Mtayarishaji Killo Pound lazima ataukumbuka sana mwaka huu wa 2022 siku za usoni kwani ndio mwaka ambao ulionesha hatua anazopiga kama mtayarishaji. Fidelis Steven Killo kama anavyojulikana rasmi ambae ni mzawa wa Kilimanjaro mwaka huu kando na kuandaa singles kadhaa ameweza kuachia album yake ya kwanza akiwa na emcee Hechi Hucho na pia ameweza kuwapiku watayarishaji wenzake katika shindano la midundo ya Boombap iliyo ratibiwa na Action Music Academy chini ya usimamizi wa mtayarishaji Black Ninja toka Boom Bap Clinic.
Tuliona ni vyema kumtafuta mtayarishaji huyu ili tuweza kuskia mawili matatu kutoka kwake kuhusu safari yake ya utayarishaji pamona na ushindi wake.
Karibu sana Micshariki Africa na hongera kwa kujinyakulia taji la mdundishaji bora kwenye shindano lililoandaliwa na Action Music Academy. Unajiskiaje baada ya kuibuka kama mdundishaji bora kwenye tuzo hili?
Kwanza na mshukuru Mungu kwa kuibuka mshindi wa tuzo ya mdudishaji bora lakini pia ni jitihada zangu pekee ambazo zimenifanya ni weze kuibuka mshindi.
Tuanze rasmi sasa kwa kukufahamu kaka Killo Pound; majina yako rasmi, unatokea wapi na unajihusisha na nini?
Kwa majina kamili naitwa Fidelis Steven Killo. Mimi ni mzaliwa wa Kilimanjaro. Najihusisha na music production, kwenye upande wa kutengeneza beat na ku mix vocal kwa ujumla.
Tueleze kuhusu historia yako ya muziki; ulianzaje safari imekuaje hadi ulipofikia kwa sasa?
Historia yangu ya muziki ilianzia shule ya secondary Morogoro Mjini. Nilikua napenda sana ku rap nyimbo za Hip Hop haswa za Marekani kama vile za Lil Wayne hadi baadhi ya marafiki zangu wakawa wananiita Lil Wiz.
Mbona unajiita Killo Pound, jina lilikujaje na lina maana gani?
Jina la Killo Pound nilipewa na rafiki yangu mganda. Nilisoma Uganda miaka miwili. Sasa wakati nikiwa naenda kutoa pesa za Tanzania nikibadili kuwa za kiganda nilikua napata pesa nyingi. Nikiwa na rudi shule rafiki yangu akawa ananiita Killo Pound. Ni kweli wa Tanzania tulikua tuki change pesa tuna matambo kidogo. Hahaha, watoto tena ni shobo tuanaita pound. Pound nika sema hili jina mbona kama lina sound vizuri? Tokea hapo nikajipa jina hilo la Killo Pound.
Hivi taarifa za shindano hili ulizipataje na ulifanyaje hadi ukafanikiwa kusepa na taji?
Taarifa nilipata mtandaoni kwa sababu nilikua nimepita chuo cha cha muziki cha Action Music Academy kwa mdaa wa miezi miwili ila baadae nikapata changamoto ya fees nikaacha nikaamua kujitafuta studio za wanaa nikabahatika kupata studio so nikaendelea kujifunza mdogo mdogo hadi nikiwa producer mzuri.
Kusepa na taji ilikua ni lazima kwa nilikua nasikiliza muziki wa Hip Hop wa Marekani tokea nikiwa mdogo hivyo loop sense ya midundo ilikua tokea nipo mdogo na ilikua rahisi kuwa piku wenzangu. Wakati wa mashindano mimi ndio nilikua mtu wa mwisho kushiriki na niliona makosa ya wadundishaji walio pita walikua wahawezi kubalance beat so mimi nikachukulia point zangu hapo.
Je mashindano kama haya yanaongeza tija yoyote kwenye game la Hip Hop la Africa Mashariki?
Ndio yana ongeza tija kubwa sana kwani sio rahisi kutafuta wadudishaji kwa urahisi. Pia yana waleta ma producer kwa pamoja ili kuweza kubadilishana ideas kama siku ya shindano. Ma producer wengi walikuja kuhudhuria na ilikua ni fursa pia kwa wadudishaji wapya kuonekana na kufahamiana na wenzao.
Je wewe umejikita kuandaa midundo ya Hip Hop peke yake au unafanya kazi na yoyote yule hata kama ni wa sebene, rnb na hata singeli?
Hapana kwa sasa nafanya beat za aina yote Hip Hop, RnB na pia Afro Beats, Drill na Trap.
Killo Pound unafanya wapi shughuli zako za utayarishaji? Je una studio yako mwenyewe au una mkataba na studio unapofanyia kazi?
