Vesi 1
Kwa jina naitwa muda/
Muda wote natembea kwa kuwa sina kituo kama uda/
Oyah ning'ang'anie kama ruba/
Nikikuacha sisimami hata ukiongea kila lugha/
Usipokwenda na mimi huwezi kuwahi michongo/
Na pia ngumu kutusua hata kama una usongo/
Ni ukweli sio uwongo/
Kama hunifati hupati unachotaka hata ukitoka nje ya bongo/
Walionifata wamepata mafanikio/
Ila wale waliodata ni waliotaka kunizidi mbio/
Walioniacha nikaenda zangu wamebaki na kilio/
Sasa wewe twende sawa ili maisha usiyaone sio/
Ila nakupa tahadhari/
Usikubali kunichezea ukinipoteza ni hatari/
Mi ndo werevu wananiita mali/
Ila elewa kuwa sina rafiki kwenye hii sayari/
Vesi 2
Leo nimeamua kuongea na wewe kindugu/
Japo kuwa miaka yote nilikuwa kimya kama bubu/
Toka kwenye ukungu/
Nifate acha kukariri huwezi eti wanaoweza wazungu/
Mi nipo kwaajili ya watu/
Wote walio hai ila sipo kwaajili ya wafu/
Tukienda sawa sisiti kukupa shavu/
Leta ubishi usinifate kama hujabaki kwenye nyavu/
Waliopoteza ni walioniona sina mpango/
Kwa tahadhari tu tegesha alarm kama chambo/
Unaevaa saa kama pambo/
Unachekesha, utabaki kuendeshwa kama mtambo/
Utapata kizunguzungu/
Kama hunifati hata ukikesha kama sungusungu/
Huu ndio ukweli chukuchuku/
Nyuma sirudi labda urudishe kumbukumbu tu/
Vesi 3
Napata tuhuma/
Nyingi kutoka kwenu/
Zinazodai kwamba sina huruma/
Nahisi sababu hakuna wa kunisukuma/
Niende mbele au mwenye ujanja wakunirudisha nyuma/
Ukishindana na mimi utajuta/
Najua umeshasikia kuwa wakakati ni ukuta/
Unaomba nirudi nyuma wafu si watafufuka/
Na nikienda mbele we unayeomba si utakuwa umekufa/