Ukaguzi Wa EP: Zimelia
Msanii: Kay Wa Mapacha
Tarehe iliyotoka: 15.11.2021
Nyimbo: 6
Watayarishaji: Wise Geniuz, Sigger
Mixing & Masteting: Wise Geniuz
Studio: AMG Studioz

Nyimbo Nilizozipenda: Nipo,Maisha Yangu, Zimelia, Struggle Za Kila Kona Asante, Inatosha,

Kay Wa Mapacha

Mwaka wa 2021 Mapacha kando na kutubariki na machata yao tofauti walizama studio na kutubariki na miradi ikiwemo EP moja nzuri toka kwa Kay iitwayo Zimelia. Mradi huu ambao umesimamiwa china ya usimamizi wa Wise Genius pale AMG Studio ni mradi mzuka sana.

Kay anatufungulia mradi huu na wimbo flani safi sana unaoitwa Nipo. Kutoka uchanaji, mashairi na unataji wa mdundo pamoja na kuimba mwenyewe kwenye kiitikio Kay anakuonesha kwa nini yeye ni veteran kwenye hili game na kuwa bado hayupo tayari kustaafu kwenda kula shushu. Wimbo huu pia umetumika kama soundtrack kwenye filamu ya BongoHoodz iitwayo Tapeli.com. Kay Anachana kwenye wimbo huu kwa majigambo kuhusu uwezo wake na kuwa bado yupo kwenye game. Wise Genius kaua sana kwenye mdundo.

Maisha Yangu ndio wa pili kwenye mradi huu na ni wimbo mzuri sana ambapo Kay anafungua pazia ili tuuone moyo wake na tuweze fahamu kuhusu matarajio na malengo juu maisha yake kwenye vinanda flani vizuri toka kwa WG. Kay anasema,

“Upendo wa Mungu/
Kujua ukweli pesa sio kila kitu/
Nawapenda ndugu/
Mtu mwenye uthubutu/
Wivu chuki sitamani cha mtu/
Nachagua moja sio kukaa patupu/
Napenda kusoma staki kukaa mbumbumbu/
Nitanue upeo niwe kachaa adimu/
Mitaa inanijua mi ni kifaa muhimu/
Napunguza kula miwa sifa za kijinga/
Nafkiria maisha njia gani nitapita/
Nafkiria future muda gani umepita/
Yalopita yamepita kuna mengi nimeficha/”

Zimelia akimshirikisha Lugombo MaKaNTa ndio wimbo uliobeba jina la EP na wimbo huu ni kama muvi flani ambapo wawili hawa wanashirikiana kwenda kuchukua hela kwa ulazima na ubaya! Sauti za mitutu, risasi na mabomu zinaskika kwenye kiitio wakati Kay akikuambia lengo ni ku Get Money ki J.U.N.I.O.R M.A.F.I.A.

Wimbo wa nne kwenye EP hii ni Struggle Kila Kona akiwa na Magazijuto kabla ya kwenda kwenye wimbo wa tano ambao ni Asante akiwa na Mfalanyombo(Trump MC).

Kwenye Asante WG anatubariki na mdundo mzuka wenye bass gita flani nzito ambayo itakosha moyo wako wakati utakaposkia ma emcee hawa wakitoa shukran kwa Mwenyezi Mungu na Hip Hop kwani maisha yao yamebadilika tangu wakutane nae. Vinanda vinapiga freshi sana na kwenye kiitikio Kay anatoa muhtasari akisema,

“Asante (Kwa kua pamoja nami kwenye kipindi cha hussle)/
Asante (Umenipa talanta umenipa kipato)/
Asante (Umenifanya ninga’re jina langu lipae)
Asante (Nyota imewaka umenifanya ning’ae)”

Inatosha akiwa na Geoff Master ndio wimbo pekee kwenye mradi ulioundwa na producer mwingine tofauti na WG. Sigger anachukua doria hapa na kuwapa hawa wawili mdundo flani old school wakati Kay akitema nyongo kuhusu mahusiano yake na mpenzi wake yalivyokwenda mrama. Geoff Master anabariki wimbo na kiitikio kizuri sana. Japokua wimbo unasikitisha emcee huyu ana mistari flani ukiskia unamuonea huruma ila unacheka kwani unaona vile mapenzi yanaweza kugeuza ukawa mwehu. Kay anachana,

“Nikawa nagombana kwa sababu za kifala/
Mtu wa vurugu hadi kwa watu wa mtaa/
Wakiniambia ukweli nikawa nakataa/
Wakiniambia nina stress bado na kataa/
Moyo ulikua unawaka kama moto wa mkaa/
Nikawa sioni raha ya kuishi kwa mtaa/
Akikosea yeye mi naomba msamaha/
Hata nikiwa na yeye bado moyo nauhadaa/
Akawa hanitaki mi nalazimisha/
Akawa anacheka mi nakasirika/
Nikiwa na yeye ndo moyo natulia/
Kumbe alikua hanitaki keshapata mwingine/”

Mcheki Kay Wa Mapacha ili uhakikishe speaker zako Zimelia.

Wasiliana na Kay Wa Mapacha;

Facebook: K Wa MaujanjaSaplayaz
Instagram: kaymapacha
WhatsApp: +255 713 233 203