Toka kwa: K Voo
Nyimbo: Uhuru
EP: Africa Revolution
Tarehe iliyotoka: 07.12.2019
Waunda mdundo: Rama Genius, Bin Laden
Studio: Killers Record, AJ Records
Vesi 1
Nimeikumbuka amani iliyokuwepo mwanzoni/
Tunapaswa kuwa deep kuunda kikosi nyomi/
Mbio za sakafuni zimeishia ukingoni/
Tumechoshwa na Ubaguzi wenu faida sizioni/
Kupata na kukosa yote kwetu ni kheri/
Tunategua mabomu na hatuwezi kufeli/
Manyanyaso mmevuka mipaka wazungu wa meli/
Napingwa na wajinga sababu ya kusema kweli/
Fikra za mapinduzi tuungane, jitambue/
Nachimba chini kwa dhati dhumuni tujikwamue/
Soma kurasa chambua kwa kina ili ugundue/
Nawalaani wanyonyaji hamna jipya nyie ngurue/
Uzao wenu unaendeleza dhambi kama kawa/
Upeo mpana uweledi ni mbinu maridhawa/
Simnyenyekei Mjerumani kama Chief Mkwawa/
Africa yangu naibeba begani mimi ni mzawa/
Natoa maoni kitu gani kifanyike/
Hatuombi misaada tumeamua tuwajibike/
Wameandaa mipango ili tusambaratike/
Wajibu wetu kuwafukuza wazungu watararike/
Vesi 2
Nafichua vilivyofichwa hizi tungo mizizi/
Wakija kwetu watalii tukienda kwao wakimbizi/
Nawakamua wakoloni majipu siulizi/
Wakati wa ukombozi ni sasa zama hizi/
Wafalme wakitenda kisicho haki nichukizo/
Watu wanauwawa kwa njama za mfululizo/
Miyeyusho isiyo idadi ubabaishaji nashuhudia/
Round hii nawachana kuliko kupindukia/
Mapambano ni makali makamanda tusilale/
Wapumzike kwa amani manguli wote wa kale/
Ujuzi wa maarifa taarifa kuhusu wale/
Tunahitaji uhuru hatuhitaji mtutawale/
Japo sayari inaongozwa na abmepari/
Ushawishi unatengenezwa kwa wigo kila mahari/
Mwisho sasa umewadia kabisa ni zamu yenu/
Mmesahau mnajiachia hii Africa sio yenu/