Wembe ni ule ule
Wagawe kisha watawale
Wachanganye
Waletee udini waletee ukabila
Leta propaganda wakose kabisa dira
Wanao ongea ongea warubuni kwa kuwahonga
Wakikataa wape vikwazo vya kiuchumi na wakiendelea kupinga washushie kimbunga
Wape elimu duni
Ili wajikatae wajione ni sifuri duniani
Waambie amani ni kutokuwa na vita kabisa
Ili watulie hata sharubu zikitikiswa
Kila siku watengenezee matatizo kisha watatulie
Ndio utabaki kitini milele
Jinadi kuwa chama ndio nguvu ya wananchi
Na bila siasa hatuwezi ishi
Waambie vyama vingi ndio demokrasia
Ilihali vingine vinasindikiza na vinashambuliwa
Ingiza virusi kwenye media na sanaa
Wote wawe wanakusifia
Pendelea ndugu zako
Nafasi kubwa weka ukoo wako
Aah mguu sawa
wana mguu sawa
Unangoja nini chukua hatua
Utapotezewa muda hadi lini macho fumbua
Ingawa hakuna kwa kwenda kusemelea
Haiimaanishi ndio tushindwe kuyaongelea
Kwenye chumba cha tiki siwezi ingia
Maana tunawapa dhamana lakini wanatugeukia
Utaambiwa njagu ni usalama wa raia
Utaambiwa hakuna aliye juu ya sheria
Hapo hapo naishia
Ukitaka mwenyewe malizia
Sitaki kutengeneza tena gurudumu lililokwisha tengenezwa
Natengeneza duara langu kuepuka kumezwa
Kuepuka kukimbizwa
kila siku ni siku ya kujifunza
Kama kuepuka kodi ningeweza
Nadhani haya yote ningemeza
Au ndio upendo unaniongoza
Najaribu tu kuwaza
Mizani ime balance au imeegemea upande fulani?
Ridhaa na uvumilivu ni kwenye vitu ambavyo kuvibadilisha haiwezekani
Tosha tu kuelewa vinavyo endelea ulimwenguni
Kella B: “Mguu Sawa”
Subscribe
Login
0 Comments