loader

Kamusi ya Kitaa – Tanzania

Msamiati Maana
Ankara/Mpunga/Mchele/Mawe Pesa
Banda Umiza Kibanda cha kuona video/mpira
Bati/Jiti Mia moja (100)
Bi Mkubwa Mama
Biere Beer
Boya/Ree/Mbulula/Ndezi/Maandazi/Nyumbu/Soro Mjinga au Mshamba au Fala
Cha Arusha/ Jani la Kondeni Bangi
Chozi(La simba)/Kidosi/Nyonjo/Nyeupe/Gongo Pombe kali ka mtaani
Chuma ulete Uizi wa kutumia "remote control" sana sana kwenye maduka
Danadana Kupepeta mpira na mguu au mtu kukuchezea kwa mfano anakupa tarehe ila kila mara anahairisha
Danga Slay Queen
Diko/Madiko diko Chakula
Dingi Baba au Jamaa
Fanya maajabu/Fanya mazuri/Fanya Uislamu Kumsaidi mtu ki fenya, kumuinua mtu ki fedha
Gadange/Inchaji Mtu mwenye uwezo au cheo
Gambe/Nyagi Pombe
Jax, Muamala,KibundaMarundo/Ma Apple/Mboga Pesa
Jero/Jeva/Shiva Mia tano (500)
Jiwe/Pini/Pumbu/Katusha/Busha/Bonge la dude/Bonge la ngoma Wimbo mkali au wimbo noma
Kabobo/ Kupiga soundi Stori isiyo na mbele au nyuma au ya uwongo na ukweli
Kaki/ Dansi Alfu tano (5000)
Karume Mia mbili (200)
Kichupa Video kwa mfano kwenye YouTube
Kiepe Chips
Kinuke mwanangu Fanya kweli mwanangu/amsha mwanangu/twende mwanangu
Kiroba/Nyau/Kinyau Pombe kali sana
Kitu/Dope/Cha Jamaica/Bob Male Bangi
Kua mwani au kufuria Mtu alie filisika
Kubugi Kukosea
Kubugi Kokosea
Kubuma/Kujamba/Kubounce/Kukwama/Kudunda Kufeli
Kubwaga manyanga Kupoteza fursa
Kuchanganya ma faili Kujichanganya
Kuchomoa betri Kufanya jambo liharibike au kuharibika
Kudandiwa/Kuisha/Kudakwa/Kudabwa Kukamatwa
Kufinya/Kubota/Kupiga menyu au kupiga diko/Kufida/Kulumbua Kula chakula
Kuibuka/Kutokea/Kutimba Kuja
Kuingia choo cha kike Kufanya kitu tofauti na kawaida au kinyume na utaratibu
Kukipika/Kufokea/Kuchana sana Ku rap vizuri sana
Kula buyu/Kula bati/Kuvunga/ Kunyamaza
Kulewa Tilalila/Kulewa nyakanya Kuleta hadi kutojielewa
Kumchimjia mtu baharini Kumsahau mtu au kumpoteza mtu
Kumuingiza mtu usiku - Kumchanganya mtu
Kung'aa/Kuoga Kupendeza
Kunyoa/Kupiga/Kugusa/Kukaza/Kupiga Kipara/Kupita Kufanya mapenzi
Kunyonga/Kutoa/Kuunda Kuanda bangi kwa ajili ya kuvuta
Kuparangana/Kupambania kombe Hali ya kutafuta maisha, kutafuta ugali
Kupiga mtumtama Kupiga Mtu Ngwala
Kupiga nondo Kuinua vyuma gym, dumbbells/barbells
Kupigwa changa la macho/Kupigwa kipapai Kufanyiwa mazingaumbwe
Kupigwa doro Kuboeka au kukosa cha kufanya, umekaa tu
Kupofua Kuiba mafuta
Kuunga/Kuchangia Kusaidi mtu na pesa
Kuuziwa mbuzi ndani ya gunia Ku koniwa au kupata kitu tofauti na ulicho tarajia
Kuvesha Kufanya anasa tofauti tofauti
Kuwaka Kulewa
Kuwaka Kuchukia na kuongea kwa hasira
Kuzengua Kusumbua
Kuzima Kupoteza Fahamu
Kwea Pipa Kupanda ndege
Kwere Noma
Lele/Kabobo Kubonga
Lomoni Maneno Mengi
Magwangwala Mawe yanayo kua na dhahabu
Matimba Uongo
Mboga saba/kishua Maisha mazuri/ Familia bora
Menu Chakula
Mia/100% Kitu kikiwa poa kabisa au kama siku imeenda poa - Twasema mia!
Miwili Alfu mbili (2000)
Miyeyusho/Mzinguaji Mtu anaesumbua
Mjeda/Bakabaka/Msoja/Soja Mwanajeshi
Mkia Makalio ya mwanamke
Mnenekwa Mlala hoi
Mori Mzuka
Motema/Mamiloo/Mama La Mama/Shori/Mchuchu Msichana/Demu/Manzi/Mke/Mchumba
Muwa/Tungi/Vyombo/Kimea(Beer)/Gambe/Nyau(Pombea Kali)/Mitula Pombe
Mwewe Ndege ya kusafiria
Niko bomba/Baridi/Niko Full/Mzuka Niko freshi
Nyero/Kanyero Noma au tatizo
Pai/Poti/Mwera/Ndata/Mzee(Wazee) Polisi
Pamba Nguo
Pango Chumba cha kupanga
Shuka la kimasai/Teni/Nite/Mwekunda/Msimbazi Alfu kumi (10000)
Sistaa/Sisteri Dada
Uani Chooni
Unanipiga kamba/unanijaza/Unanileta Unanidanganya
Utuo/Ubaoni/Umwerani Polisi
Wa Mee/ Wa Mbuzi Ujambazi
Wangoni Waizi
Wese au Zutu Mafuta ya gari
Wese/Zutu/Pofo Mafuta ya gari
Zimba/Kifaru Tajiri
1. Shujaa2. Watoto Na Michezo3. Asili Halisi4. Zoeza5. Moja Nyingi6. Unao7. Sio Poa8. Baraka9. Iqra