Toka kwa: Kaa La Moto Ft Salu Tee, Chapatizzo
Nyimbo: Malenga
Album: KESI
Producer: Sango
Mchanganya sauti na vyombo: Chzn Brain
Tarehe iliyo toka: 15.07.2019
Vesi 1
Siko hapa kudhania,Mada imejengwa kiimani,
Watakuja kujutia, msaada kutengwa njiani,
Wazugaji wametanda, vilemba vingi vichwani,
Ustadi umevikwa Sanda, ukilega hatuelezani,
Umagharibi umetuganda, wahenga hawajulikani,
Uhasidi ujuzi 'kusanda', Malenga hawatamanwi,
Wachafuzi 'wamemanda', walengwa hawatazamwi,
Wanafunzi wanatamba, kutunga hakuna thamani,
Wakufunzi wanachambwa, vina kunga ya zamani,
Eti makuzi ya kijanja, kujiunga na burudani,
Upuuzi na kujigamba, chunga Bara mpaka Pwani,
Hamna ufundi wa kupanga, hadhara haioni fanani,
Madhara ya Gundi 'visanga', hasara na uayawani,
Wanazuoni wachanga, masihara hawatofautiani,
Wasomi wasiojipanga, busara imekosa Fani,
Usomi usiokwasika, ufukara wa mizani,
Utunzi usioaminika, ishara yao utani,
Hawajifunzi kuandika, vinara wao mitaani,
Malenga amesahaulika, kwa dhiki na mitihani,
Kalenga hakufaidika, riziki yake shakani,
Mwanafundi anahitajika, hazisikiki Diwani,
Elimu haina masika, ingawa haishiki hewani,
Muhimu kuhamasika, tujizatiti nyumbani,
Ushairi ukisikika, wataitafiti hii Medani...