Kevi_Artz

Mitandao ya kijamii ina nguvu sana na inaweze kukupa kila aina ya connection unayotaka. Micshariki Africa tukiwa mitandaoni hua tunatafuta connections za Hip Hop na sanaaa ili tuweze kujifunza kutoka kwa watu husika alafu tukawaleta wahusika wenyewe kwenye jukwaa letu ili wasomaji wetu waweze kuwafahamu, kujifunza kutoka kwao na ikiwezekana kuwapa michongo inayoweza kuwafanya jamaa hawa wakapata rizki zao.

Mitaa ya Twitter ndipo nilipokutana na mwana sanaa wetu wa leo Kevi_Artz. Kev anapatikana Dar Es Salaam na amejikita kwa michoro yenye uwezo wa kuonesha uhalisia wa mtu kama alivyo.

Karibu sana Micshariki Africa kaka Kevi_Artz. Kwanza kabisa tuanze kwa kukufahamu kaka, majina yako rasmi, unatokea wapi na unajihusisha na shughuli gani?

Kwa majina naitwa Kelvin Jumanne Kazimili, msanii wa uchoraji wa picha za uhalisia kwa kutumia pencil na peni ya wino (bic).

Kaka Kev tueleze kidogo kuhusu historia yako; ulizaliwa wapi, mpo wangapi kwenye familia yenu, ulisomea wapi na utoto wako ulikuaje kiujumla? Pia tungependa kufahamu uligunduaje kua unakipaji cha uchoraji na umewezaje kukikuza hadi ukawa stadi kwenye mbanga hizi?

Nilizaliwa Mwanza ila makazi yangu ya sasa ni Dar Es Salaam. Mimi ni mtoto wa pili katika familia yetu na nilisoma shule ya msingi Islamiya na nikamalizia sekondari shule ya Kimandolu iliyopo Arusha, Kijenge juu pia. Baada ya hapo nikaingia Chuo Cha Mipango, Mwanza.

Nilianza kuchora nikiwa primary, kuchora kwangu ilikua ni kama kitu kinacho nipa furaha na kujivunia sababu nilipata marafiki wengi kupitia kuchora na pia marafiki hao ndio walio nifanya nijitambue kama nina kipaji kwa sababu mwanzo nilifanya kama majaribio kwa kuchora picha za kwenye vitabu. Pia baadae nikaanza kutumia picha za kwenye magazeti na saa zingine nilikua nawachorea walimu picha ubaoni.

Nilipenda kuwaonesha marafiki zangu kazi zangu na hapo wengi walizikubali na nikaanza kukubali uchoraji nilipo maliza shule ya msing kabla ya kusoma shule ya sekondari Kimandolu nilianzia kidato cha kwanza shule moja inaitwa Sunrise  iliyopo Mwanza, Pansiansi na nilikutana kwa mara ya kwanza na wachoraji wanao fanya vizuri zaidi ambapo walinifanya nami nihamasike zaidi, alafu kitu nilicho kipenda katika shule iyo ingawa ilikua haina somo la uchoraji ila uchoraji ulikua na nafasi katika shule hiyo.

Kulikua na magazeti ambayo wachoraji walikua wakiyatengeneza kwa kuandika kwa pencil na kuchora katuni kitu ambacho kilikua kinafanya uchoraji upendwe zaidi katika shule hiyo. Wanafunzi walipenda kusoma katuni hizo ambazo zilikua ziki husu story zinazoendelea, shule za michezo na vitu mbali mbali ambapo magazeti hayo pia yalikua yakitoa mafunzo, ila nilikuja kuumwa so sikumaliza katika shule iyo nilikuja kuhamia shule nyingine inaitwa Bidii.

Shule hiyo mambo yalikua yamekaza na nilikua sipati mda mwingi wakuchora ila nafasi ndogo kwangu ilkua kama fursa. Baadae niliwapa wazo wachoraji wa shule hiyo kuhusu magazeti ya shule hapo nilipo hamia. Wachoraji wengine walipenda nikaenda nao kwa mwalimu kupeleka wazo ilo walimu wakakubali nikaanza kuchora magazeti kama ya wale wachoraji wa shule nilio toka. Nilikua na rafiki zangu ambao wenyewe walikua ni kunipa story za shule na mimi nikawa nachora tu. Baadae nikaja kuhamia Arusha kidato cha pili ambapo ndio nilimaliza sekondary nkaingia chuo, O Level.