Mimi nafanyia kazi 24 Record ambayo ina patikana Mwenge, Dar es Salaam ila sina mkataba kwani bado tuna pambana kujitafuta.
Nini kinacho mtofautisha Killo Pound na mtayarishaji yoyote yule?
Killo Pound ni producer tofauti sana na wengine na midundo yangu ni tofauti sana ukiitofautisha na ya wengine kwani ukiisikila vizuri una weza ukasema na toka majuu kumbe ni bongo tu. Choping na cutting zangu kwenye sample ni za tofauti sana.
Inapokuja kwa miradi umeshaanda miradi na wasanii gani na miradi yenyewe ni ipi?
Mradi wangu wa kwanza niliandaa mwenyewe ambao unaitwa No More Discussion nikiwa na Hechi Hucho ila pia kwa upande wa singles nimefanya na wasanii kama vile Nepo Nova, Magozi na Pido Mox. Pia kuna mradi nilianda na Bill Balla. Kuongezea pia ni kua kuna mradi bado haujatoka na no EP ya Hechi Hucho, mimi ndio nilifanya mix ya vocal inaitwa Tantana. Pia kuna ngoma nimefanya na Odong Odowa haija toka.
No More Discussion album yenu pamoja na Hechi ilikua moto sana. Huu mradi ulikujaje na je mapokezi kutoka kwa mashabiki yalikuaje? Hii kazi hamkumkaribisha mtu yeyote mwingine ilikua Killo Pound na Hechi tu, mbona mliamua hivi?
Mradi wa No More Discussion ulikua una mpango wa kuwashirikisha wasanii wengi ila ikatokea changamoto ya baadhi ya wasanii wali kua mbali kutokana na majukumu ya kimaisha so Hechi ndo alikua free na mimi nilikua na mdaa wangu nisha tenga nika ona ngoja tu kill me na mwanangu Hechi Hucho
Nashukuru mapokezi yalikua mazuri japo kulikua na changamoto ya mauzo ya direct selling, sikuweza kuuza nakala sana nikaamua kuuweka Audiomack na nimefanikiwa kupata streams 1k so nijambo jema kwa hatua hii ya kwanza.
Kando na kua mdundishaji je unafanya shughuli gani zingine ili kuweza kujiongezea kipato?
Kwa sasa na deal tu na music production sina kazi nyengine ni muziki tu.
Kama mtayarishaji unalizungumziaje swala la heshima kwa watayarishaji kwenu nyie, je watu wanathamini mchango wenu kwa game la Hip Hop?
Heshima tuna pata ila sio tunayo stahili kwa sababu game la Hip Hop. Tuna supporti na ku push kazi ila kwa kipato bado ni kidogo ndo maana game pia linaenda kwa speed ndogo na sababu pia ni uwekezaji mdogo.
Hivi nani humfanya mwenzake aonekane emcee au mtayarishaji?
Emcee ni emcee tu kabla ya mdudishaji, msanii paka anakuja studio ana kua yupo full ki vina ila akija studio ndo kuna sheria tu za kumnyoosha awe emcee mzuri.
Ni wadundishaji gani unawakubali hapa Africa Mashariki?
Duke Tachez, Black Ninja, Black Beat
Gharama zako za kazi zipoje mtu anapotaka kufanya kazi na wewe?
kwa beat moja ni 70,000Tshs kwa upande wa vocal pia ni 70,000Tshs so nikama laki na arubaini hela za kitanzania lakini pia kuna maongezi.
Una ushauri gani kwa chipukizi yoyote yule anaetaka kuwa mtayarishaji, msanii au mchoraji?
Ushauri wangu ni kupenda kitu unachokifanya na pia kujifunza kila siku kwa sababu music industry ina badilika kila siku na ni vizuri kusikiza wenzako wanafanya nini ili uweze kuleta ubunifu mpya kwenye game.
Unapatikana wapi kwenye mitandao ya kijamii?
Natumia jina la Killo Pound kwa mitandao yote tofauti na Tik Tok ambapo natumia Killo Pound Tz.
Una neno gani kwa ajili ya mashabiki zako na waandaji wa shindano la udundishaji la Action Music Academy lililo ratibiwa na Black Ninja?
Mashabiki zangu na omba support yenu muendele kuunga mkono harakati za muziki ili tuweza kupata waandaji wengi wa ududishaji. Pia pongezi nyingi ziende kwa Black Ninja kwa kuratibu na mchongo mzima.
Shukran sana kwa mda wako na kila la heri kwenye mishe zao.
Wasiliana na Killo Pound kupitia;
Facebook: Fidelis Steven
Instagram: killopound