha… unaweza usiandike hata maelezo ya ziada. Unaweza kutumia software kama JetAudio kufanya hii kazi na ni nzuri zaidi kwa watoa miradi kama album, ep na mixtape.

Tuje kwenye majukwaa ya muziki sasa, hapa ndio kimbembe kipo. Wengi wanapenda ku complicate kwa kutokujua kanuni za kujaza taarifa/maelekezo kuhusu wimbo.

Twende moja kwa moja YouTube, unapojaza taarifa kuhusu wimbo au mradi flani yafuatayo ni ya kuzingatia:
- Ikiwa unatoa video rasmi unatakiwa uweke jina la msanii na jina la wimbo na specification yaani “Jina la msanii - Jina la wimbo (Official Video)” unaweza weka pia “Official Music Video” hapo ukipenda.
- Ikiwa ni audio rasmi unaweka jina la msanii, la wimbo na specification yaani “Jina la msanii- Jina la wimbo (Official Audio)” unaweza weka pia “Official Music Audio” ukipenda.
- Ikiwa ni lyrics za wimbo unaweka “Jina la msanii - Jina la wimbo (Official Lyric Video) au unaweza weka “Lyric Video”. Hapa kuongeza neno music description inakua ndefu zaidi na haina mantiki kwa upande wangu.
- Ikiwa ni visualizer unaweka “Jina la msanii - Jina la wimbo (Official Visualizer) au unaweka “Visualizer” tu.

Kutumia mchanganyiko wa maneno mengi kwenye description ya wimbo mfano “Official Music Lyric Video” ni kutokujua. Unatakiwa uwe specific sana unapoelezea.

Kitu kingine ni matumizi ya herufi kubwa, hyphen/dash na mabano ni kuwa makini navyo. Mfano huu hapa chini,

Fivara - Wakala (Official Video)
Fivara - Wakala (Official Audio)
Fivara - Wakala (Lyric Video)
Fivara - Wakala (Visualizer).