Huko sikua nikichora picha kwa uhalisia kwasababu mitandao nilikua sjaanza kuitumia hivyo sikuwai kuwaza kama mtu anaweza kuchorwa picha ya uhalisia. Nilivyo ingia chuo nilikutana na mchoraji anaitwa Hashim. Mchoraji huyo alikua amenizidi hivyo alinionesha watu anao wafuatilia mitandaoni ambao wana muamasisha, kwa mara ya kwanza niliona picha za ualisia kupitia Instagram sikuweza kuamini ila nilivyo ona videos ndio nikatamani nami nije niweze kuchora picha zenye uahalisi.

Wakati ulipokua unaanza uchoraji na pia sasa pengine akina nani walikupa au wanakupa motisha ya hiki unachofanya?

Watu walio ni inspire sana Obed Artz (TZ), Arinze (Naija), Kelviokafor (London) nimekua nikifuatilia kazi zao zikawa zinanipa nguvu ya kujitafuta. Kupitia sanaa hii nimejiajiari mwenyewe na ndio kazi pekee nayo fanya inanipa kipato cha kuendesha maisha.

Nimeona sehemu kua unajitambulisha kama "Hyperrealism artist". Hapa unamaanisha nini, tafadhali tufafanulie kidogo.

Napenda kutumia neno hyperrealism ambalo linamaanishani aina ya uchoraji unaofanana na picha ya ubora wa juu.

Ni kazi gani ulioifanya ambayo unaipenda sana na ambayo hukupa tabasamu sana ukiiona?

Mchoro nao upenda ni ambayo nimemchora mtoto wa mjomba kama ana sali na kuupa jina la "Give us our daily bread" nikimaanisha “Tupe mkate wetu wa kila siku”. Mchoro huo naupenda kwasababu nikiuona ni kama unanihimiza nikumbuke kusali.

Changamoto zipo kwenye kila aina ya kazi, zako ni zipi na unakabiliana nazo kivipi?

Nimekua nikitumia mitandao kutangaza biashara zangu changamoto mwanzo ulikua mgumu kwa sababu sikua na mtaji mzuri wakununua vifaa husika na pia vifaa kwa Tanzania vilikua adimu ila niilitumia uwezo wangu na vifa nilivyo kua navyo kuhakikisha kazi zinakua vizuri. Kidogo kidogo nilianza kupata wateja mitandaoni ingawa wengi hawakuniamini kwa sababu mitandao imekua na matapeli wengi so nilihakikisha na weka na video nikiwa nachor. Kuna watu walianza kuniamini na kuvutiwa na kazi na hawakujali umbali wa mkoa au nchi. Kila mteja nilihakikasha kazi yake ameifurahia. Kuptia mmoja mmoja mteja nilipata connection za marafiki zake.

Je mtu akitaka kujifunza kwako unatoa darasa na gharama zako zipoje? Pia inapokuja kwa gharama za kuchorewa hua unalipisha shilingi ngapi?

Gharama zangu ni kulingana na aina ya mchoro na ukubwa wa mchoro, ila kwa picha za order A4 nafanaya laki, A3 laki mbili, A2 laki mbili na themanini, A1 laki nne na sabini.

Sanaa na muziki ni kama mapacha, wewe unapokua unapiga kazi hii hua unaskia muziki gani?

Sanaa na muziki zinaendana napia hua nkifanya kazi napenda kusikiliza Hip Hop na Reggae. Hua najiisi nipo katika sayari nyingine kwenye mazingira haya.

Unaongeleaje mchango wa serikali zetu kwenye sanaa yetu. Je nini wafanye ili kuweza kuhimiza jamii kuikubali sanaa kama ajira?

Serikali ningependa watusaidie kuanzisha tuzo za kila mwaka kwa ajili ya sanaa pia kama wanazo weka kwenye muziki wa Tanzania. Tuzo hizi zingesaidia kufanya vijana waweke juhudi ya ubunifu katika kazi zao.

Pia unapatikana wapi kwenye mitandao ya kijamii?

Mitandaoni napatika kama;

Twitter: keviArtz
Instagram: Kevi_Artz
Facebook: kevi_artz
YouTube: kevi_artz